Mzazi kumpa mtoto chochote anachokitaka ni sawa na kumharibu?

Mzazi kumpa mtoto chochote anachokitaka ni sawa na kumharibu?

Mtoto wako lazima ajue kuwa si kila anachokitamani lazima akipate. Mimi watoto wangu huwa wananiomba baadhi ya vitu nawaambia kwa sasa sina pesa nikipata nitakununulia. Usimpe mtoto kila anachokihitaji ambacho sio essential kwenye maisha. Lazima watoto wajue kuna kukosa na kuishi bila ya kuwa na unachokipenda. Hizi habari za "junior mwanangu, junior mwanangu" kila anapoona kitu anataka na unampa, unaharibu watoto, you wont live with them forever. You might be gone one day, wakati bado wapo wadogo, they'll live a miserable life kwa kuwa walizowea kudekezwa. Mpe vitu vya lazima na hata mara maoja moja visivyo vya lazima kama una uwezo, lkn mtoto wako lazima ajue kuna kukosa, hata kama una uwezo, lazima ajue si9 kila unachokipenda utakipata.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Mzazi mwenye uwezo kumpa mtoto chochote anachokitaka ni sawa na kumharibu? Na kumnyima napo ndio kumjenga?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, nilipokuwa form one mnamo mwaka 2000 katika shule moja ya secondary tulipata kupewa T-shirts flani hivi rangi ya dark blue ambazo tulikuwa tunavaa siku ya Ijumaa kama sare ya shule kwa maana siku ile (Ijumaa) ilipangwa kuwa ndio siku ya michezo kwa wanafunzi. Hivyo ikifika saa 6 mchana tu baaaaas masomo yote husitishwa na wanafunzi wote huenda viwanjani kwa ajili ya michezo huku ndugu zetu waislamu wakielekea misikitini (Masjid) kwa ajili ya swala ya Ijumaa.

Sasa bwana ile t-shirt yangu nilikomaa nayo miaka mitatu. Yaaani form one yote ninayo, form two bado ninadunda nayo mpaka form three hiyo mwaka 2002 ngoma ninakomaa nayo ingawa akawa imepauka sana kwa maana wanadai zilikuwa zimetengenezwa kwa cheap cotton hivyo zilikuwa zinatoa rangi wakati wa kufua.

Ilipofika mwezi wa sita, baada ya kufungua likizo ndefu, basi toleo jipya la t-shirt likatolewa, t-shirt nzuri hiiiiizooo, dark blue flani hivi zinavutika vutika mkikaa pale assembling point basi zinang'aaaaa mpaka raha.

Karibia nusu ya rafiki zangu wengi walizinunua t-shirts zile mpaka wasichana. Nikawa ninajisikia inferior sana mbele za wenzangu.

Baada ya kuona vile, mimi niliporudi home tu nikasubiri jioni muda wa kula nikamwambia mama yangu kwa maana shida nyingi huwa ninaongea na mama na sio baba. Mama akalifikisha lile suala kwa mzee baba. Aisee mzee baba aliwaka sio mchezo. Mzee alikuwa anasema "mama Hassan (hilo Hassan ni jina la uongo) hawa watoto ukiwaendekeza kuwapa chochote wanachokitaka utawaharibu hawa, tukifa watashindwa kuishi kwa ndugu" ingawa ilipofika mwisho wa mwezi mama alipewa pesa na baba kisha akanipa mimi nikaenda nunua t-shirt mpyaaaa na mimi nionekane msafi mbele ya mademu wa form 3.

Wazazi mlipo humu Jamiiforums eti ni kweli kumpa mtoto kile anachokitaka ni kumharibu? Na kumyima napo ndio kumjenga?

Ninakaribisha maoni yenu.

BIASHARA: Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kuna kitu nimegundua katika maelezo yako, huenda mzee wako kuna kitu amegundua juu yako kuna mienendo yako baba inampa shida ndiyo maana anakua mkali kukupa kila kitu, usije mletea wajukuu kabla ya wakati,
 
Dunia ya Sasa ni Mzazi wa ajabu sana, atakayetaka mwanawe ahangike kama yeye alivyoangaika.

Mpe mtoto kila kitu anachokuomba, na hata vile asivyokuomba Mpe nahii nipamoja na kumjengea uwezo wa kujiamin n.k.

Tuwalinde watoto kwa kuhakikisha tunawapa wanachotaka ili mradi kinamjenga nasio kubomoa.

NB..Nmesoma Kichwa cha uzi na Aya yakwanza.
 
Dah mi nimekulia mazingira ambayo ni ya ushuani ila sikupata ile burudani ya kuwa mtoto kabisa. Ile sijui unataka toy unanunuliwa. Nguo mpya unanunuliwa. Sikumbuki kama ni more than 3 times nimenunuliwa nguo mpya dukani kwenye zile sikukuu. Nguo nyingi zilikuwa za kurithi kwa braza.

Ilikuwa ni manyanyaso na kukoseshwa raha 24/7 but i thank God nimekuwa na misuli ya imani sana. Niko imara katika maisha yote yawe ya raha ama shida.

Ila watoto wangu nitawaspoil sana tu as long as napata nafasi na hela ipo. Give them butters, ni malaika hao hawana hatia but as soon as 18yrs inapofika ni mwendo wa jeshi!
 
Mshua wako atakuwa alikuwa mkoloni

Ha ha ha

Hata nguo una rithi.....daaaa
 
Unauliza kitu ambacho majibu yake unayo !!??
😎 😎 😎
Jamiiforums ni sehemu ambayo watu hukutana wakiwa na mawazo tofauti tofauti ndio maana nikaamua kuomba michango ya wadau humu.

Kuna wadau wanasema sio huku wengine wakisema ndio
 
Mahitaji ya muhimu kama unauwezo mpe,maana nimeona kuna wazazi wanataka watoto wayaishi maisha waliyowaishi wao!
 
Siwezi mpa kila kitu kila anapohitaji.Kuna vingine anahitaji viko nje ya uwezo wangu so siwezi mpa.Kuna vingine anahitaji lakini vina madhara yake.Mf.mi wanangu bado wadogo kuna wakati nlitoka kila mara wananiambia niwaletee chocolate,pipi biscuits.Siwezi waletea kila siku Kwa nawaambia vinaharibu Meno,so badala yake ntawaletea Ubuyu, popcorn etc.

Kuna huyu wa 8yrs aliniambia nimnunulie iPad (Sijui alijulia wap)nikamwambia sina pesa hiyo Kwa sasa na hata kama ningekua nayo nisingempa Kwasababu sijaona umuhimu wa kukipata kitu hicho Kwa umri wake.

Kwa mtazamo wangu mtoto apewe kila ambacho kina umuhimu kwake Kwa wakati husika,na si kila anachohitaji bila kujali umuhimu wa anachoomba. unavoacha kumpa mpe sababu ili aridhike.
 
Siwezi mpa kila kitu kila anapohitaji.Kuna vingine anahitaji viko nje ya uwezo wangu so siwezi mpa.Kuna vingine anahitaji lakini vina madhara yake.Mf.mi wanangu bado wadogo kuna wakati nlitoka kila mara wananiambia niwaletee chocolate,pipi biscuits.Siwezi waletea kila siku Kwa nawaambia vinaharibu Meno,so badala yake ntawaletea Ubuyu, popcorn etc.
It's okay@
 
Back
Top Bottom