Mzee Benjamin Mkapa asherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuzindua kitabu chake cha 'My Life, My Purpose'

Mzee Benjamin Mkapa asherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuzindua kitabu chake cha 'My Life, My Purpose'

Mzee mkapa anasema uwepo wa vyama vingi vya siasa vinadhoofisha demokrasia kwa sabab wengi wanaingia kwa maslahi
 
Jana katika uzinduzi wa Kitabu cha Raisi Mstaafu Benjamin William Mkapa, Prof. Semboja alisema nakala hizi zinapatikana Morogoro Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza na Arusha. Je, kwa Arusha Kitabu hiki kinauzwa Bookshop gani?
 
1. Mzee wa kuita wananchi malofa.
2. Engineer wa mauaji ya Mwembechai na Pemba
3. Mastermind wa EPA
4. Mmiliki wa ANBEN
5. Mwasisi wa Mikataba MIBOVU ya madini. walipomkosoa akasema ni WAVIVU WA KUFIKIRI
 
Ingependeza Kama angeomba radhi kwa kwa niaba ya baba yake! Inaonyesha hakuheshimu kazi ya ualimu! Anasema ikishindikana uwe mwalimu! Yaani kwake kazi ya ualimu ni baada ya kukosa zingine zote!!!!
Mwalimu tulia
Hiyo ni historia huwa haibadilishwi
Amesimulia matukio yalivokuwa
 
Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi toa nasaha kwa mtu ambaye ni kiongozi ama ana ndoto za kuwa kiongozi.

Mwalimu alisema,ukiwa kiongozi kuna changamoto nyingi ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza athiri ufanisi ama ndoto zako wakati wa kipindi chako Uongozi.

Mwalimu alisema,Ukiwa Kiongozi utakuwa na presha ya Mke/Mme wako,je atakuwa nyuma yako kukutia moyo hasa pale utakapokuwa hupatikani nyumbani na muda mwingi ukitumikia umma ama jamii?

Presha ya pili ni ndugu na marafiki,hii Ni changamoto nyingine,Ndugu na marafiki zako huamini unapokuwa katika nafasi basi nao wanatakiwa kunufaika na nafasi yako.

Presha ya tatu ni wasaidizi na washauri wako,je wamekuzunguka ili kuyafanya maono ,ndoto,dhima na malengo yako kama kiongozi ufanikiwe ama wanataka kutumia fursa hiyo kukupotosha ili wao wafanikiwe kupitia wewe?

Kwenye kitabu cha My life,My Purpose, Mzee Mkapa anasononeshwa na jinsi Presha hizi ambazo Mwalimu Nyerere aliyatahadharisha zilivyofifisha ama kuathiri furaha ya Mzee Mkapa kuwa kiongozi mkuu wa nchi Kwa Miaka 10.

1. MARAFIKI
Mzee Mkapa anakiri na kusononeshwa jinsi marafiki na washauri wake walivyompotosha kwenye sakata la EPA,Walipomwambi pesa hizo zitatumika kwenye kampeni lakini zikaishia mikononi mwa Wachache.

2. NDUGU
Mzee Mkapa anasononeka jinsi alivyonyoshewa vidole kwa madai ya ndugu zake kunufaika na utawala wake hasa wakati wa ubinafsishaji.

3. WASAIDIZI
Mzee Mkapa anasononeka jinsi Baadhi ya wasaidizi wake walivyompotosha na wengine kutaka kubadilisha Katiba ya Zanzibar.

4. FAMILIA
Mzee Mkapa anakiri kuwa ni ngumu sana Kwa mwanamke kukubali kuishi nae kwani muda mwingi alikuwa katika majukumu ya kikazi na kutopatikana nyumbani na hata kukaa Na familia,Mzee Mkapa anasema,Mama Anna Ni mwanamke wa aina yake aliyekubali na hata kuvumulia kuishi nae na hata kuwalea watoto bila yeye Mkapa kupatikana muda mwingi.

