Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Huna imani na Mungu lakini Mungu yupo ndani ya moyo wako. Mara nasoma biblia. Akili gani sasa hizi
 
Sio tunachekesha. Hakuna hasara africa tunayo kama kubadili maisha yetu ya asili na kujifanya ni watu wa kisasa. Ukiangalia huyu wazazi walimchelewa. Hv hujiuliz kwanini ni watoto wachache wa kiarabu wanaishi tofauti na tamaduni zao? Sisi tumepoteana kuhc kila kitu ni usasa. Nina binti ana miaka 23 na ninakuhakikishia akiwa kwenye dari langu atafuata kila nilichoratibu aisee. Acha niendelee kuitwa mkuda tu.
Mtoto mwenyewee umemkutaa hajui kusimama na msimamo wake, ila sio mie, siishi kwa kumridhisha mtu. Never.

Na wazazi walishindwaaa kwangu tena had kwa kutumia watu wa nje. Lol
 
Una miaka 13 au 15,MTU mwenye miaka 24 hawezi kua mjinga hivyo,unamkosea bi Mkubwa sio kwa kotokwenda kanisani wala msikitini,kwa kutotii sheria zake alizojiwekea kwenye NYUMBA YAKE..Unamnyima raha kwenye NYUMBA yake ,why can't you just leave the nest Dada Mkubwa??why kubishana na mwenye mji??ulipo kua Chuo alikua anakulazimisha uende kanisani??chagua kuha
ma au nenda kanisani...kama waziri alivyo tuambia tutalipa kodi au tuhamie Burundi, sheria zipo hivyo hiyo...upo chini ya sheria zake
 
Viashiria vipi sasa vinakufanya useme kuna uwezekano Mungu yupo? Nilichogundua we ni mbishi na hutaki uweke mind yako iwe free kupokea mawazo mapya, may be unahisi tupo kwenye ushindani wa who is right and who is wrong, hata nikikuuliza kwa nini unahisi kuna uwezekano wa uwepo wa Mungu kama unavyosema utaanza kuleta siasa... Kikubwa umeomba ushauri, ushauri wangu nenda kanisani kama mzazi wako anavyosema kuhusu kusikiliza neno nni juu yako, unaweza kumlazimisha farasi kwenda kwenye maji lakini huwezi mlazimisha anywe maji m
Hakuna kiashiria chochote. Sema put in perspective, mwaka 1600 ungemuambia mtu kuna simu unaweza kutumia mawimbi kuwasiliana na mtu wa mbali akasikia.. angebisha, ila saivi ni kitu cha kawaida.
So I acknowledge kwamba huu ni ulimwengu wenye infinite possibilities, everything we know might be a very very small slice of everything there is to be known.

Lakini hii haimpi mtu lesseni ya kuclaim kitu chochote na kuforce tuamini kipo, eti kwakuwa 1960 hakukuwa na simu ndio leo useme in the future kutakuwa na watu ambao hawali ila hawafi tukaamini tu bila kiashiria chochote. Hatuwezi kukataa kwa asilimia 100 kwakuwa historia imetufundisha hivyo, lakini tutasema possibility ipo lakini tutakubali with certainity siku tukiona evidence.

Sio lazima uone kiashiria ndio useme kuna possibility ya kitu.

So even with God, currently hakuna kiashiria chochote wala ushahidi wowote kuwa yupo, Lakini naweka akiba ya kutosema hayupo kwasababu ulimwengu huu hautabiriki with certainity...Hata from the fundamental blocks of the universe (atoms, molecules, electrons) it is not predictable, it is probabilistic.

hata infinite multiuniverses could be possible, but not certain.

God could be there but not certain at the moment.

I am not anti-God, if he comes I will beleive, But currently he hasn't.
 
[emoji3][emoji3][emoji3] Hakuna tajiri ambae hana dini kacheki hata hao top 100.
Pili siendi kanisani wala msikitini, niliacha hayo mambo, even my father dont do that.
Lakini kwa uzoefu wangu mdogo, im above 35, i am educated. Nimeiona changamoto ya hiyo lifestyle.
To each his own, nilichotoa ni ushauri tu.
Sir Chande Freemason, lakini alizikwa kwa rituals za ki Hindu, Bob Marley na Jah wake mwishowe akarudi Roman Catholic akazikwa...Kingunge Ngombale Mwiru.
Kuna sehemu kasema wachina hawaamini Mungu, nikajua hata research simple tu hafanyi. Wachina na mambo spiritual ni wakongwe dunia hii, leo mtu anasema hawaamini uwepo wa Mungu/miungu[emoji847]
Swala la kutafuta taasisi ya kuzikiwa na kuamini kuna mungu ni vitu viwili tofarent.
 
