Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Na wote wenye zile chembe chembe waanze kujiondoa wenyewe.....dawa ya fangasi maji ya betri tuu.....pole pole inaisha....
 
kwa hiyo kila anayeshauri anatakiwa kuanzisha chama?
Kama anaona ana itikadi tofauti na vyama vilivyopo ni bora aanzishe chama chake, lakini siyo kulazimisha itikadi zako zikubaliwe katika vyama vilivyopo.
 
akapumzike zake kibaha achunge mbuzi siasa zishamtupa mkono
 
Binafi demokrasia ipo CHADEMA kupita vyama vyote ila tu imezoeleka sana kutoka kwa wanasiasa wapenda vyeo pale wanaposhindwa nafasi basi huhaha na kudhubutu kuahama huku wakitoa mapungufu lukuki ya chama lengwa, cha ajabu leo yuko chadema anasema jinsi gani ccm walivyo na hujuma kupitiliza ahh kashinwd chadema anahamia ccm yale aliyoyasema juzi kashasahau anaanza kusema jinsi ccm ilivyo nzuri na kusema mabaya ya CHADEMA. Hivyo hawa wanasiasa hasa wa kuhamahama ni watu wa kuwa nao makini sana kupita kiasi
 
Ni kisingizio tu, Lipumba kakaa tangu lini, afadhali hata CHADEMA fomu wanakupa ujaze, Kule CCM marufuku hata kuinusa.
Bora wenzenu wanapokezana ila nyinyi Mtu akionesha ana dalili za kutaka uenyekiti na ana sifa na uwezo anaundiwa zengwe aonekane msaliti au arudi kwa baba muumba mbingu na nchi katika mazingira ya kutatanisha.
 
@jd41,Kila anayetaka kugombea uenyekiti, anataka kumdhuru? Ndio yaleyale ya akina Zitto, ati wanataka kumgeuka, mara wasaliti!
 
Huyu alikuwa anatafuta sababu ya kujiondoa ila akawa hana sasa kaamua kutumia hili swala la uchaguzi kama sababu.

Siku si nyingi mtamsikia karudi CCM arudishiwe mashamba yake.
 
...Kaka yangu Frederick Tluway Sumaye, shikamoo kaka yangu. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu tulikutana nawe mwaka 2012 Iringa (sikumbuki jina la hotel ila ilikuwa mtaa adjacent na ilipokuwa Barclays Bank). Ni kipindi ulikuwa na "figisu" na Mh Mary Nagu japo sikumbuki kwa sasa ilikuwa ni kwa ajili ya nini. Tuliongea mengi, ilikuwa wewe au KONYAGI?

Nilishangaa baada ya siku nyingi kupita kusikia umehamia CHADEMA, lakini kwa kukumbuka uliyoniambia siku hiyo (mbele ya mwalimu fulani wa Ruaha University) niliamua kukupa benefits of doubt.
Najua utayakumbuka yote niliyoaandika hapa. Wewe ni Mlutheri mwenzangu, so please tell me my brother. Niendelee kuamini uliyoniambia au haya uliyotuambia sasa?
 
Ila alichofanyiwa CHADEMA hakikuwa sahihi, pamoja na madhaifu yake kama alikuwa hatakiwi aenge elezwa tuu na si kudhalilishwa namna ile, ni kweli CHADEMA tuna hasira kweli kweli na 'dola' lakini haikuwa sahihi kumbwagia hasira zetu Sumaye.
Kukubali kugombea kuna mawili,kushinda au kushindwa hivyo demokrasia siyo kushinda tu hata kushindwa ni demokrasia.walioliweka neno mheshimiwa kisheria walikosea sana.
 
Nasema ni aibu kubwa kwa Waziri Mkuu mstaafu kukiri hadharani kuwa analazimika kuachana na siasa eti kwakuwa anamuogopa kiongozi wa chama cha upinzani. Anaogopa maneno aliyosema Kiongozi wa Upinzani.

Ila sishangai maana anayeogopwa amewahi kuzoa mawaziri wakuu wastaafu wawili kwa mpigo na kuwafanya kuwa wapinzani.

Kama Waziri Mkuu mstaafu anamuogopa kiongozi wa upinzani basi kiongozi huyo ni imara sana!
 
Back
Top Bottom