5. SIASA KUGEUKA KUWA UADUI BADALA YA USHINDANI
Mzee Mkapa anakiri jinsi siasa zilivyotia doa maisha yake Na malengo yake Baada ya kushuhudia wakati wa Uongozi wake watu wakifariki Kwa sababu ya harakati za kisiasa wakati wa kipindi chake cha Uongozi.

6. SIASA
Mkapa anakiri wapo waliompotosha kuhusu pesa za EPA kuwa zitasaidia kampeni za Chama chake ,hili ni doa kwake,Mkapa anazidi kusononeshwa na chama chake kuwa Mpaka Sasa kinadhani kipo Kwenye mfumo wa Chama kimoja.

Siasa iliyobadilishwa kutoka kwenye ushindani Na kuwa uadui ndiyo ilisababisha Baadhi ya Watanzania kupoteza maisha na wengine kukimbia nchi.

Maana waliouawa,waliuawa wakiwa kwenye harakati za kisiasa zilizotambulika kisheria mwaka 1992.

Siasa zisiwe uadui bali ziwe ni ushindani.

7. KATIBA
Katiba ya Tanzania haiwapi hofu viongozi bali inawapa jeuri ya kufanya chochote wanachotaka Na hata kuyafumbia macho yanayofanywa Na wasaidizi wake kwa kukusudia ama kutokukusudia maana Katiba inawalinda katika kila wafanyalo Kwa nafasi ya Urais,Mzee Mkapa anasononeshwa na yaliyotokea wakati wa Utawala wake,lakini Kwa mtazamo wangu hayawezi kuwa funzo Kwa wengine maana lolote utakalolifanya kwa nafasi ya Urais linakuweka salama.

8. WAKOSOAJI
Yote yanayomsononesha Mzee Mkapa Kwa sasa yakipigiwa kelele na baadhi ya vyombo vya Habari,wanaharakati na washindani wake,lakini walionekana wasio mtakia heri ama Rais Mkapa,lakini Sasa yamegeuka kuwa sononeko kubwa Kwa Mzee Mkapa.

9. MFARIJI MKUU
Mzee Mkapa anakiri ukiwa kiongozi basi Wewe ndiyo mfariji mkuu,Mkapa anasema moja ya madhaifu yake ni kuwa Mfariji mkuu Na anakiri wazi katika Viongozi waliopewa kipawa cha Ufariji Mkuu ni Jakaya Mrisho Kikwete,Mzee Mkapa anawapa somo wale wote walio Kwenye nafasi za Uongozi kujua wao Ni wafariji wakuu, katika hali ya huzuni Na majonzi,unaowaongoza wanatarajia uwape Faraja badala ya kutia msumali wa moto Kwenye nyama inayoteseka na majonzi.
 
Hakuna marefu yasiyo na nchi. Mwisho wa siku tunarudi pale pale tulipoanzia
 
MMMM Nasubiri kitabu cha JIwe.Haaaa Good analysis ila sasa marais wana kinga katiba ingekuwa inaruhusu tungewaulizia kwenye vyombo vya mahakama na ingewapunguzia jeuri watawala
 
Kuliko kubaki akisononeka, na kwakuwa Mzee ana kinga na ulinzi, basi nitamani kusikia ama kuona Mzee akiwataja kwa majina wale wote walio husika kupiga pesa ya EPA.
 
Mambo mengi yamezungumzwa kwenye tukio la uzinduzi wa kitabu cha Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa; 'My Life, My Purpose' (Maisha Yangu, Malengo Yangu). Muhtasari wa kitabu chenyewe unaonesha ni kitabu kizuri sana, ni kitabu cha lazima kusoma ( A must read book). Ni moja ya vitabu ambavyo kila msomaji wa vitabu na wanafunzi wa Sekondari na vyuo wanapaswa kuvisoma.
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo isipokuwa mimi binafsi kwa sababu ya utukutu wangu nakiita kitabu hiki 'An Admittance Of Old Man' (Ungamo La Shaibu).
Ni 'Kiri' kwa sababu ya mambo makubwa matatu; moja ni mauaji ya wafuasi wa CUF yaliyotokea January 2001 kule Pemba. Pili ni matumizi ya Fedha za 'Wizi' maarufu kama fedha za EPA ambazo kwa mujibu wa Rais Mkapa zilitumika kwenye kampeni za Urais mwaka 2005, (kampeni nyepesi kuwahi kutokea kwa CCM tangu kuanza kwa vyama vingi).
Tatu ni CCM kujiona ipo kwenye mfumo wa Chama kimoja, na hili liwe ujumbe kwa Rais Magufuli.
Pamoja na mambo mengine mengi mazuri lakini hayo machache yananipa kiburi cha kukiita kitabu hiki 'Ungamo La Shaibu'
Kitu kimoja alichosahau Mh. Mkapa ni ile kauli yake aliyotoa kwenye viwanja vya Jangwani - August 2015; 'WATANZANIA NI WAPUMBAVU NA MALOFA'.
Natumai mzee Mkapa atazungumzia kauli hii siku yoyote apatapo fursa! Kabla jua halijafifia.

