Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Aliyechagua shule ndio alipe Ada.
Mbona unashindwa kuelewa mambo madogo.

Yaani kuna wanawake ukizaa nao inakuwa Kama umezaa na mwendawazimu.

Shule uchague wewe alafu mwanaume uliyezaa Naye alipe Ada. 😂😂
Mnhhhh wewe utoto unakusumbua, mtoto wako asiende shule nzuri kisa mama yake kachagua shule..?!
 

Shosti nenda mahakamani, ukipoteza utajua nini next...
 
Kuna maswali ya kukuuliza hapa,
*Je, mlijadiliana na baba yake wapi huyo mtoto akasome, iwe private school au serikalini?
*Kama mlijadiliana, alikubali na mkakubaliana atakuwa na uwezo wa kulipia kiasi gani kwa mwaka?
*Kama alisema hana uwezo wa kumpeleka mtoto shule ya private, je ulifanya maamuzi ya kumpeleka huko mwenyewe?

Nauliza hivi kwa sababu haya mambo sio ya kujifanyia bila makubaliano. Kama jamaa hana uwezo wa kumpeleka mtoto shule ya 2m, wewe ukang'ang'ania huko kwa show off za wanawake walio wengi, kosa ni lako. Kama mlikubaliana basi ana makosa na anawajibika kumsomesha shule mliyokubaliana.

Humu watu wana makasiriko sana, hizi issues hatuombi zimkute mtu ila that's part of life, kuachana kupo japo hatuombei hivyo, shida ni jinsi mtakavyoishi na kumlea mtoto huku mkiwa separate.

Kingine, hizi ni issues za ustawi wa jamii, huko mahakamani nilidhani mnaenda kutengua(talaka) ndoa tu na kuweka misingi ya malezi ya mtoto.
 

Ndio maana nawe nikakuambia kuwa wewe akili yako ni chenga.

Kama unajua kabisa watoto wote wanapaswa kupewa haki Sawa. Nini kinakufanya usimpeleke Mtoto Kwa Baba yake ili apewe Huduma na ndugu zake Kwa pamoja?

Kama unataka haki tenda Haki.
Ukiwa Mbali utapata Haki za Mbali
Ukiwa karibu utapata Haki za ukaribu.

Mtoto akiwa mbali ni Kama Mwanampotevu aliypotezea na Mama yake.

Ushaambiwa fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

Pia kiuchumi sio rahisi kuhudumia mtu ambaye yupo nje ya Mfumo. Na nigharama. Sijui wapi huelewi.
Mtoto anayelelewa na Mama yake yupo nje ya Mfumo wa Baba yake.
Ndio maana haya baadaye akikua ata-base na Kwa mama tuu

Mtoto unataka apate Haki zote Kwa Baba yake, mpeleke Kwa Baba yake.
Hutaki basi Acha kulalamika kuwa Baba hamjali mtoto ilhali wewe ndio humjali mtoto kwani hutaki kumpeleka Kwa Baba yake.

Unataka atumiwe Ada ili ujisifu Kwa watu huko unasomesha wewe kumbe anayesomesha ni Baba yake
Ukitaka sifa inabidi uzigharamikie.
 
Relax mama,leta akaunti namba ya shule nikusaidie kulipa ada,wewe mwenyewe utanifikiria baada ya kuona bank slip.
Achana na mambo ya mahakamani utajichoresha tu.))
Kuna ulazima gani wa kumsomesha English Medium wakati shule za serikali zimejaa na wanasema elimu ni bure?
 

Eti mtoto unataka apate haki za baba yake,mpeleke kwa baba yake...

Yaani nimeangalia tena posts zako kwenye topic hii...duh!
 

Hatma ya mtoto ni apelekwe Kwa Baba yake mbona jibu lipo wazi Mkuu.

Hata akifika Leo ustawi au mahakamani ataambiwa Kwa nini asimkabidhi mtoto Kwa Baba yake ikiwa yeye hawezi kumtunza Mtoto.
Atatoa hoja zake Kama zinamashiko basi ndio Baba ataambiwa yeye uwezo wake Ukoje.
 
Baba alivyomwacha mtoto kwa mama yake hakujua kuna ulawiti sijui mambo gani..unandika mambo ya kufikirika ......Kwa kheri.
Umepewa hoja za msingi sana, mkubwa akivuliwa nguo anachutama kuficha uchi.
 
Eti mtoto unataka apate haki za baba yake,mpeleke kwa baba yake...