Sio tunachekesha. Hakuna hasara africa tunayo kama kubadili maisha yetu ya asili na kujifanya ni watu wa kisasa. Ukiangalia huyu wazazi walimchelewa. Hv hujiuliz kwanini ni watoto wachache wa kiarabu wanaishi tofauti na tamaduni zao? Sisi tumepoteana kuhc kila kitu ni usasa. Nina binti ana miaka 23 na ninakuhakikishia akiwa kwenye dari langu atafuata kila nilichoratibu aisee. Acha niendelee kuitwa mkuda tu.
Maisha ya asili ya africa ni kusali rozali ya bikra maria wa vatican na kumswalia mtume wa Macca??
 
Imani ya kikristo inazalisha Aesheists wengi mno mna sio imani sahihi ndo mna wengi wasioamini Mungu wametokea huko kwenye ukristo

Am proud to be a Muslim
Wow, ni jambo jema la kupongeza. sikujua hili...Basi kumbe hii imani inazalisha free thinkers na sio watumwa wa akili.
 
Kupungukiwa imani ni tatizo linaletwa na usasa! Mama yako anakuelekeza njia iliyo njema. Sali sana uondokane na hako kashetani ka-usasa kalikokukamata.
Yeye usasa wake wa kuacha mila na tamaduni za kiafrica za kuabudu miti, mizimu, na kukimbilia usasa wa kuamini mila za wazungu na waarabu na dini zao unaona ni sawa eti?
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
upo wewe sahihi kabisa,mzazi hayuko sahihi na wala hajui kuwa hayuko sahihi,sasa dawa jitahidi utafute maisha uhame hapo haraka sana
 
Kwa sasa jamii imeharibika sana hasa kwa wanafunzi wa sasa mbaya zaidi hawa wanachuo baadhi yao siyo wote tena wachache tu ila ukibahatika kuwaona mara nyingi wanawabeza hata wazazi wao USHOGA UMEWAHARIBU SANA LESIBIANISM
 
Mtoto mwenyewee umemkutaa hajui kusimama na msimamo wake, ila sio mie, siishi kwa kumridhisha mtu. Never.

Na wazazi walishindwaaa kwangu tena had kwa kutumia watu wa nje. Lol
Ndio nakuambia walichelewa mi wa kwangu tangu akiwa mdogo nimemuivisha sana kwenye dini. Na kingine exposure sana. Mi wanangu nimewapeleka nje sana so nimewafundisha kulinda utamaduni wao coz hakuna jipya. Ndio watu watakuheshim.
 
Maisha ya asili ya africa ni kusali rozali ya bikra maria wa vatican na kumswalia mtume wa Macca??
Hayo unafanya wewe. Mi mlutheri na ni imani tu hiyo haibadilishi asili yangu kama mchagga. Mi sio mlutheri mmorden ni kama ukienda Japan ukakuta Mlutheri mjapan haiuondoi ujapan wake Chief. Kingine safir sana utapata exposure ya kutosha na unavyosikia mtu ana msimamo ni katika kulinda asili yake sio ya watu
 
Kwahyo kabla ya wazungu na usasa wao kuja Africa, wachaga walikuwa Walutheri?
 
Fanya hata kuuza nyanya uishi kivyako hayo yote utaepukana nayo.

By the way namuonea huruma sana mwanaume yyt atakayejichanganya kukuoa.

Tafakari kisha chukua hatua
 
Ongezea tena fungu lingine kutoka kitabu kingine kilichoandikwa na watu wengine ambao kipindi wanaandika walikuwa hawakufikirii wewe mmatumbi.
And when it is said unto them: Follow that which Allah hath revealed, they say: We follow that wherein we found our fathers. What! Even though their fathers were wholly unintelligent and had no guidance, would they follow them?
2:170
 
Kwahyo kabla ya wazungu na usasa wao kuja Africa, wachaga walikuwa Walutheri?
Elewa wazungu nao walipelekewa dini kama sisi tu lakin haijaondoa utamaduni wao. Ni kama mbuddist aliyeko India au Thailand na Japani hao wote ni dini moja ila tamaduni tofauti kabisa. Au ukienda Ethiopia wale waoptic wa pale na wale wa Misri ibada zao ni zile zile ila wanautamaduni tofauti. So muhim nikujigundua we ninan tu. Wazungu wenyewe hawana dini kwasasa kwa taarifa yako
 
Back
Top Bottom