Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Utayakumbuka majira haya na utayatamani na hutayapata.
 
Imani ya kikristo inazalisha Aesheists wengi mno mna sio imani sahihi ndo mna wengi wasioamini Mungu wametokea huko kwenye ukristo

Am proud to be a Muslim
Hii ni kweli hii , hizi ni takwimu za mwaka jana ukiristo umeporomoka vibaya mno mpaka kufika chini ya asilimia 50% katika nchi yenye wakiristo wengi kabisa .Na idadi kubwa wakikimbilia kwenye Atheism na Uislamu kwa kiasi fulani .Baada ya miaka kumi panapo majaaliwa inaweza ikafika asilimia 20% idadi ya wakiristo UK au pungufu zaidi.
IMG_20221209_174740.jpg

Screenshot_20221209_174926.jpg

Mimi naona Africa tu kwa sasa labda na American kusini kwa mbali ukiristo wafuasi hawapungui kwa kasi...

cc Execute ukikaidi utapigwa2 Stress Challenger che mitoga
 
Hii ni kweli hii , hizi ni takwimu za mwaka jana ukiristo umeporomoka vibaya mno mpaka kufika chini ya asilimia 50% katika nchi yenye wakiristo wengi kabisa .Na idadi kubwa wakikimbilia kwenye Atheism na Uislamu kwa kiasi fulani .Baada ya miaka kumi panapo majaaliwa inaweza ikafika asilimia 20% idadi ya wakiristo UK au pungufu zaidi.View attachment 2440858

View attachment 2440859

Mimi naona Africa tu kwa sasa labda na American kusini kwa mbali ukiristo wafuasi hawapungui kwa kasi...

cc Execute ukikaidi utapigwa2 Stress Challenger che mitoga
Dah mbaya sana...inaonekana Africa na America kusini bado wana akili mgando
 
Hii ni kweli hii , hizi ni takwimu za mwaka jana ukiristo umeporomoka vibaya mno mpaka kufika chini ya asilimia 50% katika nchi yenye wakiristo wengi kabisa .Na idadi kubwa wakikimbilia kwenye Atheism na Uislamu kwa kiasi fulani .Baada ya miaka kumi panapo majaaliwa inaweza ikafika asilimia 20% idadi ya wakiristo UK au pungufu zaidi.View attachment 2440858

View attachment 2440859

Mimi naona Africa tu kwa sasa labda na American kusini kwa mbali ukiristo wafuasi hawapungui kwa kasi...

cc Execute ukikaidi utapigwa2 Stress Challenger che mitoga
( وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ ۚ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا )

الإسراء (81) Al-Israa

Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!

Allah hajakosea
Time will tell
 
Weka fungu lingine tena kutoka kitabu kingine kilichoandikwa watu wengine kwaajili ya watu wengine ambao hawana undugu na wewe na kipindi wanaandika hawakuwa wanakufikiria wewe mmatumbi
 
Imani ya kikristo inazalisha Aesheists wengi mno mna sio imani sahihi ndo mna wengi wasioamini Mungu wametokea huko kwenye ukristo

Am proud to be a Muslim
Asilimia ya waislamu, hasa wanaoishi katika nchi inayotawaliwa na sheria za kiislamu, hawawez kisema kua hawaamini. Watabaki tu kua ile 'muislamu jina' ila sio waislam kama quran inavotaka muislam awe. Wakristo wao dini yao haina vitisho sana kwahio hawaogopi kusema sio waamin tena. Kuna wakristo jina pia.
Screenshot_20221209-193452_Google.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia ya waislamu, hasa wanaoishi katika nchi inayotawaliwa na sheria za kiislamu, hawawez kisema kua hawaamini. Watabaki tu kua ile 'muislamu jina' ila sio waislam kama quran inavotaka muislam awe. Wakristo wao dini yao haina vitisho sana kwahio hawaogopi kusema sio waamin tena. Kuna wakristo jina pia.View attachment 2440938

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakiruhusu dini iwe free, middle east yote itakuwa secular.
 
Wakiruhusu dini iwe free, middle east yote itakuwa secular.
Dubai wao since 2019 mpaka leo wameanza 'kulegeza' usilamu wao. Hakuna tena sharia law wala nn... nilikua kwenye kundi moja telegram na watu wa dubai, walikua wanashangaa jinsi Nigeria walivo wakali na sheria za kiislamu, wakisema kua hayo ni mambo ya kale...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia ya waislamu, hasa wanaoishi katika nchi inayotawaliwa na sheria za kiislamu, hawawez kisema kua hawaamini. Watabaki tu kua ile 'muislamu jina' ila sio waislam kama quran inavotaka muislam awe. Wakristo wao dini yao haina vitisho sana kwahio hawaogopi kusema sio waamin tena. Kuna wakristo jina pia.View attachment 2440938

Sent using Jamii Forums mobile app
Ata iyo ofisi unoyofanya kazi kuna miiko ya kazi ukiivunja you are fired
Sasa ije kua dini tena alotuletea Muumba wa mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo

