Uchaguzi 2020 Mzee Kikwete: Ninakopanga sijafukuzwa

Uchaguzi 2020 Mzee Kikwete: Ninakopanga sijafukuzwa

Huyu Jakaya kikwete Rais mtaafu amenishangaza sana jana kwa kauli yake ya kuishi nyumba ya kupanga na bado ana mkataba na mwenye nyumba.

Kichangia neno katika kupokea nyumba za vingozi mzee Kikwete bila aibu ametoa kauli ya kuzua chuki na taharauki kubwa sana kwa mtu kama mimi mwenye kumfahamu Kikwete kwa upana.

Kikwete amekuwa Naibu Waziri kwa miaka mingi, Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka 10 na Rais miaka 10, leo analalamika kupanga.

Amelipwa zaidi ya million 12×10 kama Waziri wa Mambo ya Nje achiliambali vyeo vyake huko nyuma.

Amelipwa million 36×10 kama Rais na marupurupu kibao. Pamoja na kiinua mgongo cha karibu nusu Billion, bado Kikwete analipwa mafao ya kutia simanzi kwa mtu wa kawaida.

Amejengewa nyumba (Ikulu ndogo) msonga na Suma JKT akiwa hata hajastaafu. Ukiingia Msoga utashangaa sana ukubwa wa Ikulu ile na miundombinu yake ya nchi zilizoendelea.

Amejengewa nyumba Bagamoyo kwa mamake na Suma JKT. Ni nyumba ya kufuru.

Ana nyumba karibu kila mkoa na mitaa kibao hapa Dar, achilia mbali alizojenga nje South Africa na Dubai.

Kwa kauli aliyoitoa jana, inatia simanzi na unafiki mkubwa sana kuwa amepanga. Je, mzee Kikwete anataka kumdanganya nani kuwa anaishi maisha ya shida na amepanga so wamjengee taratibu tena kwa uimara mkubwa?

Kama ulimsikiliza na kumwangalia Kikwete usoni, alionesha kutofurahishwa na ujenzi na kuona kama hakuridhika na ile nyumba ambayo kwa mtu wa kawaida hata tajiri ungeiona kuwa ya mapesa mengi.

USSR
Ccm mama yenu ni mmoja naye ni IBILISI SHETANI.
Mmeinyonya nchi hii na bado hamridhiki

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Nadhani ni wakati muafaka sasa wa kuwaondoa ccm madarakani maana wanatumia vibaya hela zetu za kodi, hizo hela walizotumia kujenga nyumba zingetumika kusomesha watanzania wasio na uwezo.
Heri wenye nazo wanagawana huku kwangu kukavu tia mchuzi sijui kajamba nani.. gurudumu bado ni kubwa kweli na hata kulizungusha ni shida!
Sikuona haja ya wao kujengewa nyumba kwani wamekosa nini..?
Tayari wanauhakika wa mfereji wa pesa,chakula,ulinzi,mavazi n.k
Wanatumia mipesa kunufaishana walio nufaika huku kuna wanafunzi wanakosa mikopo!,Kuna watu hawajalipwa mafao!.. hii na ikawe taswira kwa wengine na watambue kuwa unatakiwa ujipiganie utoke kwenye Lindi la umaskini hawa viongozi wapo kwaajili yao hizo nyengine mbwembwe.
 
Bora uyo tunayejua amekula wanananchi walikula wakiwemo wafanyakazi hewa walilipwa, nao vyeti feki walikuwemo ajira zimo pamoja na kundi lote ilo mishahara kila mwaka inaongezeka na barabara zimendelea . sasa huyu sijui pesa anapeleka wapi wakati izo flyover ni isani mengine yote ameyakuta tena yy ndo akayaharibu standard yake
Tatizo lake anakula mwenyewe ndo ugomvi na wananchi ulipo
 
Ile ilikuwa joke tu ili achomekee ujumbe wake bila kumkwaza au kuonekana anapingana na JPM. Yeye kusema ni kuwa wasiharakishe saaana ujenzi na kuharibu quality maana Rais aliagiza nyumba iishe by Jan 2021.

