Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

Endelea kuota una degree unachoma mishikaki utakua billionaire, una degree unachoma mahindi road utakua billionaire, ntakupiga kidole mda sio mrefu endelea hivyo hivyo
Nenda steers Dar uone wenye degree wanachoma chips kuku wanalipwa mshahara mkubwa sana

Kipapatio na tu chips kidogo tu mitaani elfu mbili mia Tano pale panasoma elfu 10 na matajiri,maafisa serikali nk wanagombea.Sehemu ya kuuza imekaa kibosu chips za mtaani sahani Hilo pale unapata robo tu na kipapatio Cha kuku elfu 10 imeondoka
 
Mimi mwenyewe naumia sana Mkuu yan mpka unahisi kuna watu sijui wanamuomba Mungu yupi sababu na ww unasali tena unafunga unaomnba miujiza hyo hyo lakn wanapata wengine wanaojiweza na walio vizuri kiuchumi[emoji17][emoji17]
Mungu hayupo mkuu.

Kumtegemea Mungu ni kupoteza muda.

Fanya kila uwezalo kufanikiwa sio kuweka False hopes kwa Mungu asiye kuwepo.
 
Una amini Fiction character Mungu halafu unajipa False hopes kwamba yeye ndiye mpaji wa mahitaji yako.

Wakati kutwa kucha unahenya kutafuta pesa kwa nguvu za mwili wako ili kukidhi mahitaji yako.

Mnajifariji na illusion God.

Sijui mnawazaga kwa kutumia makalio, nyie wafia dini?
Dah
 
Swali langu likikuja nilidhani wakati wa kumuombea marehemu nawe huwa unaungana kumuombea pia kwa Mungu. Na kama ni hivyo nilijiuliza huwa unamuombea kwa Mungu yupi wakati unaamini Mungu hayupo?! Ndio mantiki ya swali langu hili.
Unapotushinda kwa hoja ni hapo kwenye uthibitisho kwa maana unataka kuamini uwepo wa Mungu mpaka umuone kwa macho? Yanayotokea duniani huoni kuna nguvu isiyoonekana inasababisha?( Mungu)?. Kwahiyo wewe tumaini lako ni nini hapa duniani( egemeo)
Je unadhani hata tukio la kuzaliwa kwako ni matokeo ya mbegu (BABA) na yai ( mama) na si kwamba pia kuna nguvu za Mungu katika uumbaji wako?
Nguvu hiyo isiyo onekana uta iitaje Mungu wakati hata haijawahi kuonekana?

Kwa nini una conclude nguvu hiyo ni Mungu?
 
Inahuzunisha sana kuona kazi wafanyazo watoto waliosomeshwa kwa gharama wakiwa bodaboda na wachoma chips.

Mzazi kugharamia masomo ya mwanao ili aje kuwa mpambaniaji wa kazi hizo na za namna hiyo au kutokuja kuwa na future yoyote mtaani inaleta huzuni kwa mtoto mwenyewe hata kwa mzazi pia.

Wanasiasa hawafanyi ujinga huu kamwe wao na kizazi chao wanaandaliana future bora watoto wao. Hakuna mwanasiasa hata mmoja ataruhusu mwanae awe boda boda au mchoma chipsi wala kutanga tanga mtaani hovyo bila future yoyote ile.

Mzazi jukumu lako lisiishie kuzaa na kupeleka mtoto shule pekee bali muandalie na future bora mtoto wako.

[IMG alt="lukesam"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/275/275627.jpg?1500562796[/IMG]

lukesam

JF-Expert Member​

  • "Hatuwezi kuwa matajiri wote kama Bakhresa lakini ni vizuri sisi watu weusi tukajifunza kwao na jamii nyingine kama za wahindi.
Inawezekana wazee wetu walishakosea huko nyuma ila sasa ni muda wa kujisahihisha na kuwa bora kuliko wao.

Wazazi wa kiafrika wana tabia za kichoyo na kibinafsi, hata akiwa na duka lake hataki mtoto wake auze au ajue jinsi ya kuendesha biashara, anaogopa kuibiwa hata kijana wake hamuamini.

Watoto wetu wanahangaika sana kutafuta ajira kwasababu walienda shule kusomea taaluma za ndoto zao bila kujua baada ya kumaliza wataenda kufanyia kazi wapi. Tofauti na sisi, hawa wenye asili ya kihindi na matajiri wengine, watoto wao wanaenda shule kusomea taaluma ambazo wanajua wakitoka hapo wataenda kupata ajira kwenye miradi ya familia.

Tuweke nguvu katika kuanzisha miradi ya kifamilia, familia za kitanzania tuache ubinafsi. Ndio maana hata ukimshauri mtu aandike wosia au agawe mali zake akiwa hai anakushangaa, mzee kabisa anataka afe akiwa anamiliki mali zake zote.

