Unauliza kama kutoamini kuwa kuna nguvu ya Mungu ni sawa? Au ni kuamini kitu kilicho kweli?
Tushaona imani unaweza kuamini hata uongo, kitu cha muhimu ni ukweli. Kwa nini unajikita kwenye imani bado?
Hayo ni maswali mawili tofauti.
Swali la kwanza, kuamini, au kutoamini kwamba kuna nguvu ya Mungu (hizi ni pande mbili za shilingi moja ile ile) sio tu ni sawa, hii ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania. Pia, hii ni haki ya binadamu iliyopitishwa katika Universal Declaration of Human Rights. Azimio hili limepitishwa na Umoja wa Mataifa December 10 1948.
KIla mtu ana haki ya kibinadamu ya kuamini au kutoamini nguvu za Mungu wake anavyotaka. Na katika kuongelea imani, maadam tunaongelea imani tu, hakuna imani iliyoishinda nyingine, maadam haiingilii uhuru wa wengine.
Kwa hivyo, ukitaka kuamini nguvu za Mungu wako ambaye ni mti wa mbuyu, una haki hiyo, na hilo ni sawa. Ukitaka kuamini Mungu wako ni Yesu Kristo Masiha, una haki hiyo, na hilo ni sawa. Ukitaka kuamini Mungu wako Allah, ni haki yako, na hilo ni sawa, ukitaka kuamini miungu yako isiyo na idadi, una haki hiyo, na hilo ni sawa, ukitaka kutoamini Mungu yeyote, kama mimi, ukasema hizi habari za Mungu zote ni ujinga mtupu, hiyo nayo ni haki yako ya kibinadamu, ni sawa tu.
Na mimi, licha ya kutoamini Mungu yeyote, tukiwa katika habari za imani, natetea haki za watu wote kuamini wanavyotaka, au kutoamini, ilimradi kuwe na mipaka mizuri ya kutoingiliana.
Hilo ni swali la kwanza, kutoamini katika nguvu ya Mungu katika maisha ya binadamu ni sawa?
Kwa kuwa tumekubaliana awali kwamba ukweli ni muhimu kuliko imani, kwa sababu ukweli upo mmoja tu, na imani unaweza kuamini hata uongo, tunapata swali la pili tofauti. Swali la kuangalia ukweli.
Je, ukiamini katika nguvu za Mungu unaamini katika ukweli? Huyo Mungu yupi kweli?.
Jibu ni, kwa kuanzia Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote anayesemwa kuwa ni muumba wa vyote, Mungu huyu hayupo, anaweza kuoneshwa kimantiki kwamba huyu ni muhusika wa hadithi ya kutungwa na watu tu, na hivyo, kuamini katika nguvu zake ni sawa na kuangakia sinema ya James Bond 007 na kujirusha kutoka ghorofani ukiamini kwamba utaruka kwa nguvu za Ki James Bond kutika katika filamu ya Casino Royale.