Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Inawezekana kabisa msomi akaanzisha biashara ya chipsi kisomi,
Upo sahihi kabisa na wala haujakosea katika maelezo mtaji wake wa kufanya yote anautoa wapi Sawa Jimmy muuza Viepe,
 
Kama hana akili za kujiongeza Kwa nini usimpe kazi Yako?

Kama unamsikilizaga Kishimba ndio utaelewa Huwa anaongea nini.Lazima kurithisha Watoto kazi unayofanya ila Sasa kama wewe ni mtumishi hapo ndipo kimbembe huja.

Ni kujitahidi kuwa na kazi biashara au mradi Nje ya Ajira Ili arithi.
 
Nadhani hujakulia kijijini , kule familia nzima mnaenda Shamba, wakati wa likizo inasaidia kuzalisha chakula mnachokula na urithi ni hayo mashamba
 
Upo sahihi kabisa na wala haujakosea katika maelezo mtaji wake wa kufanya yote anautoa wapi
Sehemu ya usomi ni kujua pa kupata mitaji. Siku hizi kuna mpaka Venture Capitalist na Angel Capitalists maalum wamejikita kufanya biashara na watu wa Global South, hii mitaji ya $10,000 - 20,000 ni rahisi sana kupata kama una idea nzuri na unaweza kui present.

Tatizo, hao tunaowaita wasomi wetu wanajua hata kuandika hizo presentation?

Wanayo hata hiyo idea nzuri ya ku present?

Wameshapitia hata websites kama www.kiva.org kuangalia peer microfinance systems zina options gani?

Unaona Mkenya anapiga soft loan ya US dola $50,000 online kwa kucheza na mtandao tu?

Sasa huyu Mkenya tu, si Mmarekani wala Muingereza. Kwetu wako wapi watu kama hawa?


Au wasomi wanalalamika JF na kuperuzi insta tu?

Wasomi wanajua kuishi kwa intentionality? Hata walichokisomea wanajua kwa nini wamekisomea? Au wamesoma ili wapate degree/vyeti na kuitwa wasomi tu na kutegemea kazi za kuajiriwa ofisini?

Ila naelewa sana Bongo Nyoso serikali nyoko, unaweza kumpata mtu anataka kukutumia mkopo wa $50,000 mifumo yetu yenyewe ikakubana.
 
Sasa wewe unadhani wanatakiwa wamfundishe nini? Kazi Ile Ile ya kwao harafu yeye akimaliza shule yake aje kuongeza input kwenye mradi huo.

Mfano Mimi binafsi Nina passion ya Ufugaji,ningependa Watoto waje wajifunze mambo ya mifugo au wakienda Nje ya fani wajifunze Business administration and marketing but Wakiwa wanakua watakuwa wanaona na kushiriki nachofanya ,then nikija kuchoka wa take over waendelee.

Tofauti na hapo wajifunze gani za Afya ndio Bado Zina soko japo la kugombania,content creator hii wanaweza fanya Kwa ku make reference tuu ya mradi wa nyumbani,mambo ya counseling nk.
 
Tuliosoma na tunapitia haya tunaelewa maumivu yake. Binafsi napitia haya. Baba yangu ni rafiki mfariji pekee anayeelewa maumivu yake na anasikitika sana.
Upo Kama Mimi aisee, babangu ndo pekee anaeelewa hii situation.....Mungu ampe kheri zaidi na zaidi.
 
Wote wataenda Ferry? Wenye fursa hizo ni wachache ila majority ni fukara tuu.

But kujiajiri kama una pa kuanzia au location Ina afadhari ila kujiajiri Kwa kujikimu Bora Ajira.
 
We jamaa unastahili kupewa PhD ya heshima.
 
Mzazi anakuwa anakuwa hajui mkuu
 
Kazi nyingi ndogo ndogo Zina pesa kuliko hizo kubwa Kwa sababu hizi hazina Cha TRA Wala leseni ni Nguvu zako tuu.

Ukipambana Kwa malengo huchukii mda unahamia kwenye biashara kubwa zaidi.

Kazi za maofisini ni kujikimu vinginevyo uwe kwenye cheo
 
Wote wataenda Ferry? Wenye fursa hizo ni wachache ila majority ni fukara tuu.