Tukichukulia kila kauli seriously, tutakufa kwa BP mapema sana

Pamoja na hayo, hii kufuru ya kuwajengea hawa watu mahekalu inatia ukakasi kidogo.
 
Bora uyo tunayejua amekula wanananchi walikula wakiwemo wafanyakazi hewa walilipwa, nao vyeti feki walikuwemo ajira zimo pamoja na kundi lote ilo mishahara kila mwaka inaongezeka na barabara zimendelea . sasa huyu sijui pesa anapeleka wapi wakati izo flyover ni isani mengine yote ameyakuta tena yy ndo akayaharibu standard yake
Point kubwa Sana hii. Kuna watu wagumu kuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndio amepanga sasa unataka akakae Msoga wakat anahitaji kuishi Dar
huo ni unafiki na roho ya kimaskin.
Wangap wana majumba yao mazuri mikoani kwao ila Dar wanapanga?
Akisema anapanga ni kweli ana nyumba ila kwa mahali anapopenda kuishi hajapata sasa ulitaka aseme ana nyumba Msoga?? kwan nan hajui kama ana nyumba Msoga??
toa roho yako ya husda wewe utaishia hivyo hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heri wenye nazo wanagawana huku kwangu kukavu tia mchuzi sijui kajamba nani.. gurudumu bado ni kubwa kweli na hata kulizungusha ni shida!
Sikuona haja ya wao kujengewa nyumba kwani wamekosa nini..?
Tayari wanauhakika wa mfereji wa pesa,chakula,ulinzi,mavazi n.k
Wanatumia mipesa kunufaishana walio nufaika huku kuna wanafunzi wanakosa mikopo!,Kuna watu hawajalipwa mafao!.. hii na ikawe taswira kwa wengine na watambue kuwa unatakiwa ujipiganie utoke kwenye Lindi la umaskini hawa viongozi wapo kwaajili yao hizo nyengine mbwembwe.
Aliyekosa mikopo ni wewe au unawasemea? mbona watu wamepata mikopo ila kama alikosa labda kuna sababu.usiwe kwa vile unawesa kuandika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo unataka kusema nini?
Wote nyie ni CCM mnashirikiana kula hii nchi.
Sasa umeingia wivu baada ya mwenzako kula zaidi.
Dawa yenu tarehe 28.
Imenibidi nirudie kuisoma ID ya mleta uzi huu kama mara nne hivi, kuthibitisha kama NI YEYE. Kwani, sio kawaida kuto kuunga mkono au kusifia kwa lolote litalofanywa na Serikali au CCM!
Leo DISHI limekaa sawa, tena nadhani ni kwa muda tu!
 
Hahaha msidanganyike, Makonda alikuwa mkuu wa wilaya na Mkoa kwa miaka 4tu, kajenga maghorofa.

Kikwete kawa rais kwa miaka 10, waziri miaka 15, kanali wa jeshi, halafu akwambie kapanga nawe masikio yakusimame, hizo akili au matope?!
 
Kaamua tu kupanga.
Nenda kaangalie kule Msoga kajenga nini.
Huyo mzee ana hela chafu.
 
Wacha nirudie tena. Hekima ni jambo la mbolea sana kwa binadamu yoyote anayeishi chini ya jua.
Na ni jambo tena la msingi sana kwa kiongozi yoyote aliyewahi kutokea kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi huku chini ya jua.
Ni hayo tu
 
Bora uyo tunayejua amekula wanananchi walikula wakiwemo wafanyakazi hewa walilipwa, nao vyeti feki walikuwemo ajira zimo pamoja na kundi lote ilo mishahara kila mwaka inaongezeka na barabara zimendelea . sasa huyu sijui pesa anapeleka wapi wakati izo flyover ni isani mengine yote ameyakuta tena yy ndo akayaharibu standard yake
Upo sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom