Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Huyo baba labda alijaribu kuishi kizungu ila mambo yaende. Si ajabu ukienda kwake bila taarifa unakarishwa sebuleni na wanaendelea kula. Hudhuria mazishi unapopata nafasi, sio ili watu wakuone.
Sio kuishi Kizungu, hakuwa mnafiki, Misibani watu hawaendi kuomboleza bali unafiki ili waonekane na wao walikuwepo
 
Haya mambo ya misiba tunapokwenda ni kubaya uswazi tunaishi na watu wenye Roho mbaya usisafiri misiba miwili ikakupita utaambiwa hautokagi misibani watasahau kama ulishawahi kuchimba kaburi la mzazi wao miaka mitatu iliyopita
kwani lengo la kwenda msibani ni lipi? inaeonekana Bongo mna malengo tofauti
 
Kuna wakati jamii inakuwa bore kuliko pesa zako,hapo sasa watakao waza kususiwa msiba ni wale waliopo hai,kwa fursa hizi,inabidi nianzishe kikundi cha kulia msibani
 
Ukiona hivyo hapo hakuna waislam wa kweli muislam wa kweli ambaye mcha Mungu Hana muda wa malipizi ya aina hiyo huamini katika stahiki nne za marehemu kuoshwa,kuvikwa sanda,kusaliwa na kuzikwa kinyume chake waliopo hapo ni waislam wa majina
Mkuu mbona ujaweka kukamuliwa mavi?

Nyau de adriz
 
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli za kutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka Jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu.

Bahati mbaya hata watoto wake mke pia walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.

Hii stori inakuja kufanana kidogo sana na hii yangu ambayo niliishugudia.

Hii imenikumbusha mwaka 2019 nilihudhuria msiba wa babu huko Musoma kijijini cha Nyabange Wilaya ya Butiama. Nzengo walikuja kama kawaida wakashughulika kila kitu wakaandaa, lilipofika suala la kula kile chakula wakaitana baadae nikaona kila mtu anaenda kwake, kila kitu walicho andaa walikiacha kama kilivyo tukabakia ndugu tu.

Wakasema, mjomba ambae ndio msiba ulikuwa umepangwa hakuwa anakula kwenye misiba na yeye alikuwa anachangia tu. Na mke wake alikuwa anakuja kupika na kuondoka kula hawali wala hawakai kwenye msiba wa nzengo. Waligoma kabisa, sasa chakula walichokuwa wameandaa nikama sisi ndugu tusingekimaliza hata kama tungekula siku 2 bado kingebaki kingi tu. Ikabidi ndugu waitane na wakaongee na wazee mjomba akapigwa faini ya mbuzi ndio wakaja kushiriki.

Toka hapo mjomba hajawahi kuacha kuhudhuria misiba anakwambia nilichokiona sikuile ni fedheha hata kama unauwezo ile ni mbaya sana.
Mnamwadhibu huyo mzee au familia yake?
 
Umeleta hoja nzuri kwangu. Hivi, mtu akifa wananzengo wakaja wakajaa kama mia tano au elfu hivi hadi msiba ukaisha. Kuna faida gani?

Na mtu akifa, wananzengo wasije bali wakaja ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na marehemu na ndugu wa marehemu kama kumi tu hadi msiba ukaisha, hasara yake ni ipi?
 
Temea chini nuksi hiyo isikuvae.

Kama una makandokando ya kutohudhuria misiba ya kwenye nzengo unayoishi, jitahidi ndugu nenda, siku hiyo ua shughuli zako.

Jamii inayokuzunguka ndiyo wanaokupima nyendo na tabia zako.

Hapa siyo Ulaya utasema kuna vikundi vya mazishi na wafariji wa kukodi.

Ukiona jamii inakutenga siku ya msiba wako, cha kufanya kuwa mpole, usilete ujuaji ama ngebe zako kabisa.

