Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Aliyekuwa Rais kumuita aliyekuwa waziri mkuu wake kuwa ni mpumbavu na ni lofa pamoja na kuwa yeye ndiye aliye mteua kutoka katika mamilioni ya watanzania ni sawa na kujitukana mwenyewe. Mkapa asingekuwa mpumbavu angeshindwaje kutambua kuwa anaemteua ni mpumbavu? Naona kuna kila dalili ya jazba baada ya kusikia harufu ya anguko la chama chao.
 
Lowasa is a leader and Magufuli is a manager,here are their differenceses:

– The manager administers; the leader innovates.
– The manager is a copy; the leader is an original.
– The manager maintains; the leader develops.
– The manager focuses on systems and structure; the leader focuses on people.
– The manager relies on control; the leader inspires trust.
– The manager has a short-range view; the leader has a long-range perspective.
– The manager asks how and when; the leader asks what and why.
– The manager has his or her eye always on the bottom line; the leader’s eye is on the horizon.
– The manager imitates; the leader originates.
– The manager accepts the status quo; the leader challenges it.
– The manager is the classic good soldier; the leader is his or her own person.
– The manager does things right; the leader does the right thing.

BYE BYE CCM!
 
Huo ni uthibitisho kwamba ccm wametambua anguko kuu linalowasubiri, na ni lazima tuwaangushe maana hakuna namna.
 
Naimani hawa waigizaji watashughurikiwa ..Lowasa alipanda daladala mwaka gani alafu marofa yapo hapa yanakenua tu? kweli kuna watu wapumbavu na hata Biblia inawatambua, maigizo ya Lowassa ni upumbavu wa karne kutokea duniani
 
kweli nyinyi ni malofa na wapumbavu hamuelewi hata mueleweshe vipi. Sumaye hajasema anakuja komboa amekuja kuwasaidia kuongoza sababu hamjui.....wapumbavu ni nyinyi
 
Warioba alipigwa na Makonda hah hah. Jana kadhirihisha udhaifu wake mbele ya jamii iliyokuwa inamheshimu.

Alitukanwa na awanaccm wenzake sana. Lakini jana kwa hiari yake akajipileka kuongea alichoona ni kumnadi Magufuli.

Ama kweli Mkapa ulikosea kutuita sisi tuliokupa ulaji miaka 10 kumbe wako pembeni yako.
 
Lowasa nampenda ndo maana simpi kura yangu.. Nataka apumzike atibiwe ili aweze kuishi mda mrefu zaidi...

Ukimpenda lowasa huwezi kumpa kura... Ukiwa na rafiki yako mgonjwa kama lowasa sidhani kama unaweza kumpa kazi au jukumu zitto alisimamie...ukifanya hivyo utakuwa humpendi rafiki yako kwa dhati.

#okoa maisha ya lowasa kwa kumyima kura#
 

huyu jamaa kiboko yake ni mama ana tu alipomletea maneno yake ya shombo kibano alichopata hatakaa hakisahau.
 
mada hii isiunganishwe na mada nyingine.

TUWAJIDILI WATANZANIA MALOFA NA WASIO MALOFA.

neno lofa linajumuisha wazururaji, wasio na kazi na wasio na kitu yaani ni masikini.

Rais mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa kasema wapinzani ni MALOFA.


NB:
1.Malofa ni watanzania na wamo kwenye vyama vyote na wengine hawana vyama. Kwa hiyo malofa siyo wapinzani peke yao,hata ccm wamo.

2.Malofa wote ni walipa kodi.

3.Molofa wote ni wapiga kura.

4.Malofa waliopo leo upinzani , jana walikuwa malofa ndani ya CCM na ndio haohao waliomfanya Kikwete akashinda kwa 80% mwaka 2005 kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania ni masikini(malofa) na hivyo hata asilimia kubwa ya kura alizopata kikwete ni kutoka kwa malofa.

ni kweli hatukatai nchi yetu ya Tanzania ina malofa wengi sana wakiwemo wapinzani, wakiwemo CCM na wale wasio na vyama.

Je ni nani alipenda kuwa lofa yaani asiye na kazi yoyote na asiye na kitu?

huu ulofa kauleta nani? wakati tunaishi kwenye nchi tajiri?

utajiri wa nchi yetu ni utajiri wa watanzania wote lakini leo sisi tu malofa.

Serikali ya CCM hasa ikiongozwa na Mkapa ndio imewafanya watanzania kuwa MALOFA.

ili mtu asiwe lofa alipaswa kuwa ana kazi.

ieleweke kuwa wajibu wa serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata ajira/kazi.

