Miaka iliyopita hata kwenye vikao vya Bunge ilishazoeleka na kuaminika kuwa wenye uwezo wa kutoa maneno ya kuudhi na kuvunja heshima za watu ni wapinzani, hii ni kutokana na ukweli kuwa nguvu ya mtu anayeelekea kushindwa au kuungwa mkono ni kilio au matusi.Nilishangaa sana katika uzinduzi wa ccm kuona watu ambao tulidhani kwa sasa ndiyo ingalau wanaheshimika kuona ndiyo vinara wa kuporomosha matusi bila haya wala aibu.
Kitendo cha Rais wa awamu ya tatu Mzee Mkapa kutamka aina ile ya maneno nafikiri haikuwa sahihi pia sidhani kuwa hata mgombea mwenyewe anaweza kutamka maneno yale, ni dhahili kuwa "ukifiwa sharti jicho lako mfiwa liwe jekundu" Maneno hayo yalipaswa kama ni lazma yasemwe na watu kama wakina Nape ambao ingalau ndiyo wamiliki wa chama iweje leo mtu ambaye alijijengea heshma katika uongozi wake aamuue kuwaharibia wenzake?
Mzee mkapa wakati wa uongozi wake alishawahi kutamka maneno ya kuudhi kuwa "waandishi wa habari wa tanzania ni uchwara" kauli ambayo ilimsumbua sana, ninachotaka kushauri CCM ni kuwa "Mwanamke halazimishwi kuolewa na ikitokea kumuoa kwa lazima inaweza ikawa umeoa msaliti, kun'gang'ania watu waliowachoka ni kupoteza muda, pia hicho ndiyo kilichowafikisha hapo mlipo pigeni kampeni za kistaarabu, watanzania waliowengi wanafahamu mlichokifanya katika uongozi wenu, rekodi yenu ndiyo itawaingiza au kuwatoa Ikulu, kama mmewatumikia wananchi vizuri hamna haja ya kutumia matusi na kuwaponda wasio kubaliana nanyi lamsingi pigeni kampeni za kistaarabu mwisho wa siku tarehe 25 oktoba kila mtu akafahamishwe mamuzi ya wananchi.