Hapo huwa imelengwa faini ya kujikosha na kurejeshwa kundini.

Kwa hiyo faini itakayoamriwa ndugu watakuchangia na ikishatolewa, watu wataendelea kushirikiana na wewe kama kawaida.

Mi niliona hayo kwa ndugu yangu, ilibidi wanandugu tuchangishane kununua huyo ng'ombe aliotozwa na nzengo katikati ya msiba, watu wamegoma kuzika mpaka ng'ombe alipotoka ndiyohali ya hewa ikarejea kawaida.

Mambo ya kijamii ni marahisi pia ni magumu sana usiombee yakukute mr.
Hatari sii mchezo watu wanataka kula nyama
 
Ndio maana kuna kampuni za kuzika, huu ujinga utaisha one day, kwamba kazima uhudhurie misiba hata kama alie kufa hamjuani

Na waombolezaji hata ukiwambia walie machozi wanalia ilimradi uwape Hela yao mloelewana.
Kuomba siku hizi unakodi mziki hata ukitaka ukeshe au kama una spika yako unaweka flash muda wote mapambio kama yote.
Kuliko kujaza Wa hila wasio na Mungu moyoni
 
Yani kutohudhuria msibani ni adhabu? Wamatumbi mnasafari ndefu sana.

Misiba inajaza na inakaa muda mrefu sababu watu wengi hawana shughuli za msingi za kufanya. Itafika hatua watu wataenda misibani kwa invitation.
 
Heka heka hizi huwa zipo huku tu kwetu Africa hususa Tanzania. Mbona nchi za wenzetu ni kawaida kabisa. Yaani mazikoni mnakuaa wachache tu na kampuni ndio inahusika na maziko.
 
Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli za kutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.

Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka Jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu.

Bahati mbaya hata watoto wake mke pia walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.

Hii stori inakuja kufanana kidogo sana na hii yangu ambayo niliishugudia.

Hii imenikumbusha mwaka 2019 nilihudhuria msiba wa babu huko Musoma kijijini cha Nyabange Wilaya ya Butiama. Nzengo walikuja kama kawaida wakashughulika kila kitu wakaandaa, lilipofika suala la kula kile chakula wakaitana baadae nikaona kila mtu anaenda kwake, kila kitu walicho andaa walikiacha kama kilivyo tukabakia ndugu tu.

Wakasema, mjomba ambae ndio msiba ulikuwa umepangwa hakuwa anakula kwenye misiba na yeye alikuwa anachangia tu. Na mke wake alikuwa anakuja kupika na kuondoka kula hawali wala hawakai kwenye msiba wa nzengo. Waligoma kabisa, sasa chakula walichokuwa wameandaa nikama sisi ndugu tusingekimaliza hata kama tungekula siku 2 bado kingebaki kingi tu. Ikabidi ndugu waitane na wakaongee na wazee mjomba akapigwa faini ya mbuzi ndio wakaja kushiriki.

Toka hapo mjomba hajawahi kuacha kuhudhuria misiba anakwambia nilichokiona sikuile ni fedheha hata kama unauwezo ile ni mbaya sana.
Shida sio Mzee ila mke na watt ndo wapuuzi
WLiiga tabia ya kipuuzi
Mke hakukaa kwenye nafasi yake ku cover huo udhaifu wa mume
Hivi vitu vipo Kuna watu wameubwa hivyo
 
Hapo shida ni pesa tu wala sio kuhudhuria misiba.

Hapo ingekua ng'ombe 1 ama 2 wako chini, michele ya kufa mtu msiba ungejaa watu na mazishi yangeenda poa tu.

Ukiwa masikini ukafa ndio unaletewa masharti ya kipumbavu kama hayo mara ulikua huhudhurii misiba, mara ulikua huchangii jumuia na ujinga mwingine ila ukiwa na pesa hata mbwa wako akifa askofu ama shehe anakuja kumuombea aende mbinguni.
😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom