Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Dah sijui ingekuwaje endapo tungekuwa uhusiano. Nimehuzuni sana.

Toka hapo kwa mama yako wewe pumbavu
Umeelekezwa vizuri unaleta ubishi maandazi kama unaona unayajua sana kakae kwako uishi utakavyo. Mbwa mshenzi
Kwa kumtukana na kumuita mbwa na wewe utajiita una imani kweli??
 
Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako..ila wewe hapo unatengeza tu ushuhuda..sauli ndo alikua mbane lakini alipo kutana na Simba wa yuda mmhhh...alipondwa pondwa akafinyangwa finyangwa mengine Ni historia,am done.
 
Kuelekezwa sijakataa. Kama anataka anihubiri na kunielekeza ni sawa. ila sio kunilazimisha.
Kwenda kanisani sio jambo la shurti.
Kwa jinsi ulivyoweka hoja yako na jinsi unavyoitetea inaonyesha wewe kijana una uwezo mkubwa sana wa kiakili, kuchambua mambo na kusimamia unachokiamini. Pamoja na kwamba kama mzazi najua kwa nini mama yako anafanya afanyavyo, lakini bado narudia kusema uko very intelligent. Wengi humu hawatakuelewa kwa sababu ya mazoea ya namna jamii yetu inavyofikiri na kukariri mambo. Ushauri wangu kama nilivyosema hapo juu jaribu kwenda makanisa ya zamani ROMA, Lutheran etc ili uone na pengine utashawishika. Sasa ukiachana na hoja yako iliyoko mezani mimi sijui umesomea nini lakini huko mbele ya safari utakuja kuwa very potential, hasa kama kiongozi, ni nadra sana kuona vijana wa leo wenye misimamo, kujiamini na kusimamia wanachokiamini.
 
Ongezea fungu lingine kutoka kitabu kingine kilichoandikwa na mtu mwingine ambaye hakujui na wala hatakujua wewe mmatumbi.
And when Our clear revelations are recited unto them, they who look not for the meeting with Us say: Bring a Lecture other than this, or change it. Say (O Muhammad): It is not for me to change it of my accord. I only follow that which is inspired in me. Lo! if I disobey my Lord I fear the retribution of an awful Day.

10:15
 
Asante, Nimegundua Athiest wengi ni critical thinkers maana hawana institution au dini yoyote inayowasaidia kufikiria...Ninashangaa hapa hata watu hawafikirii nje ya box. Yani wanafikiria ndani ya box la dini zao tu.
ila ajabu ningesema mimi naamini uislam mama analazimisha niende kanisani. Ungeona wanavyojaa kunitetea.
Hapa ishu ni mimi kuwa athiest ndio maana wananipinga.

Yani hizi dini zimefunga sana akili za watu.
Je umewahi kufikiria kwenda kwenye imani ya dini ya Kiislamu?
 
Ikifika Jumapili wewe zuga tu kwamba unaenda kanisani,ukiamka asubuhi jitayarishe Kisha chukua Biblia yako na utoke ujifanye unaenda kanisani...ukifika huko njiani fanya diversion uingie kijiweni ukapige story na Wana ama uende kwenye movie😂
 
Ongezea fungu lingine kutoka kitabu kingine kilichoandikwa na mtu mwingine ambaye hakujui na wala hatakujua wewe mmatumbi.
And when Our clear revelations are recited unto them, they who look not for the meeting with Us say: Bring a Lecture other than this, or change it. Say (O Muhammad): It is not for me to change it of my accord. I only follow that which is inspired in me. Lo! if I disobey my Lord I fear the retribution of an awful Day.

10:15
 
Kitendo cha kwenda ili anione ni thamani kubwa sana nmempa. Maana kiuhalisia sipendi hata kwenda hayo maeneo.

Na nachat kwasababu sioni cha kugain hapo kanisani, kila hubiri nlishasikia na hiyo biblia naijua kuliko wachungaji. Na hata nikisema niwaulize maswali hakuna atakayechomoka.

