Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani


Huyu baba ana uwezo kiuchumi,kiakili sina uhakika kimaadili, huyu mwanamke sio mjinga kutojua aliyekuwa mume wake ana uwezo wa kumhudumia mwanae.

Kuwashobokea watoto unazunguka sana, huyo baba kama ana uwezo amhudumie mwanae,period. Na kisha labda mambo ni mengi tu huyu mtoto ananyimwa mpaka kum frustrate huyu mama,..
 
Nadhani ungetulia vizuri na kuelewa usingetetea, mtoa mada anazungumgumza suala la kumpeleka mtoto ingilishi midiam, na hajasema baba mtoto hatoi matunzo, na kama umesoma vizuri Mzazi mwenzie amemjibu uza nyumba which means na nyumba kaachiwa Ili mtoto awe Salama, Kwa mstabali huo matunzo anatoa ila Hilo la kulazimishwa kumlipia ada mtoto inglish midiamu ndo amelikataa, hebu soma tena uanze upya kutetea hoja yako
 
Mtoto apelekwe shule za serikali ni bure
Hayo ni mambo ambayo wewe na mzazi mwenzio mnaweza kukaa na kujadiliana na kufikia maamuzi hayo kutokana na kipato au Hali ya uchumi kwa wakati uliopo na sio kufanya maamuzi hayo kwa kiburi na jeuri.....

Kama uchumi wako unaruhusu kwanini usimpe huduma Bora mwanao ikiwemo na kumsomesha shule nzuri.....??
 
Aende atajua mbele kwa mbele...tena mmeng'ang'ania ada ukute mambo mengi tu huyu mtoto ananyimwa,msimuangalie mtoto..kisa tu analelewa na mama yake...
Sisi hatujang'ang'ania ada ni mto mada ndiye aliyezungumzia mambo ya ada na ndo maana hoja nyingi zimeegemea hapo angeeleza Kila kitu nadhani ungeona utofauti, naona wanawake pengine mnafikiri wanaume hawapend watoto au hawataki kutunza hapanaa, hoja imeletwa Kwa habari ya ada kumlazimisha baba mtoto alipie ada shule za gharama hiyo sio sawa kabisa
 
Kubwagwa na mwanamke ni jambo lingine na kumhudumia mtoto wako ni jambo lingine ambalo halihusiani na jambo la kwanza......

Achana na mwanamke aliyekubwaga timiza wajibu wako kwa mtoto wako....
Mbona jamaa anatimiza wajibu wake mpaka anasema kama vipi auze nyumba. Hiyo ni tosha kutuambia kuwa jamaa anaufikirio sana ila huyu mwanamke ndio anaweza kuwa tatizo
 
tatizo wanawake wa kisasa hamjui hata kusema I am sorry....kiini cha hilo ni sababu iliyofanya ndoa ikafa. mmejaa viburi kupitiliza mkidhani mume na mke ni sawa. madhara yake ndiyo hayo, jamaa anajua unasota na mtoto ipo siku mtoto atamtafuta baba yake
 
Mbona jamaa anatimiza wajibu wake mpaka anasema kama vipi auze nyumba. Hiyo ni tosha kutuambia kuwa jamaa anaufikirio sana ila huyu mwanamke ndio anaweza kuwa tatizo
Hapana Ndugu...Mimi kwa mtazamo jawabu hilo halitoshi kuwa jibu la baba muwajibikaji kwa mtoto wake..... Hilo ni jibu fupi kwa mtu asiyependa kufanya kile alichoambiwa afanye.....ukipima uzito jambo lililo mbele yake na jibu alilotoa.......

Sasa mama atauzaje anayoishi yeye na mwanae kwa ajili ya kulipa tu ada....??

Na kama unapitia wakati mgumu kifedha si mambo ya kuzungumza na mwenzio kuamua hatima nyingine ya masomo na mustakabali wa mtoto wenu kwa pamoja.....??
 
Kama hauna facts, hata hizi ni assumptions tu
Sasa ndugu hapo fact ni zipi katika hili.....tunachojadili hapa ni suala mtoto kukosa huduma za baba yake mzazi......kama ilivyo wasilishwa na mama wa mtoto.......
 
Wale wanaume waliokua wanakudanganya kuwa wanaweza kukufikisha,ukaanza kumdharau mumeo kwa Sasa hawakufikishii matumizi ?? Au nao wamekukimbia ??
Wanawake badilikeni tamaa zenu zinawaponza Watoto.!! Nje ya Ndoa wanaume wadangaji hawakutumii Hata msg yenye kiemoji Cha love mana hawataki kujishughulisha kulea Watoto Wa watu. Wanaume wanahangaika Kwa ajili ya familia bila kujali shukrani ,wanastahili Heshima.

Wanawake wanawaza starehe zao za kimwili na kusahau jesho ya familia na ndio chanzo Cha ndoa nyingi kuvunjika.

Mpeleke Mtoto Shule za serikali baba Watoto ameshakatwa tozo Kule Ili Mtoto asome.
 
Na kwa nini asibaki kwa mama yake....kisa tu mama ametaka mtoto aende international school?!..khaa

Unaona ulivyochenga sasa.
Ndio maana nikakumbia wengi wenu akili ni chenga, mnawatia aibu wanawake wenye akili ambao ni wachache.

Sasa Kama umechagua wewe international school si ulipe ADA. Kuna aliyekuzuia.

Ukishakuwa nje ya Mfumo wa mwanaume huna haki Kama Mke, mke aliyepo kwenye ndoa ndio anaweza kumshawishi mume wake tena Kwa majadiliano ya adabu kuwa Mtoto asome wapi.

Sasa ukishakuwa mpita njia huna hiyo Haki. Anayeangaliwa ni mtoto sio Kauli ya Mama yake(wewe).

Anayejua uchumi wa Mwanaume ni Yule mke WA ndoa anayeishi ndani ya mwanaume sio wewe WA nje huko.

Sijui wapi hamuelewi
 
Bab si anatakiwa awajibike kwenye malezi.
 
Sasa ndugu hapo fact ni zipi katika hili.....tunachojadili hapa ni suala mtoto kukosa huduma za baba yake mzazi......kama ilivyo wasilishwa na mama wa mtoto.......
Mkuu, kuna gap kubwa sana ya uelewa kati yetu. Hiyo story ni one sided, with little or no facts, hatuwezi kuongea mambo mengi kama vile watu wa ustawi wa jamii. Atueleze kwanini kaachwa na kutekelezwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…