Yaani nimeangalia tena posts zako kwenye topic hii...duh!

Sasa unataka sifa alafu huwezi kuzigharamikia, huo ni uchizi.

Ni Sawa na Baba ambaye hajamtunza na kumlea mtoto alafu mtoto akifanikiwa ndio amshobokee mtoto. Ndio kesi Kama hii.

Mama na Baba wanahaki Sawa katika matunzo ya mtoto. Ikitokea kutengana taritbu zinafuatwa kulingana na uwezo wa wawili HAO.
Huna uwezo iwe WA Akili, uchumi, maadili hovyo basi unakosa vigezo vya kuishi na mtoto.
 
Yaanii bidada anataka kukomoa ndio Nia yake mkuu kwangu ndio ninachokiona Kwa sababu kama nyumba kaachiwa kwahiyo anataka kumfirisi mwanaume kupitia mtoto
 
Acha ngonjera, hayo ma-slay and drama queens lazima wajifunze in a hard way.
Sasa hapo ndugu una mfunza in hard way ni mama au mtoto wako mwenyewe.....??

Kwani madai ya mama ni kumhudumia yeye au mtoto wako.....??

Sasa kuacha kutoa huduma za mtoto wako kunamkomoaje mama mtoto wako....na kwanini ufikirie kumkomoa mtu ambaye anamtunza mtoto wako.....??

Kwanini unakwepa uwajibikaji kwa jambo ambalo umelisababisha mwenyewe.....??

Kwanini umpe adhabu kiumbe ambaye hakukuomba umlete duniani kwa kosa ambalo pengine hata halifahamu au ahusiki nalo......??
 
Mpelekee mtoto wake ss kama unaye mwenyewe unataka ahudumie tena wakati anao watoto wengine. We chukua mpelekee mwqnae akae naye
 
Mtoto apelekwe shule za serikali ni bure
 
Si kweli asilimia kubwa ya me wana tabia moja ya hovyo Sana akigombana na ke basi hata watoto anawachukia hatoi huduma yupo radhi alee watoto wa hawara ambao si wake na kuacha watoto wake wakihangaika, na ndio hao hao wa Kwanza kulalamika wametendwa na watoto wa kambo pia wametengwa na watoto rejea malalamiko ya baba Naseeb wako wengi wenye tabia kama hiyo

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Ulimfanya nini huyo kidume mpaka akakuachia mpaka nyumba? Halafu nitaendelea
 
Kabla ya hapo kifamilia mmeyajadili kuhusisha ndugu zake (kaka, dada, shangazi, mama, baba, n.k). Na je mtoto ni chatta lake au anaokoteza kucha na kutembea?!
 
Kuna mwingine nae alishauriwa vibaya na wenzake, jamaa anampa 100k kwa mwezi, kampangia chumba ili mtoto apate pa kulala. Yule mwanamke akaona haitoshi bora aende ustawi wa jamii ili matunzo yaongezwe as aliona jamaa anapesa so ana wajibu wa kumhudumia yeye na mtoto, poor that girl.

Kafika ustawi akaulizwa unapewa kiasi gani, kasema 100k, malazi ya mtoto analipa baba yake. Akaulizwa unajishughukisha na nini kajibu hana kazi kwa sasa, kaambiwa TAFUTA KAZI. Jamaa kwa hasira akasema nina uwezo wa kutoa 50k kila mwezi na sina uwezo tena wa kulipia chumba. Ikapita hivyo, bidada akaambiwa arudishe mtoto kwa bibi ili hiyo 50k iwe inatumwa huko kila mwezi.

Watu mnadhani huko ustawi ni roller coaster sio.?
 
Mwambie ukweli...yeye alisikia raha tuu wadhungu wanaseleleka ndiani ya mbususu
Hapana Ndugu.....si vyema kumhukumu mtu au kuhukumu kwa habari hii fupi ya huyu bibie....hatujui ni jambo gani lilipelekea kuvunjika kwa ndoa hiyo.......

Tusimame kwenye hoja ya msingi ambayo ni baba anakwepa uwajibikaji kwa mtoto wake......sifahamu uwezo au kipato Cha huyo mwanaume lakini kwa hali yoyote aliyonayo anapaswa kuwajibika kama baba........

Kwanini mkiachana mnakuwa maadui.... kwanini mnajenga uadui ambao muda mwingine unamuangamiza mtoto.....???

Hata kama huna kipato KIZURI kwanini msikae mkaelewana na mzazi namna nzuri ya kumlea kijana wenu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…