Na hizo laana unazosema mimi siziamini.
Aiseeee [emoji23] [emoji23]
 
Mmh sawa, sikuile nilitaka kumpasha na kumchenjia pale sebuleni...ila nikaona mama yupo haitokuwa sawa.
Wala huna haja ya kumkaripia, labda kama alikwambia kwa njia ya kukushushia heshima ila kama aliongea politely wala huna haja ya kumkasirikia.
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Nimeishia tu kwamba una miaka 24, sioni haja ya kuendelea kusoma,


Jibu;
Wewe siyo mtoto, hivyo siyo sahihi kulazimishwa mambo ya imani, wanatakiwa wakushauri kwa busara.
 
Niko na mzee, ila mzee hana time na haya mambo,...mama ndio anashupalia.

Vitabu ni vingi sana, kwasababu nilipokuwa form 2 nilikuwa na passion sana na dini. Yani ile tunaenda prepo wenzangu wanasoma physics mimi nilikuwa nasoma dini kila siku, so asilimia 80+ ya prepo zangu from form 2 to form 5 nilikuwa nasoma dini tu.
Vichache ni kama
Old & New testament
Heaven is for real-Todd turpo
The case for christ-Lee strobel
The attributes of God-Arthur Pink
Systematic theology-Wayne Grudem
The desire of Ages, The great controversy-Elen G. white
Catechism of the catholic church-
Roman catholic Encyclopedia karibia zote nilizisoma maana zilikuwa library shuleni
Here I stand-Maisha ya Martin Luther
Faragha ya kiroho, ukuaji wa kiroho-somebody Meinard Mtitu
Za wachungaji wa kibongo ndio usiseme
Vya kina mwakasege, Deo Njeni, na wengine wengi ambao hata sasa sivikumbuki majina

Vile vya ushuhuda kama nililala nikaamka usiku Yesu akanichukua akanipeleka kuzimu na mbinguni, nilishasoma vingi mno.
Ndiyo maana nilisema hapo juu huyu kijana ni very knowledgeable, wengi humu hivyo vitabu, kama kweli umevisoma, hawajavigusa au wanesoma vichache sana, na sababu kubwa ni kutopenda kusoma na kujielimisha. Ndiyo maana kwenye arguments hapa utaambulia matusi, kejeli na mambo ya kufuata mkumbo tuuu..
 
Mi natamani sana nipate mdada mwenye akili kama huyu, mwenye uwezo wa kutafakari.

Umenifurahisha sana, una akili na nzuri zaidi ni hiyo avatar ya mirabel, watu wanaongalia animation movies wana akili nyingi
Hakuna mke hapo kama anabishana na mzazi wake wewe atakusikiliza?
 
Hata hio 0.000000001% tayari kuna imani ndogo juu ya uwepo wake, Yesu alisema imani ndogo mfano wa punje ya haradali unaweza fanya mambo makubwa mno, sasa hio sio completely zero, imani yako ndogo hio imepelekewa na sababu zipi?
God could be there, Im not saying God is there.
Understand the differenece
 
Jehanam ipo kwa ajili ya wanao kaidi, na paradiso ni kwa ajili ya wanao tii UKO HURU KUCHAGUA mahali upapendapo,
Kama Jehanam ipo waambie waniongezee kuni, waichochee kabisa.
Nyie ndio mnaamini kuna Babu chrismas na Popo bawa?
 
Nilitegemea aina hii ya makanisa. Nina swali je umewahi kufikiria kwenda yale makanisa kama ROMA au Lutheran? I mean yale makanisa ya zamani ambayo tulikuwa nayo kabla ya haya ya mwendokasi??
Kuna tofauti gani kule?
 
Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako..ila wewe hapo unatengeza tu ushuhuda..sauli ndo alikua mbane lakini alipo kutana na Simba wa yuda mmhhh...alipondwa pondwa akafinyangwa finyangwa mengine Ni historia,am done.
Aah bro, Mimi sio Sauli
 
Back
Top Bottom