But kujiajiri kama una pa kuanzia au location Ina afadhari ila kujiajiri Kwa kujikimu Bora Ajira.
Nimetoa mfano wa Ferry tu , sasa nakupa mwengine>
Kuna jamaa mimi natengeneza gari kwake pale Magomeni mapipa, wameandika "tunaziba pancha 24 hours"
Ni kibanda tu cha kuziba pancha na kubadili tairi, Hakina leseni wala ushuru wa manispaaa, wao wanalipa kodi kwa mwenye nyumba Elfu 50 kwa mwezi, Gari moja kubadili tairi ni 3,000, kuziba pancha 5,000/- gari kubwa na 3,000 gari ndogo: Kujaza upepo tairi moja ni 1000:

Wanaziba karibu daladal zote za Morogoro road to Kariakoo na zile za manibo mwananyamala.
Wafanyakazi wanaingia kwa shift, magari ya mchanga, mafuso ya mkoa na daladala wacha sisi wa gari zetu z TEMESa, anaingiza more than laki 2 kwa siku na halipi kodi, huyo mtu utamwambia akaajiriwe?
 
Hahaa. Kwa nini mkuu, mbona vitu vya kawaida tu?
Kiranga! Hivi hili la wengi wa viongozi wetu kutokea familia masikini kisha tukawapa madaraka makubwa mfano Uwaziri, Ukatibu wa Wizara na hata Urais, je wewe binafsi waona ni zuri jambo hili? Pia, umewahi kufikiri kujihusisha na siasa za hapa nyumbani TZ?
 
Umasikini nini?

Inawezekana mtu akawa na umasikini wa mali halafu akawa na utajiri wa mawazo wa kuweza kuongoza?

Nina tatizo kubwa sana na wazo la kumpa au kumzuia mtu uongozi kwa kuangalia yeye masikini au tajiri.

Kwanza kabisa, kidemokrasia, kumnyima mtu uongozi kwa sababu yeye ni masikini ni kuwanyima watu wengi nafasi za uongozi. Kwa hiyo hii si demokrasia.

Pia, uwezo wa uongozi si lazima uendane na uwezo wa kiuchumi. Hivyo, ukisema masikini asiongoze, unaweza kujinyima talent ya watu wengi wanaoweza kuongoza.

Lakini zaidi, hata ukisema uwape matajiri tu uongozi, huna guarantee kwamba mtu kuweza kujitajirisha yeye ndiyo kigezo cha kuweza kuitajirisha jamii, kwa sababu mtu anaweza kuwa mbinafsi anayeweza kujitajirisha yeye vizuri, lakini asiijali jamii. Na hapo utajiri wake unakuwa disqualification actually.

Kwa hivyo, ningependa watu kupewa uongozi on the merit, kwa kuangalia uwezo wao wa kuongoza, bila kujali wao ni matajiri au masikini.

Kwa msingi huu, mtu tajiri, ambaye ni mwizi, kapata utajiri wake kwa wizi, anakuwa disqualified kuongoza, na mtu ambaye amekuwa masikini, licha ya kuwa alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuiba akajizuia, anaonekana atafaa sana kuongoza, kwa sababu ana sifa ya uadilifu.

Tunatakiwa kuupiga vita umasikini kiasi kwamba tuwe na nafasi nyingi za kuukwepa umasikini bila kupitia uongozi. Tupate viongozi ambao wanataka kuongoza ili kutatua matatizo ya jamii, si kujitajirisha.
 
Hii dhana ilinichanganya sana. Kwa muktadha huo wa 'tafsiri ya masikini', basi nimepata suluhu. Shukrani mkuu[emoji120]
 
Kuuza chips napo ni biashara kama zingine

Ova
 
Tatizo lenu mnasoma mkiwa hamjui mnataka nini, mimi wakati nasoma, malengo yangu ilikuwa ni kupata hela, sikusoma ili elimu inipeleke popote zaidi ya kutaka inipe muongozo wa kupata hela. Na ndio maana afterwards, nilifanya kazi kila sehemu so long as nilikuwa naona hapa patanipa hela. Sisi tumefungia vyeti vingi ndani, tukiwa ulaya ili tupige maokoto kwa sababu ndo tulichokuwa tunataka. Kazi za taaluma zetu zilikuwepo ila wages zipo chini, wanyama tukaingia street, the rest is history na badae tukarudi darasani kusoma ili tusionekane wajinga kwenye jamii na tu inspire our generations badae. Well, nachotaka kusema ni kwamba, kids of nowdays wajue ni nini wanataka kukipata out of hizo elimu zao wanazosoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…