Nimeshamwambia mara nyingi sana aje amchukue aishi naye ila hatak,kwahiyo akienda kusema hivyo mahakanan sitakua na pingamizi,
Achana naye huyo mpuuzi.
Lea mtoto wako mwenyewe, Mungu atakubariki.
Achana naye, nasisitiza achana naye.
Wala usiumie. Usimhangaishe.
Mimi nimelelewa na Upande wa Mama. Najivunia hivi nilivyo, na namshukuru Mungu Kwa mpango wake alioufanya nikalelewe hivi.
Nasisitiza, usimsumbue, muache Kama hataki kumlea Mwanaye. Mlee Kwa uwezo wako tuu, mtoto atafanya vizuri tuu.
Mpeleke shule za kawaida Ila hakikisha unamfuatilia Kwa umakini na kuikuza akili na Uelewa wake kuhusu Dunia.
Mimi Taikon nimeishi hivyo na nimelelewa hivyo. Mpaka nimemaliza Chuo kikuu na sasa najitegemea Kwa kila kitu.
Usigombane na mtu kisa mtoto wako uliyemzaa Kama hataki au anazembea kumtunza. Hiyo ni baraka. Alafu Mungu anataka akufundishe Jambo.
Unachopaswa kufanya, ni kuangalia Kwa umakini Mungu anataka kufanya nini kwenye maisha ya mtoto wako huyo.
Nimeandika mpaka yasiyohusu. Ila ni Kwa sababu naelewa Hali unayopitia na anayopitia mtoto. Lakini hiyo isikufanye kushindwa au kugombana na huyo Baba yake.
Mkaushie.
Matunda yake atayaona after 20yrs to come.