credits; kutoka ukuta wa facebook wa Dr. Christopher Cyrilo;
 
Kama kwenye suala la KATIBA hajazungumza ukweli kuwa KATIBA YA JAJI WARIOBA ndiyo inayobeba matakwa na mapendekeza ya Wananchi na ndio inayopaswa kutumika basi hata yeye ni MNAFIKI TU.
 
Mungu akuzidishie baraka na maisha yenye furaha Rais wetu mstaafu mzee Mkapa. Leo umetimiza miaka 81, Hongera sana.

Amen!
huyu ndiy aliyeanzisha board ya mikopo na kufanya wanufaika kukatwa 8% aliyepo madarakani kaongeza hadi 15% kabisa ili awakwamue wanufaika.
huyu na aliyepo madarakani ndiyo waliouza nyumba za umma kwa ndugu na ... wao (rejea issue ya mussa magufuli na bwana magufuli kukimbilia kituo cha polisi pale mabatini kisa kaandikwa... alidai wanataka kumuua)
huyu kupitia kwa wazir wake MRAMBA ndiyo waliotaka tule majani ili ndege ya raisi inunuliwe
huyu ndiye aliyeuza kiwira Coal mining kwa familia yake.
aliuza viwanda kwa makaburu na kuwafokea waliohoji kwamba wanawivu wa kike
Kwamujibu wa maandiko huyu ni muovu asiyepaswa kuombewa
 
Mkapa kazungumza mengi lakini amekuwa na lugha ya kujitetea labda kwa sababu Bilal hayupo kutueleza upande wa pili anakiri kuhusika kuingizwa mkenge kwenye epa lakini ametoa kauli yenye ukakasi kuwa aliambiwa hizo pesa zingeisaidia ccm ili nchi ipambane na rushwa huwa haiitaji pesa zisizoeleweka kuingia madarakani labda kwa kujua madhambi aliyofanya alifanya kila njia Dr. Salim asiweze kuwa mgombea urais wa ccm maana angepata ukweli angemshugurikia, pia amezungumzia kashifa ya rada wakati ikinunuliwa watu wengi walipinga lakini anakubali tuliinunua kwa bei kubwa na baadae chenji ikarudishwa ila hasemi waliomshauri vibaya walichukuliwa hatua gani jambo jingine ni kufanya biashara wakati akiwa ikulu anasahau mtu aliyesema anamuenzi Mw. Nyerere alisema ikulu ni mahali patakatifu aache unafiki wa kujifanya anamuenzi wakati kiukweli alikuwa anafanya kinyume na mambo aliyoyataka baba wa Taifa ukweli mkubwa yeye amechangia kuirudisha Tanzania nyuma badala ya kwenda mbele na ili tusirudie hayo makosa inabidi kuwaondolea marais kinga ya kutoshitakiwa ili kila mtu akiingia ikulu afanye kazi ya kuwatumikia wananchi
 
Kama kaelezea kuhusu ununuzi wa NBC pia itabidi tukanunue Kitabu wa Kunyumba.
iliuzwa siku ya public holiday hahahahahah. kuna wajinga wanawaita wapinzani majizi ukiwauliza wameiba nini wanabung'aa
 
Back
Top Bottom