Mzazi kumpa mtoto chochote anachokitaka ni sawa na kumharibu?

Mtoto wako lazima ajue kuwa si kila anachokitamani lazima akipate. Mimi watoto wangu huwa wananiomba baadhi ya vitu nawaambia kwa sasa sina pesa nikipata nitakununulia. Usimpe mtoto kila anachokihitaji ambacho sio essential kwenye maisha. Lazima watoto wajue kuna kukosa na kuishi bila ya kuwa na unachokipenda. Hizi habari za "junior mwanangu, junior mwanangu" kila anapoona kitu anataka na unampa, unaharibu watoto, you wont live with them forever. You might be gone one day, wakati bado wapo wadogo, they'll live a miserable life kwa kuwa walizowea kudekezwa. Mpe vitu vya lazima na hata mara maoja moja visivyo vya lazima kama una uwezo, lkn mtoto wako lazima ajue kuna kukosa, hata kama una uwezo, lazima ajue si9 kila unachokipenda utakipata.
 
Kuna kitu nimegundua katika maelezo yako, huenda mzee wako kuna kitu amegundua juu yako kuna mienendo yako baba inampa shida ndiyo maana anakua mkali kukupa kila kitu, usije mletea wajukuu kabla ya wakati,
 
Dunia ya Sasa ni Mzazi wa ajabu sana, atakayetaka mwanawe ahangike kama yeye alivyoangaika.

Mpe mtoto kila kitu anachokuomba, na hata vile asivyokuomba Mpe nahii nipamoja na kumjengea uwezo wa kujiamin n.k.

Tuwalinde watoto kwa kuhakikisha tunawapa wanachotaka ili mradi kinamjenga nasio kubomoa.

NB..Nmesoma Kichwa cha uzi na Aya yakwanza.
 
Dah mi nimekulia mazingira ambayo ni ya ushuani ila sikupata ile burudani ya kuwa mtoto kabisa. Ile sijui unataka toy unanunuliwa. Nguo mpya unanunuliwa. Sikumbuki kama ni more than 3 times nimenunuliwa nguo mpya dukani kwenye zile sikukuu. Nguo nyingi zilikuwa za kurithi kwa braza.

Ilikuwa ni manyanyaso na kukoseshwa raha 24/7 but i thank God nimekuwa na misuli ya imani sana. Niko imara katika maisha yote yawe ya raha ama shida.

Ila watoto wangu nitawaspoil sana tu as long as napata nafasi na hela ipo. Give them butters, ni malaika hao hawana hatia but as soon as 18yrs inapofika ni mwendo wa jeshi!
 

Mshua wako atakuwa alikuwa mkoloni

Ha ha ha

Hata nguo una rithi.....daaaa
 
Unauliza kitu ambacho majibu yake unayo !!??
😎 😎 😎
Jamiiforums ni sehemu ambayo watu hukutana wakiwa na mawazo tofauti tofauti ndio maana nikaamua kuomba michango ya wadau humu.

Kuna wadau wanasema sio huku wengine wakisema ndio
 
Mahitaji ya muhimu kama unauwezo mpe,maana nimeona kuna wazazi wanataka watoto wayaishi maisha waliyowaishi wao!
 
Siwezi mpa kila kitu kila anapohitaji.Kuna vingine anahitaji viko nje ya uwezo wangu so siwezi mpa.Kuna vingine anahitaji lakini vina madhara yake.Mf.mi wanangu bado wadogo kuna wakati nlitoka kila mara wananiambia niwaletee chocolate,pipi biscuits.Siwezi waletea kila siku Kwa nawaambia vinaharibu Meno,so badala yake ntawaletea Ubuyu, popcorn etc.

Kuna huyu wa 8yrs aliniambia nimnunulie iPad (Sijui alijulia wap)nikamwambia sina pesa hiyo Kwa sasa na hata kama ningekua nayo nisingempa Kwasababu sijaona umuhimu wa kukipata kitu hicho Kwa umri wake.

Kwa mtazamo wangu mtoto apewe kila ambacho kina umuhimu kwake Kwa wakati husika,na si kila anachohitaji bila kujali umuhimu wa anachoomba. unavoacha kumpa mpe sababu ili aridhike.
 
It's okay@
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…