Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Miaka iliyopita hata kwenye vikao vya Bunge ilishazoeleka na kuaminika kuwa wenye uwezo wa kutoa maneno ya kuudhi na kuvunja heshima za watu ni wapinzani, hii ni kutokana na ukweli kuwa nguvu ya mtu anayeelekea kushindwa au kuungwa mkono ni kilio au matusi.Nilishangaa sana katika uzinduzi wa ccm kuona watu ambao tulidhani kwa sasa ndiyo ingalau wanaheshimika kuona ndiyo vinara wa kuporomosha matusi bila haya wala aibu.

Kitendo cha Rais wa awamu ya tatu Mzee Mkapa kutamka aina ile ya maneno nafikiri haikuwa sahihi pia sidhani kuwa hata mgombea mwenyewe anaweza kutamka maneno yale, ni dhahili kuwa "ukifiwa sharti jicho lako mfiwa liwe jekundu" Maneno hayo yalipaswa kama ni lazma yasemwe na watu kama wakina Nape ambao ingalau ndiyo wamiliki wa chama iweje leo mtu ambaye alijijengea heshma katika uongozi wake aamuue kuwaharibia wenzake?

Mzee mkapa wakati wa uongozi wake alishawahi kutamka maneno ya kuudhi kuwa "waandishi wa habari wa tanzania ni uchwara" kauli ambayo ilimsumbua sana, ninachotaka kushauri CCM ni kuwa "Mwanamke halazimishwi kuolewa na ikitokea kumuoa kwa lazima inaweza ikawa umeoa msaliti, kun'gang'ania watu waliowachoka ni kupoteza muda, pia hicho ndiyo kilichowafikisha hapo mlipo pigeni kampeni za kistaarabu, watanzania waliowengi wanafahamu mlichokifanya katika uongozi wenu, rekodi yenu ndiyo itawaingiza au kuwatoa Ikulu, kama mmewatumikia wananchi vizuri hamna haja ya kutumia matusi na kuwaponda wasio kubaliana nanyi lamsingi pigeni kampeni za kistaarabu mwisho wa siku tarehe 25 oktoba kila mtu akafahamishwe mamuzi ya wananchi.
 
CCM: Kampeni za Matusi sio sahihi rikodi yenu ndiyo itawaingiza au kuwatoa Ikulu!
Sasa hapo ulikuwa unaiambia CCM kwamba matusi sio sahihi au ulikuwa unainukuu CCM kwamba imesema matusi sio sahihi? Tujifunze uandishi wa titles jamani!
 
Sasa hapo ulikuwa unaiambia CCM kwamba matusi sio sahihi au ulikuwa unainukuu CCM kwamba imesema matusi sio sahihi? Tujifunze uandishi wa titles jamani!
Tunaoandika humu wengi sio waandishi wa habari kitaaluma ukitaka weledi kasome magazeti ambayo yanamipaka ya uandishi nilitaka nikutusi ila ngoja tu nikuache nisije nikajiunga na hao niliowataja
 
Anold kwenye bunge nakumbuka sana watoaji wa mtusi na vijembe walikuwa wabunge wa chama kikuu Tawala.Tuliwasikia akina Lusinde,Mwigulu,aliyekuwa Naibu waziri wa magazeti, na Spika alipeta tu.Sishangai huku uraini mabosi wao wakitukana ni hulka walijijengea.
 
Hao wanao ng'ang'ania kuingia ikulu kwa mabavu wana record gani!? Sshv wana leta unafiki wa kuzurula kama mbwa koko
 
CCM na hasa Magufuli ni bora angetumia muda wake mwingi kuwaomba wananchi msamaha kwa mabaya yote yaliyosababishwa na CCM kupitia kwa serikali zake zote za awali...

Eti utamkuta mgombea huyu wa CCM naye anadiriki kuungana na wananchi kulalamikia hali duni za huduma mbali mbali za kijamii.... utafikiri hajui nani yupo nyuma ya yote hayo...??

Kama si dharau ni nini basi....??? Alafu kuna watu wengi wanampigia makofi, vifijo na vigelegele... KWELI..??
 
Mkapa amejishushia thamani pia Ccm yake ameishushia thamani arudi pale alipotolea matamko machafu kuwaomba radhi Watanzania vinginevyo Ccm tayari ipo mahabusu .
 