Mwanzoni mwa miaka ya 70(early 1970s) serikali ya mwalimu Nyerere ya wakati ule iliamua kuanzisha viwanda na ilifanikiwa chini ya waziri mkuu wa wakati ule mzee Cleopa Msuya.

hilo lilipofanyika watanzania wengi hawakuwa na tatizo la ajira na wakati ule kulikuwa na idara maalumu ya kazi kama siyo wizara. Nafasi za kazi zilikuwa zinatafuta watu kwa maana kuwa zilikuwa nyingi kukidhi watanzania wenye kuhitaji ajira. Haikuwa ajabu kwa miaka ile mtu kwenda kwenye ubao wa matangazo ya kazi na kujichagulia akafanye kazi katika kampuni ipi na ni kazi ya aina gani, tofauti na sasa ambapo watu wanatafuta kazi na wala hawana cha kuchagua aina ya kazi kwa kuwa hakuna kazi.

wakati ule watu walipokuwa na kazi usingeweza kuwaita malofa kama anavyowaita Mkapa leo watanzania kuwa ni malofa.

Mkapa alipoingia madarakani alianza kuutengeneza ulofa kwa watanzania hasa baada ya mwalimu Nyerere kufariki kwa kuwa asingeweza kufanya hayo mbele ya mwalimu.

alianza kuuza raslimali za watanzania kwa kuruhusu uuzwaji wa madini kwa bei ya kutupwa na uanzishwaji wa migodi mingi bila tija. Ilikuwa ni wakati ule ambapo mgodi wa Bulyankulu ulianzishwa kibabe na kuwaaua watanzania wasio na hatia kwa kuwafukia katika mashimo ya dhahabu wakiwa hai kama ilivyopigiwa kelele nyingi na wapinzani wakati ule akiweno Mrema.

kama haitoshi Mkapa aliamua kuuza viwanda vyetu na mashirika mbalimbali ya kiserikali yaliyokuwa yanatoa idadi kubwa ya ajira kwa watanzania ili wasiwe malofa.

mashirika hayo yaliwafuta kazi mamia kwa mamia waliokuwa wakihudumu na kufanya kazi katika viwanda na kuwaacha wakiwa hawana kazi na huo ukawa mwanzo mkubwa wa kuzalisha MALOFA wa nchi hii. Hao wafanyakazi hawakuwa peke yao, walikuwa wanafamilia zao. Familia ziliyumba, walishindwa kuzihudumia, walishindwa kusomesha watoto na kujikuta wanazalisha malofa wengi zaidi kwa kuwa ndoto ya elimu ilikufa kwa watoto wengi.

viwanda alivyovibinafisisha Mkapa vingi vilikufa kabisa baadae na hivyo kutozalisha ajira hata moja, hata wale wachache waliobakizwa kufanya kazi katika viwanda vile nao walipoteza kazi na kugeuka MALOFA ikiwa ni pamoja na familia zao.


Rais anayeondoka sasa Mhe Jakaya Kikwete alipokuwa anaingia alituahidi neema ya ajira millioni mbili, maana yake alikuwa anataka kuufuta ULOFA wa watanzania uliosababishwa kwa kiasi kikubwa na Mzee Mkapa. Cha ajabu Kikwete naye akaunda serikali ya kuliibia zaidi taifa kuliko awamu nyingine yoyote katika historia ya nchi hii.

kibaya zaidi ni kwamba wakati huu serikali ilikuwa haizalishi tofauti na wakati ule ambapo serikali ilikuwa inazalisha kupitia viwanda vyake vilivyokuja kuuzwa na Mkapa. Wakati huu pato la serikali lilikuwa ni Kodi toka kwa wananchi. Kodi hiyohiyo ikawa inaibiwa kupitia kashifa nyingi ndogondogo za ufisadi na kashifa/skendo kubwa kubwa za ufisadi na mafisadi kulindwa.

badala ya kuwasaidia malofa wapate kazi ili wasiwe malofa serikali ya Kikwete ikawa inaiba mpaka hela ya serikali ambayo ndani yake imo pia kodi ya hao malofa kwa kuwa wanalipa kodi kupitia bidhaa mbalimbali wanazonunua na kutumia.