Suluhisho la kusomea uhasibu au uchumi na kuishia kuwa muuza chipsi au bodaboda ni kuanzisha miradi ya kifamilia. Binafsi naona hii itapunguza sana tatizo la ajira na hali ya umaskini katika familia zetu.

Inaumiza sana kupoteza miaka mingi shuleni na kuishia kufanya kazi ambazo hata hazihitaji elimu".
Familia ,ndugu Ni wabinafsi na wachoyo

Hilo ndio kuu
 
Zote ni kazi isipokuwa inategema unafanya kwa namna gani, Hakimu Mahakama za Wilaya tunawalipa 1,700,000/-[milioni moja laki saba ]kwa mwezi na kwa siku 56,666.6/- [elfu hamsini na sita]

Muuza Maandazi pale Ferry-upande wa Kigamboni banda la tatu mkono wa kushoto anafunga 9,000,000/-[milioni tisa]kwa mwezi na Tshs 300,000/- [laki tatu] kwa siku.

Kwa Mwaka HAKIMU = 20,400,000/- [Milioni ishirini na laki nne]

Kwa Mwaka Muuza Maandazi Ferry = 108,000,000/- [milioni mia moja na nane]

Muuza maandazi wa Ferry halipi kodi wala hana TIN, TFDA , OSHA, NSSF, FIRE na manispaa wala hawaangaikinnaye maana ni mmchinga, ukishuka tu ferry banda la tatu lililojaa vitafunwa, .
Kila pantoni inaposhusha anauza si chini ya elfu 30 sasa ukitoa ghrama zote ndio inabaki laki tatu.
Wafanyakazi wanaingia kwa shifti.
HV wew ndio jaji kweli

HIV kwann usifiche ufukara wako
 
Sasa mimi siamini Mungu yupo, nitaomba vipi kwa huyo Mungu?

Pia, tofautisha uthibitisho na kuona kwa macho. Unaweza kuona kwa macho kitu ambacho hakipo. Mara nyingi tunaona movies za watu waliokufa, tunawaona kwa macho, je, hilo linathibitisha wapo? Halithibitishi.

Unaweza kuthibitisha, kwa kutumia mantiki, kwamba, mama mzazi wa mtoto ni lazima atakuwa na umri mkubwa kuliko mtoto, bila kumuona mama wala mtoto, kwa kutumia mantiki tu.

Yani katika ulimwengu huu non-relativistic, haiwezekani mtoto akawa na umri mkubwa kuliko mama yake mzazi. Hili halihitaji kumuona mama wala mtoto kuelewa.

Mimi sihitaji kumuona Mungu, nahitaji uthibitisho wenye logical consistency, usio na contradiction, kwamba Mungu yupo.

Nasema hivi, huwezi kuthibitisha kwamba Mungu yupo, kwa sababu hayupo. Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.

Kwamba yanayotokea duniani kuna nguvu isiyoonekana inayoyasababisha haimaanishi nguvu hiyo ni Mungu.

Kama vile ambavyo, ukweli kwamba wewe una baba mzazi haumaanishi baba yako mzazi ni James Bond 007. Ukisema baba yako mzazi ni James Bond 007, kama fact, tupe ushahidi na uthibitisho wa hilo.

Usiseme tu "mimi lazima nina baba mzazi, haiwezekani ikawa nimejizaa mwenyewe, hivyo, lazima baba yangu ni James Bond 007". Hapo itakuwa umeunganisha mambo yasiyo na muungano. Logical non sequitur fallacy.

Vivyo hivyo, ukweli kwamba mambo yanayoendelea duniani yana nguvu zisizoonekana zinqzoyasababisha, haumaanishi nguvu hizo ni kazima ziwe Mungu.

Umeuliza tumaini langu ni nini? Tumaini langu ni uwezo wa watu kujifunza na kukabikiana na mazingira yao, elimu. Sihitaji Mungu. Kwa sababu Mungu hayupo. Watu wamekufa maelfu ya miaka kwa kukosa dawa za antibiotic, mpaka mwaka 1928 wanasayansi wakazigundua. Huyo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote alikuwa wapi miaka yote akaachia watu wafe kwa vidonda tu kwa sababu hawakujua kutengeneza antibiotic?

Kuzaliwa kwangu hakuhitaji Mungu, kunahitaji baba na mama yangu tu.

Kwa sababu Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, angekuwapo, ulimwengu usingekuwa na mapungufu uliyonayo leo.

Na kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
Kwa hapa umenibana ngoja nijipange tena..
 
Kipapatio na tu chips kidogo tu mitaani elfu mbili mia Tano pale panasoma elfu 10 na matajiri,maafisa serikali nk wanagombea.Sehemu ya kuuza imekaa kibosu chips za mtaani sahani Hilo pale unapata robo tu na kipapatio Cha kuku elfu 10 imeondoka
Umesomea Public Relation alafu unaishia kua kibarua muuza kitimoto roast na choma kwenye Bar fulani, eti utakua billionaire?
 