QUOTE=Domy;13749200]Mpumbavu na Lofa ni yule aliyeuza Benki kwa bei ya kutupa!
attachment.php

Paul Alex huyo ndiye mbabe Mkapa aliyeweza kukaa na Sumaye kama Waziri Mkuu kwa miaka 10
na enzi hizo Wapinzani (Mrema na NCCR) bila ya kufurukuta licha ya MEDIA nayo kutukanwa kubanwa
leo mnashangaa matusi
HIVI ANGERUDI sijui UKAWA wangeenda wapi?[/QUOTE]

Sasa wakati umefika,kila wanachosema na kufanya kinawarudia.Ni kama mchawi akifikia mwisho huwa anasema yote aliyoyafanya na kuishia kichanganyikiwa!
 
View attachment 280079
Nakuongezea na wewe acha upumbavvu maana una ugonjwa wa kusahau mpumbavu mkubwa tena uwe na heshima kwa viongozi wako inaonekana wewe hata wazazi wako umewashinda

CCM mmekuwaje,mmeingia msimu wa matusi nini?
Kila mtu anatukana,hata bila sababu.
Mungu akusamehe ndugu,pole kwa jazba na karibu ukawa.
 
Tunaimani na magufuli katika uchapakazi,uadilifu na ufuatiliaji.......tumchague magufuli hao wengine wanamatatizo mengi katika ufanyaji kazi wao,

Magufuli ni menager mzuri,lakini tulipofika tunataka kiongozi,Tunamtaka Lowasa
 
Kumbe hata wewe ni mpumbafu! Unaandika ujinga tu. ---- wewe

Mungu Baba,Mwana na Roho mtakatifu akusamehe dhambi zako.Namwamuru pepo wa matusi aliyewaingia CCM atoke.Akutoke,pepo tokaaaaa!
Sasa karibu Ukawa!
 
Wana JF wengi ni wapotoshaji. Mkapa kazungumzia viongozi anaowajua wapi amesema watanzania wapumbavu. Vile vile hamjui fasihi kila kitu mnakichukulia kilivyo.. Kiongozi mmoja aliwahi kusema " I cannot let my Country to the Dogs" Jamaa wakasema katuita mbwa. Tuzungumze hoja na bahati mbaya mmeenda kuizungumzia kwa waswahili ambao wameshaona maneno yale yana ukweli. Hivi Petro (with due respect) alipomkana Masiha wakati siku zote walikuwa naye tukiiteje kitendo hicho kwa lugha nyepesi? Mungu atubariki tuvuke salama
 
Nitulie kwasababu gani?
Halafu wewe kuna kitu unanitafuta na sijui ni nini?
Sema tu usiogope!
Ila karibu Ukawa
Nikutafute wewe utanisaidia nini maishani mwangu? Umekuwa Mungu! Mimi siyo nyumbu kwa taarifa yako!
 
Mzee hajazisoma nyakati.Tangu aachie ngazi ni miaka kumi,kwa hiyo mtoto wa kipindi hicho mwenye miaka minane alikuwa hajui lolote kuhusu yeye lakini mtoto huyo ndio mpiga kura wa leo.Anadhani kuwa idadi kubwa ya wapiga kura ni walewale walioridhika na maisha ya chakula bei chee huku nchi ikiwekwa rehani.Ukali wake unawalenga wachache waliokuwa na ufahamu enzi zake lakini kundi kubwa la wapiga kura halimjui zaidi ya kusikia hadithi zake za chakula bei chee.Kizazi kipya wengi wanamshangaa kwa sababu wengi wasingeshangaa endapo kauli hizo angetoa JK mtu wa wakati wao na si huyo wa kuhadithiwa..
 
mkapa katutukana si wapinzani tu ila watanzania wote kwa sababu kama ccm walituibia ukianza na meremeta, epa, kiwira, twiga wetu, tembo, migodini rada n.k kote huko hakuna mwizi aliyeshughulikiwa na bado ikashinda 2005, 2010 watanzania wakasema mko safi muendelee kutuongoza kwa nini tusiwe malofa na wapumbavu mkapa kamaliza mzee wa uwaz na ukweli kazi kwetu. habar ndio hiyo
 
mkapa katutukana si wapinzani tu ila watanzania wote kwa sababu kama ccm walituibia ukianza na meremeta, epa, kiwira, twiga wetu, tembo, migodini rada n.k kote huko hakuna mwizi aliyeshughulikiwa na bado ikashinda 2005, 2010 watanzania wakasema mko safi muendelee kutuongoza kwa nini tusiwe malofa na wapumbavu mkapa kamaliza mzee wa uwaz na ukweli kazi kwetu. habar ndio hiyo

Nenda jaribu kumwambia baba yako kuwa wewe ni lofa pumbavu.

swissme
 
Back
Top Bottom