Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi toa nasaha kwa mtu ambaye ni kiongozi ama ana ndoto za kuwa kiongozi.
Mwalimu alisema,ukiwa kiongozi kuna changamoto nyingi ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza athiri ufanisi ama ndoto zako wakati wa kipindi chako Uongozi.
Mwalimu alisema,Ukiwa Kiongozi utakuwa na presha ya Mke/Mme wako,je atakuwa nyuma yako kukutia moyo hasa pale utakapokuwa hupatikani nyumbani na muda mwingi ukitumikia umma ama jamii?
Presha ya pili ni ndugu na marafiki,hii Ni changamoto nyingine,Ndugu na marafiki zako huamini unapokuwa katika nafasi basi nao wanatakiwa kunufaika na nafasi yako.
Presha ya tatu ni wasaidizi na washauri wako,je wamekuzunguka ili kuyafanya maono ,ndoto,dhima na malengo yako kama kiongozi ufanikiwe ama wanataka kutumia fursa hiyo kukupotosha ili wao wafanikiwe kupitia wewe?
Kwenye kitabu cha My life,My Purpose, Mzee Mkapa anasononeshwa na jinsi Presha hizi ambazo Mwalimu Nyerere aliyatahadharisha zilivyofifisha ama kuathiri furaha ya Mzee Mkapa kuwa kiongozi mkuu wa nchi Kwa Miaka 10.
1. MARAFIKI
Mzee Mkapa anakiri na kusononeshwa jinsi marafiki na washauri wake walivyompotosha kwenye sakata la EPA,Walipomwambi pesa hizo zitatumika kwenye kampeni lakini zikaishia mikononi mwa Wachache.
2. NDUGU
Mzee Mkapa anasononeka jinsi alivyonyoshewa vidole kwa madai ya ndugu zake kunufaika na utawala wake hasa wakati wa ubinafsishaji.
3. WASAIDIZI
Mzee Mkapa anasononeka jinsi Baadhi ya wasaidizi wake walivyompotosha na wengine kutaka kubadilisha Katiba ya Zanzibar.
4. FAMILIA
Mzee Mkapa anakiri kuwa ni ngumu sana Kwa mwanamke kukubali kuishi nae kwani muda mwingi alikuwa katika majukumu ya kikazi na kutopatikana nyumbani na hata kukaa Na familia,Mzee Mkapa anasema,Mama Anna Ni mwanamke wa aina yake aliyekubali na hata kuvumulia kuishi nae na hata kuwalea watoto bila yeye Mkapa kupatikana muda mwingi.
5. SIASA KUGEUKA KUWA UADUI BADALA YA USHINDANI
Mzee Mkapa anakiri jinsi siasa zilivyotia doa maisha yake Na malengo yake Baada ya kushuhudia wakati wa Uongozi wake watu wakifariki Kwa sababu ya harakati za kisiasa wakati wa kipindi chake cha Uongozi.
6. SIASA
Mkapa anakiri wapo waliompotosha kuhusu pesa za EPA kuwa zitasaidia kampeni za Chama chake ,hili ni doa kwake,Mkapa anazidi kusononeshwa na chama chake kuwa Mpaka Sasa kinadhani kipo Kwenye mfumo wa Chama kimoja.
Siasa iliyobadilishwa kutoka kwenye ushindani Na kuwa uadui ndiyo ilisababisha Baadhi ya Watanzania kupoteza maisha na wengine kukimbia nchi.
Maana waliouawa,waliuawa wakiwa kwenye harakati za kisiasa zilizotambulika kisheria mwaka 1992.
Siasa zisiwe uadui bali ziwe ni ushindani.
7. KATIBA
Katiba ya Tanzania haiwapi hofu viongozi bali inawapa jeuri ya kufanya chochote wanachotaka Na hata kuyafumbia macho yanayofanywa Na wasaidizi wake kwa kukusudia ama kutokukusudia maana Katiba inawalinda katika kila wafanyalo Kwa nafasi ya Urais,Mzee Mkapa anasononeshwa na yaliyotokea wakati wa Utawala wake,lakini Kwa mtazamo wangu hayawezi kuwa funzo Kwa wengine maana lolote utakalolifanya kwa nafasi ya Urais linakuweka salama.
8. WAKOSOAJI
Yote yanayomsononesha Mzee Mkapa Kwa sasa yakipigiwa kelele na baadhi ya vyombo vya Habari,wanaharakati na washindani wake,lakini walionekana wasio mtakia heri ama Rais Mkapa,lakini Sasa yamegeuka kuwa sononeko kubwa Kwa Mzee Mkapa.
9. MFARIJI MKUU
Mzee Mkapa anakiri ukiwa kiongozi basi Wewe ndiyo mfariji mkuu,Mkapa anasema moja ya madhaifu yake ni kuwa Mfariji mkuu Na anakiri wazi katika Viongozi waliopewa kipawa cha Ufariji Mkuu ni Jakaya Mrisho Kikwete,Mzee Mkapa anawapa somo wale wote walio Kwenye nafasi za Uongozi kujua wao Ni wafariji wakuu, katika hali ya huzuni Na majonzi,unaowaongoza wanatarajia uwape Faraja badala ya kutia msumali wa moto Kwenye nyama inayoteseka na majonzi.