Kwani boda boda sio kazi?mnataka mkisoma muendeshe nagari makari
Yani unaona ni sawa kabisa mtu asome halafu aje kuendesha bodaboda?

Umuhimu wa elimu utakuwa ni upi kama wasomi wana ishia boda boda?

Sasa si bora elimu mwisho iwe form four kuliko serikali kupoteza gharama kubwa kuwapa mikopo wanafunzi wa chuo kikuu wasio na msaada wowote kwa Taifa.

Yani serikali inapoteza fedha kwenye elimu ya chuo kikuu halafu inasifu wasomi kuwa bodaboda na mama ntilie.
 
Mwanangu unajua kijiwe cha chipsi kina pesa chafu?

Watu tunalaza 80,000 mpaka 100,000 after all expenditures daily we unachukulia poa chipsi.?

Najua kuna chipsi vibanda haviingizi hiyo hela, sawa. Lakini nanyi huko kazini si wote mnaingiza hela nzuri. Wengine wana degree tangu mwaka 2015 waajiriwe kwa mshahara wa 750,000 mpaka leo hii hawajapata nyongeza. Sijui ndio Samia mwaka jana kaongeza kidogo.

Sema wabongo mmekariri kila aliyepita shule lazima aajiriwe hata kama analipwa kiduchu ili tu mzazi afurahi kuona mwanawe yuko kwenye payroll na akisimama kujitambulisha aseme nafanya kazi sehemu fulani ilihali ni kapuku.

Cha msingi maokoto, nunua kigari chako, jenga nyumba huko Kibamba.
Shida mkiona mtu ana gari mnawaza anafanya kazi wapi? Ushawahi kufikiria mtu amejiajiri?
Sasa mkuu huo mtaji wa kufungua kijiwe cha chipsi utadondoka tu kutoka mawinguni? Unachokiongea kinaweza kufanya kazi kwa mtu aliepata ajira kwanza halafu ndio ajichange kuongeza chanzo cha mapato sio kwa jobless anaeamka asubuhi akiwa hana kitu na wala ajui ataenda wapi kupata riziki
 
Accessibility
Muajiriwa anauelipwa hio 700K anaweza kumiliki vibanda km hivyo zaidi ya vitano ila wewe mzee mchoma chips sio rahisi kuwa Muajiriwa wa mshahara wa 700K

Reputation
Muajiriwa wa 700K muda wote msafi rahisi kuji Address kwa watu na kutambulisha always he/she is presentable na anaheshimika ila wewe mchoma chips huna yote haya.

Workdone
Muajiriwa wa 700K anaingia kazini morning na kutoka saa 8 na pia jumamosi na jumapili harndi job, ila wewe mchoma chips unafungua morning hadi saa 4 usiku na huna weekend....Pia Muajiriwa anafanya soft works most of time ana relax job ila mchoma chips uamke 11 uende sokoni kubeba gunia za viazi, mkaa nk ukate gunia la viazi, ukaange siku mzima jikoni "nataka rojorojo" "nataka kavu ikaushe" this is hell.

Risk And Security
Muajiriwa wa 700K hata uumwe mwezi mzima still you receive your pay, wewe ukiumwa siku moja tu kazi unayo, Muajiriwa ana mafao zaidi ya 60 Millioni baada ya kazi wewe huna chako nk

This life is full of uncertainty ukiwa na Ajira ya 700K kwa asilimia kadhaa financial uncertainty zitapungua kwako ila mchoma chips Mungu ajaalie kwakweli.

Financial Credit
Mfanyakazi wa 700K anaweza kopa zaifi ya 20 Million ajafanya most potential move, ila mchoma chips hata 100K mtu kukukopesha mtiti.

Ni vizuri pia kujifariji kwasababu hakuna namna na haya maisha.
Wee umeongea ukweli mtupu
 
Moja ya mistake sitaki kuifanya ni mwanangu azaliwe Afrika hasa Tanzania.

Hili kosa halijirudii kwa kizazi changu kijacho.

Robert Mugabe aliwahi kusema kwamba

"Once you are born in Africa life is automatically leading you 1-0"
Hehehehe daa umetisha aisee , Africa Kuna shida sana katika life cycle yetu hapo hata kama tutakataa lakini ndo ukweli
 
Umesomea Public Relation alafu unaishia kua kibarua muuza kitimoto roast na choma kwenye Bar fulani, eti utakua billionaire?
Shida Iko wapi? Kampuni uza kitimoto ikikua kubwa ndio utakuwa HR

Hata bila kampuni kukua mfano umefungua sehemu ya kitimoto wewe ndie bosi umeajiri watu wawili mmoja jikoni na mwingine mhudumu skill zako za HR si unatakiwa uzitumie? Au hukuelewa ulichosoma kazi za HR anatakiwa atumie wapi?
 
Back
Top Bottom