Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mi
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Mimi nishawekwa mtu Kati ishu za kubeti na Maza afu kipindi iko na pisi yangu ilikuepo nyumbani inasubiri kujifungua, Sasa katika mazungumzo ya Mimi na bi mkubwa shemeji yangu mke wa bro akaingilia, ila shemeji kiukweli kubeti sio kuzuri😀😀 Sasa hasira zangu zote niliamishia kwake nilimmaind kweli kweli nadhan ananiogopa mpaka leo na nikamwambia ukiona naongea na bi mkubwa kaa kando, akaanza kulia nikiri kusema shemeji yangu mke wa bro Ni mtoto 🤣🤣🤣
 
24 yrs bado upo nyumbani unafanya nini? Ndiyo maana mama yako alikuambia wazi kuwa kama unaishi kwake utafuata anachokitaka kwa lugha nyingine alikupa ujumbe wa kuhama kwake.
Mimi nlitaka kuondoka lomgtime yeye ndo akang'ang'ania nikae hapa
 
Una shida wewe binti na hukuwa na haja ya kuweka uzi kama umepanga kudharau watu wanaojitahidi kukushauri...

Kitu naona kwako, wewe ni mtu mwenye ubongo ambao upo enclosed kwenye dimension moja pekee...

Mtu anayeshindwa kutambua uwepo wa mamlaka ya kiroho, ni kama boksi tupu lisilo na mali yeyote ndani yake...
Sawa, Asante.
 
As long as ulizaliwa nao ukuwakuta wanasali kanisan umekuwa bado wanasali kansan bas utaendelea hvyo hvyo had ujitegemee.
Ukiona sasa unataka jiondoa kwenye hayo, umrkua mtu mzima, kajitegemee.
Okay, gotcha.
 
Kukutana na kusali pamoja ni ustaarabu ukiwa na umri wa kuchambua mema na mabaya unaweza kumuasi Mungu hiyo ni stage I stage II utagundua kwamba Mungu ni msaada Kwa Binadamu.
Ni kweli wapo wachungaji nk WANATUMIA Dini kujipatia KIPATO Kwa kutumia neno la Mungu Kwa MANUFAA binafsi lakini hiyo haimaanishi Kwamba Hakuna umuhimu wa kusali.
Kuna umuhimu gani wa kusali?
 
Nani kakuambia sina uwezo wa kupambanua nipate chakula?
Hata kama basi tuseme sina, inamaana nikikosa huo uwezo basi automatically nakosa na uwezo wa kupambanua imani?
Mbona unalinganisha vitu ambavyo havilinganishiki?
Hivi dini imekula asilimia ngapi ya ubongo wako?
Usisahau huyo aliyekulea mpaka umefika hapo, ana imani yake ambayo wewe unaamini imekula ubongo wake. Unataka kutuaminisha kuwa aliyekulea ubongo wake umeliwa na dini LAKINI WEWE AMBAYE HUWEZI KUMLEA HATA PAKA UBONGO WAKO MZIMA..!!

We ukapimwe akili
 
Uko sahihi, kulazimishana dini ni mambo ya zama za kale za giza ila ki Africa utapata tabu sana kuishi na wazazi vichwa vigumu kama hao na pia wao ndio wataonekana wako sahihi kwa sababu Africa dini zimekita mizizi kuliko hata huko zilipotoka.
Suluhisho ni kwenda kuishi kwako mwenyewe.
Thanks, I got you
 
Okay, gotcha.
Mimi mwenyewe mambo ya kansani yashanipita kushoto siku nyingi, nina imani zangu binafsi ila unlike you mimi nina imani Munvu yupo ila sio in the way anavyoelezewa kwenye makanisa.
Ila nimeacha hayo mambo baada ya kujitegemea
 
kuna idea mbili tofauti hapa kwanza bado upo kwenu kwahiyo kibongo bongo lazima ufuate kanuni za hapo kwenu pili mara nyingi wazazi wengi wakiafrica huwa wanategemea hata kama mtoto ni mtu mzima ufuate yeye anachofikiria ni bora kwake hata kama wewe unaona hakina logic mfano kuna kipindi nilikua nimemaliza chuo na sikua na kazi ya kueleweka ambayo mzazi kwenye fikira zake aliona inafaa kulingana na elimu aiyoniseomesha lakini akawa haelewi kwamba ajira ni ngumu kwahiyo nikawa napiga vibarua hapa na pale siku moja kanifuata huko nilikokua nimepanga kaniambia twende kwa mganga akanifanyie zindiko eti nimerogwa niikataa na nikamsihi asiniambie kitu kama hicho tena. Kiukweli aliongea na kulalamika sana na kusema watoto hatusikiizi wazazi. Lakini point sio heshima ni kuangalia kama mtu mzima kipi unaona kinakufaa na kipi hakikufai.

Tatu naona watu humu wanatoa uhusiano wa kuharibikiwa na kwenda kanisani ni mawazo yakushangaza maana kuharibikiwa ni tabia ya mtu na maamauzi na hapa hakuna mungu wala shetani anaweza kubadili tabia ya mtu ndio maana leo hii dini kila kona ila mambo maovu yanaendelea sadly wengine wafanyao ni hawa hawa wanaoshinda kanisani.

