Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Huyu Mzee angekuwa mkweli tu awataje na walio mponza!! uwenyekiti wa chama cha siasa Taifa haupatikani kwa lele mama, ni lazima intelligensia ya chama ijiridhishe pasi na shaka juu yako . Hata huko CCM huwezi kuibuka tu eti unautaka uwenyekiti CCM Taifa - thubutu!!.
 
Wanasiasa WOTE ni wachumia tumbo tu. Sasa nendeni mkafanye kazi na muwaachie siasa wanasiasa maana hiyo ndio ajira yao.
 
Yaani siku zote hizo - huyu jamaa hakuua kama hiki chama kina mwenyewe mwenye hati Miliki? Hata sisi tulio huku nje - tunafahamu fika - hicho Chama kina Mmiliki wake. Sasa yeye kaijaribu sumu kwa kulamba.
 
SUMU HAILAMBWI KWA ULIMI,JARIBU KUGOMBEA UENYEKITI WA CHADEMA TAIFA UONE CHA MOTO. SUMAYE KASHITUKA MAPEMA
 
Hapana Sumaye kaonewa .Kamati kuu ya chadema ilimwona anafaa na ndie alikuwa mgombea pekee.Kulikuwa na sababu gani ya kuitisha kura Tena?
Ndo democrasia yenyewe hiyo.Hakuna kupita bila kupingwa huku huo utaratibu haupo kabisa.
 
Sasa anayewaongoza alipata div zero , hapo hamna chama ni wahuni Tu fulani
Yaani hawafai hata kupewa kijiji, majimbo yote waliyoshinda wameyatelekeza wapo tu kumsujudia Mbowe
 
Siasa nyingi za Afrika njaa ndiyo inaharibu. Hivi Lowasa pamoja na kupata kura 6M against mshindi 8M aliamua kuasi nakurudi Rumumba, Just imagine watu wamejitolea ku- risk uhai wao, unaenda nao, then unarudi kula matapishi. Kweli ni busara watu wa aina hizo kuwaogopa coz any time wanaweza uza chama. So wale wahamiaji twende nao lkn tuwe makini hatuna imani nao.
Yaani zee la mvi tumeliamini tukalipa nafasi, then likaasi!!! hilo ni fundisho kwa kila mwanachama halisi, wale wa njaa kama mwita waitara, lowasa na yule meya wa Arusha, wamenisononesha kwelikweli, bora wangeondoka na kukaa kimya kuliko uharo wanao utoa.
 
Sumaye kaondoka CHADEMA. Hajiungi na chama chochote cha siasa.
Umeamini na wewe,sidhani kama kuna mwanasiasa anaweza kuishi kama mimi na wewe. Siasa ni kama nyama ya mtu,ukishaionja huwezi kuacha.
 
Siku/Wiki/Miezi michache ijayo utasikia kajiunga/karudi CCM...

Kwa sasa tufanye anaendelea na mazungumzo na wakuu wa nyumba yake ya awali...
 
Back
Top Bottom