Embu jitafakari tena kuisema iyo kauli
 
Weka fungu lingine tena kutoka kitabu kingine kilichoandikwa watu wengine kwaajili ya watu wengine ambao hawana undugu na wewe na kipindi wanaandika hawakuwa wanakufikiria wewe mmatumbi
Kwani umeambiwa ww ? M nimemwambia adriz sio ww
 
😀😀😀 Hakuna tajiri ambae hana dini kacheki hata hao top 100.
Pili siendi kanisani wala msikitini, niliacha hayo mambo, even my father dont do that.
Lakini kwa uzoefu wangu mdogo, im above 35, i am educated. Nimeiona changamoto ya hiyo lifestyle.
To each his own, nilichotoa ni ushauri tu.
Sir Chande Freemason, lakini alizikwa kwa rituals za ki Hindu, Bob Marley na Jah wake mwishowe akarudi Roman Catholic akazikwa...Kingunge Ngombale Mwiru.
Kuna sehemu kasema wachina hawaamini Mungu, nikajua hata research simple tu hafanyi. Wachina na mambo spiritual ni wakongwe dunia hii, leo mtu anasema hawaamini uwepo wa Mungu/miungu🤗
Mtoa mada ana uoni (upeo) hafifu. Mwepesi kuhitimisha masuala mazito bila ushahidi jadidi. Aibu!
 
Huyu jamaa amelelewa na single mother ndio maana anakuja kutusumbua huku, mzee huwa hasemi mara 2. Mara 1 usipoelewa utatembezewa bakora mapaka useme pooo

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
[emoji3][emoji3][emoji3] Hakuna tajiri ambae hana dini kacheki hata hao top 100.
Pili siendi kanisani wala msikitini, niliacha hayo mambo, even my father dont do that.
Lakini kwa uzoefu wangu mdogo, im above 35, i am educated. Nimeiona changamoto ya hiyo lifestyle.
To each his own, nilichotoa ni ushauri tu.
Sir Chande Freemason, lakini alizikwa kwa rituals za ki Hindu, Bob Marley na Jah wake mwishowe akarudi Roman Catholic akazikwa...Kingunge Ngombale Mwiru.
Kuna sehemu kasema wachina hawaamini Mungu, nikajua hata research simple tu hafanyi. Wachina na mambo spiritual ni wakongwe dunia hii, leo mtu anasema hawaamini uwepo wa Mungu/miungu[emoji847]
Elon musk mwenyew hana dini. (Haabudu mungu yyte)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo kama haya ndio huwa yanaonyesha ni kiasi gani watu wanamthamini Mungu wanae muabudu.

Katika Uislamu hii kesi ingetazamwa katika engo tofauti.

Ukiitaza vizuri hii kesi utagundua kuna mambo mawili.

1. Ni suala la mleta mada kutomtii mama yake, ambae anamuamrisha kumtii Mungu( kwenda kanisani)

2. Ni suala la mleta mada kumkufuru Mungu(kupinga uwepo wake).

Hapo kosa kubwa ni lipi?

Sasa badala ya kulinganiwa arudi kwenye mstari kwa kumrudia muumba wake, badala yake anakandiwa kwa kutomtii mama yake.

Ilhali kama atarudi kwenye mstari na kumtii muumba wake, basi automatically atamtii mzazi wake, maana ni amri kutoka kwa muumba wake kuwatii wazazi.

Ila kama ameamua kuwa atheist hivyo ajabu ipo wapi asipo mtii mzazi wake, ikiwa aliye muumba hamtii.

Kwani maatheist wanafuata muongozo gani?
 
Sijawahi kuona mtu anayesali na kuzingatia muda wa Shughuli nyingine asifanikiwe,rudia kusoma kuzingatia muda wa Shughuli nyingine.
Nimekaa na Ndugu zangu Wacatholic,Walutheri na Waislam wanaozingatia masaa ya ibada na kazi/masomo wanefanikiwa sana.
Ni jukumu lako kuchagua kumtumikia Mungu wa kweli au Kuishi Maisha yako.

Hii ni pamoja ya kuwatendea wema watu wote bila kujali undugu,ukabila,udini,kujitoa Kwa wengine na kusaidia makundi yote yasiyojiweza.
Kazi kwako.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Elon musk mwenyew hana dini. (Haabudu mungu yyte)

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa katika makuzi yake kakulia dini "evangilism", kajifunza sana na baadae kajifunza TM meditation kwa mujibu wa vyanzo vya mtandaoni. Na hakuna sehemu kasema hakuna Mungu. Pia kafikia level ambayo ana mambo yake kagundua mwenyewe. Huyu at 24 anakaa home halafu anawadindia😆😆. Kesho mfano akisema yeye ni member wa LGBTQ anaomba aeleweke kuwa ni haki ya kila mtu na jinsi alivyoumbwa🤗?
AKIWA KWAO AFATE SHERIA
 
Back
Top Bottom