Ushauri kwenda kanisani sio jambo baya we nenda imani ya mtu ipo moyoni mwa mtu fanya kama mambo yoote tuliyofanya utotoni ili kumfurahisha mzazi mfano kupretend kupenda taarifa ya habari na huku unamiaka 6 hujui hata kinachoongelewa ni nini, au kujifanya unasoma masaa sita huku uwezo wako ni masaa mawil ili tu mzazi aone unasoma kwa usongo kila mtu humu jukwaani kapretend. Sio idea mbaya just do it wont hurt.
Thanks, nitafanya hivi
 
Mada yako umeileta ya nini ikiwa unakataa ushauri unaopewa na wengi? Tatizo ni kwamba unajiona una uelewa sana kuliko Hawa wote wanaokushauri,...



Nje ya mada kidogo,
Hakuna mwanaume mwenye akili timamu anaweza kuoa mke wa namna kama yako
Huyo nilimwambia hajitambui. Kwanza kaja kuomba ushauri alafu anataka kubishana na washauri.
 
Mara useme wewe kwake ni mtoto, hapa tena unasema we ni mtu mzima uliezidi 18 yrs.
Ama kweli muwamba ngoma huvutia kwake.

Hilo jambo lako kama jamii haijakifunza basi huwa tunasoma life skills pale form 1 , ukikikosa hicho kipindi basi utasoma parsonal hygiene and good manners hapo hapo form one.

Kama unaona maza anakosea hama hapo ukakae kwake, wewe ukiwa kwako utakaa nyumba moja na mchawi??
Watu wanaosali ni ngumu sana kukaa na wasiosali kabisa na wasiomuamini Mungu kama wewe!!

Kama upo kwake fuata sheria zake la sivyo utamfanya akuchukie na kukuona wewe kama kikwazo kwenye familia.
Tatizo watoto wa kike mnapenda sana battle, yani unabattle na mzazi wako eti nani yuko sahihi, so ukiambiwa wewe ndo uko sahihi utaenda kumuonesha huu uzi ama??

Ajabu sasa ukiolewa na mume mwenye mawazo kama ya mama yako na ww utaanza kusali.
Nmeshaamua kufunika kombe mwanaharamu apite, But sidhani hata Mungu anapenda kuona binadamu aliyemuumba ananung'ununika kwa kulazimishwa kumuabudu
 
Jenga hoja acha kumprove wrong, wew jamaa nakuonaga una akili kumbe bado sehemu ya akili zako imeegemea ktk dini.

Ni ngumu kutenganisha Utumwa na Dini za watu weupe, huwez kujiita umeelimika ilihali bado unaamini dini kuwa kigezo cha maisha ya mtu mweusi, acheni ujinga, someni sana, hivyo videgree vyenu mnavyosoma kwenye vyuo vyenu vya mabua kwa kutegemea boom la serikali ili mtoboe na kukalilishwa upumbavu, basi mkigraduate acheni kujiona wajuaji.

Humu kuna wasomi zaidi yenu ambao elimu wameipata nje ya uwezo wa level zenu za syllabus, so ukiona mtu anapinga jambo fulan, jitahidi kudadisi na sio kuhukumu,

Elimu ni pana, huwa nashangaa kumuona mbongo analingia Elimu hii mnayosoma huko majalalani

Dini zote ni uongo, Mungu wa dini hayupo, na hatowai kuwepo

Sio ajabu unazidiwa akili mpaka na Mkeo Kwa akili za namna hii.
Huu mjadala hauhusu Dini ya kweli au ya uongo. Huu mjadala hauhusu mambo ya uzungu au uafrika.
Mada haihusu uamini uwepo wa Mungu au kutokuwepo.

Mada inahusu mamlaka ya familia Kwa MTOTO. Moja wapo ni mzazi kuhakikisha mtoto anaenda kanisani au msikitini. Kwenda shamba au kwenye shughuli za kifamilia n.k.

Huyo kama hataki au anajiona anaakili, aanzishe familia yake afanye atakavyo.
Mama yake hajamuambia aamini katika Mungu, Ila kamuambia aende Kanisani.

Suala la kuamini ni suala la mtu binafsi. Suala la kwenda Kanisani ni tofauti na kuamini. Kanisani watu wanapenda Kwa malengo mengi. Mojawapo ni suala la Maadili, kujenga umoja wa kijumuiya baina ya watu
Sio kila anayeenda kanisani au msikitini anaamini katika Mungu.

Ndio maana nikakuambia Wewe akili yako ni ndogo kuliko hata ya Mkeo au mwanamke utakayemuoa.
 
Nmeshaamua kufunika kombe mwanaharamu apite, But sidhani hata Mungu anapenda kuona binadamu aliyemuumba ananung'ununika kwa kulazimishwa kumuabudu

Wewe ni mtoto. Upo chini ya wazazi. Mungu Hana habari na Wewe. Jukumu kawaachia wazazi wako.
Siku ukitoka hapo NYUMBANI ndio Mungu ataanza kukuzingatia
 
Back
Top Bottom