Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Evil motives
 
Nimeshamwambia mara nyingi sana aje amchukue aishi naye ila hatak,kwahiyo akienda kusema hivyo mahakanan sitakua na pingamizi,

Achana naye huyo mpuuzi.
Lea mtoto wako mwenyewe, Mungu atakubariki.

Achana naye, nasisitiza achana naye.
Wala usiumie. Usimhangaishe.

Mimi nimelelewa na Upande wa Mama. Najivunia hivi nilivyo, na namshukuru Mungu Kwa mpango wake alioufanya nikalelewe hivi.

Nasisitiza, usimsumbue, muache Kama hataki kumlea Mwanaye. Mlee Kwa uwezo wako tuu, mtoto atafanya vizuri tuu.

Mpeleke shule za kawaida Ila hakikisha unamfuatilia Kwa umakini na kuikuza akili na Uelewa wake kuhusu Dunia.

Mimi Taikon nimeishi hivyo na nimelelewa hivyo. Mpaka nimemaliza Chuo kikuu na sasa najitegemea Kwa kila kitu.

Usigombane na mtu kisa mtoto wako uliyemzaa Kama hataki au anazembea kumtunza. Hiyo ni baraka. Alafu Mungu anataka akufundishe Jambo.

Unachopaswa kufanya, ni kuangalia Kwa umakini Mungu anataka kufanya nini kwenye maisha ya mtoto wako huyo.

Nimeandika mpaka yasiyohusu. Ila ni Kwa sababu naelewa Hali unayopitia na anayopitia mtoto. Lakini hiyo isikufanye kushindwa au kugombana na huyo Baba yake.

Mkaushie.
Matunda yake atayaona after 20yrs to come.
 
hatuna uhakika km anakwepa au la maana kama walikubaliana toto wa akasome hio shule why akatae kulipa? haimake sense, huyu dada inanekana aliamua kukomaa wnyw sema mambo hayajakaa vzuri now so antk jamaa alipe whch is not bad lkn km hawakukubaliana tangu mwanzo hio ni changamto maana huwez from nowhere ukamtaka mtu aanze kulipa 2mil kwa ratiba ambayo hakuianzsha pengine angeshirikishwa angekuwa na mawazo mengine, mawasiliano muhimu kwa wenza wenye watoto
 
Duuh Hadi mtotot anataka kubadilishwa majina?
 
Wanawake mnaopleleka wanaume zenu mahakamani kisa hawahudumii watoto akili zenu zipo migongoni.

Mtoto ni wako umem beba miezi 9 si upambane nae mwenyewe,mwanaume hataki kulea si unabadlisha hata jina la mtoto kama alikua akiitwa SAIDI JUMA unamuita SAIDI SHEILA

Yani cancel hiyo taka taka isiyojua majukumu yake,vaa umama wa asili mtoto mdogo elimu ya primary anakushinda akifika chuo utamuweza wewe?

kwanini wanawake ni legelege hivyo hata kwa mambo yenu ambayo mnatakiwa kuyavaa kisawa sawa? mwanaume halazimishwi kulea dada

huko mahakamani akiambiwa akupe 70k kila mwezi utafanyia nini hizo 70k hivi hujakutana na wanaume wehu eeh? kagoma kuhudumia hivi unafkiri ataruhusu mtoto asomeshwe shule za kulipia wakat MAMA kasema elimu ni bure?

Wanawake mfike mahali muache kulia lia na mjue kuwa kuna majukumu mengine ni yenu tu,Ashukuriwe Mungu am not a woman, mwanaume akatae hudumia mtoto wake haki angemsikia mwanae kwenye radio ya BBC tu maisha yake yote.

kwann wanawake wa siku hizi hampo tayari kuteseka kwa ajili ya watoto wenu? Kupewa mimba ndio ishakua kisingizio siku hzi,hebu jifunzeni MAMA ni zaidi ya kuingia Leba nyie kina mama.
 
ht km mmeachana ila mtoto ni wa wote waiwili so maamuz yoyte kuhusu mtoto lazima mkubaliane kwanza hio inapunguza migogoro,
 
Dada Anita, Sheria haijali hakimu amaishije bali Sheria inasemaje. Suala la kusema Elimu bora ipo private school ni dharau kwa serikali.

Je hujui kuwa mahakimu wanakula rushwa? Lakini cha ajabu akipelekwa mtuhumiwa mla rushwa mahakamani haohao mahakimu humuuliza kwa nini amechukua rushwa.

NB: Sio mahakimu wote ni wala rushwa.
 
Hadi umenitoa machozi! Asante kwa ushauri
 
Sahihi kabisa
 
Huyo uliyeenda kuishi naye au aliyekuachanisha na hiyo ndoa yako kwa nini asihudumia kulipa ada ya huyo mtoto
 
hata Mimi hivyo hivyo. huyu wa kwangu ikifika hatua ananiambia eti mtoto chakula Hana, kiwi Hana, mswaki umechakaa, nilimuoma shetani kweli kweli
 

Yani hovyo sana hawa viumbe
 
Yani hovyo sana hawa viumbe
acha hizo banaaa sio wa hovyoo, changamoto inakuja pale mwanaume anapotumia nguvu na akili nyingi kusuluhisha ama kutatua tatizo la upande wa pili.

endapo umedhamiria na kuridhia kuishi na mwanamke, watakiwa uheshimu hisia zake, baadhi ya mambo yabidi uyafumbie macho na uwe ka mjinga fulanii iviii.

Fumbo mfumbe mjinga na mwerevu ataling'amuaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…