Mzee Mbowe anawachezea akili vijana wake wa CHADEMA, mwisho wa siku wataangukia kwenye mtego wake

Ozon

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2024
Posts
2,910
Reaction score
4,711
Baada ya hotuba yake kwenye mazishi ya Mzee Mtei (RIP), vijana wengi wanaonekana kukoshwa na hotuba hiyo, wengine wakimpongeza kwa hashtags kwenye social media. Wengine wanaona kama ni mwelekeo mzuri wa Mbowe kurudisha heshima iliyotetereka ndani ya chama chake cha CHADEMA kwa siku za hivi karibuni.

Lakini huyu Mzee atawashangaza; muda utaongea.
 
Unawaona viongozi wa sasa wa Chadema ni mapoyoyo? Mbowe amesema aliyosema lakini hayawezi kudhoofisha msimamo wa Chadema juu ya kinachoitwa maridhiano,just wait and see.
 
Mzee wa watu hana jema, akikaa kimya shida, akisema shida.
Ila anapaswa kulaumiwa kwa tabia mbaya ya 'baadhi' ya vijana alio walea huku mitandaoni.

Kwa ninavyofikiri; Chadema kama chama kina wafuasi wengi wasiopenda na wasio wanademokrasia, pengine kuliko vyama vyote nchini.
 
Atashangaaa Yeye.

Ni either Aludi kwenye mstari, Au aendelee kula buyu.
Mbowe kurudi kwenye mstari ni ndoto zisizowezekana katika uhalisia, na anautumia mwanya huo kwa baadhi ya wafuasi wake wanaodhani kwamba anaweza kurudi kwenye mstari. Mtego huo.
 
Unawaona viongozi wa sasa wa Chadema ni mapoyoyo? Mbowe amesema aliyosema lakini hayawezi kudhoofisha msimamo wa Chadema juu ya kinachoitwa maridhiano,just wait and see.
Sio mapoyoyo ila yule Mzee ni mtu wa dili wawe makini sana.
 
Kwani alichoongea Mbowe, wengine kina Heche au Lissu au Mnyika n.k hawajaongea?

Kwani CCM na serikali yake haijui kwamba inafanya ukandamizaji kwa wanasiasa wa vyama mbadala kiasi cha kuondoa dhana nzima ya demokrasia?
 
Angalizo. Mbowe ni rafiki wa karibu na mkubwa sana wa yule muovu kutoka Zanzibar. Rafiki wa adui nae yafaa kumwita adui.
 
Mzee wa watu hana jema, akikaa kimya shida, akisema shida.
Ila anapaswa kulaumiwa kwa tabia mbaya ya 'baadhi' ya vijana alio walea huku mitandaoni.

Kwa ninavyofikiri; Chadema kama chama kina wafuasi wengi wasiopenda na wasio wanademokrasia, pengine kuliko vyama vyote nchini.
Vyovyote vile, haimwondolei kuwa mtu wa dili, dalali, na msanii katika siasa za upinzani.
 
Back
Top Bottom