LEO MKAPA ANAKUJA MBELE YA WATANZANIA NA KUTUDHIHAKI SISI MALOFA AMBAO ULOFA WETU UMETOKANA NA CCM NA YEYE MWENYEWE AKIWA MSHIRIKI MKUBWA KUFANIKISHA HILI.

naamini hata watanzania wasio malofa hawapendi watanzania wenzao wawe malofa ama waendelee kuwa malofa, naamini watanzania wote wasio malofa wana ndugu zao ambao ni malofa na hawapendi ndugu zao waendelee kuwa malofa kwa maana ya kukosa kazi na kitu(mali).

CCM kupitia viongozi wake imeonyesha dharau kubwa mbele ya Watanzania wote.

lazima kama taifa tuungane pamoja kuiondoa CCM iliyojaa jeuri, kiburi,majivuno na ukosefu wa hekima kwa wananchi wake, viongozi haohao wa serikali akiwemo mkapa na kikwete na magufuli ambaye ni mgombea walipewa dhamana ya kuiongoza nchi hii na hao malofa kupitia kura zao. marais wote waliotangulia walipigiwa kura na malofa , wabunge na mawaziri wote waliotangulia na wanaomaliza muda wao nao hawakuingia uongozini bila kura za watanzania malofa.


natoa rai kwa watanzania wote wale malofa na wasio malofa kwa kuwa hakuna anayependa ulofa wala jirani yake ama ndugu yake awe lofa kwa pamoja tukomeshe dharau hii ya watawala kwa kuikataa CCM yenye jeuri na kila aina ya dharau kwa watanzania.

JOSEPH MSHINGA
Lofa mwenzenu na ndugu yenu kwa wasio malofa.
 
wengi hawajui kuwa kuwa mpumbavu sio tusi, ni neno lenye maudhi tu, kama vile kuwa -----. saying that Mkapa hakutakiwa kulisema kwa ukali vile!dah, jamaa yule ukali hadi anazeeka nao.ndio maana waandishi uchwara wa bongo walikuwa wanamuogopa kuliko.
Mwalimu Nyerere alitumia neno hili bila shida. Vipi na Sugu Bungeni.
Queen Esther
 
kweli nyinyi ni malofa na wapumbavu hamuelewi hata mueleweshe vipi. Sumaye hajasema anakuja komboa amekuja kuwasaidia kuongoza sababu hamjui.....wapumbavu ni nyinyi

Ndio upana wa mtazamo wako ulipoishia?
 
Mbona mnapotosha maana halisi nyie watu' Mheshimiwa mkapa amesema' Nanukuu' Kuna watu wanajifanya leo hii wanataka kuwakomboa watanzania wakati watanzania walishakombolewatangu enzi za Tanu na Asp kutoka kwa wakoloni watu hao Wanaojifanya Wanataka Kuwakomboa Watanzania Ni WAPUMBAVU" Eti mnasema Mkapa kawatukana watanzania Acheni Uongo Tusi Lenu Lile Ukawa, Kwani nani asiyejua sera za ukawa ni kuwakomboa watanzania kutoka kwenye Umasikini' wkt wenyewe hata hawafanani na wanachokisema Nyuso zao wote zimejaa uchu wa madaraka kila mmoja, Hivi Niwaulize! Nyie mliotoka ccm' Hivi Kweli Mlikuwa Na Nia Hii Ya Kutukomboa Watanzania Na Kuleta Mabadiliko Toka Kitambo..? Au Idea Hii Imekuja Pale Tu Alipokatwa Jina Baba Yenu Lowasa..? Kama Toka Kitambo Basi Mngetoka Nae Mapema Wala Msingesubiri Ccm Imkate Jina, Na Kama Baada Ya Kukatwa Jina Basi Dhahiri Kwamba Nyinyi Mna Uchu Wa Madaraka Kama Sio Ubinafsi, Kwani Nyinyi Mbona Hamfiki Hata Theruthi Ya Wana Ccm Wote Na Wala Hamstahili Kuongozi Umma Wa Watanzania Wote.
 

Kwasasa mshapoteza hadhi yakumkashifu yeyote ndani ya CCM,tena ni vema mkaweka akiba ya maneno kwani hamuwezi jua 2020 kitatokea nini,mlimwita Lowasa fisadi leo mmemkabidhi bendera,sasa naona mnataka kurudia kosa lilelile,ni bora mkae kimya mshazoea vyakunyonga.
Mtaanza kumkashifu mzee Mkapa halafu kesho mtageuza maneno
 

Umeongea kama unakula mahindi.ya kukaanga ya msimu ulioisha!
Toroka uje,"Lowasa Rais,hata mimi nilikuwa huko"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…