Mzee mmoja amefariki na M/Mungu alimjaalia kweli enzi za uhai wake mali kweli kweli za kutosha, katika kujumuika na nzengo Mzee hakuwa na historia ya kuhudhuria misiba ya wengine na hata kushiriki tu hakuwa anafanya hivyo enzi za uhai wake kabisa na hakuwa anajali.
Sasa ya Mungu mengi bwana leo yeye ndio amefariki toka Jumatatu. Nyumbani kwake pamewekwa maturubai na ratiba ya mazishi ila hakuna watu.
Bahati mbaya hata watoto wake mke pia walimuiga tabia. Wapo wenyewe na ndugu majirani hakuna hata mmoja na watu hawana habari napo ni kama vile hakuna kitu vinaendelea pale kila mtu anaendelea na mambo yake.
Hii stori inakuja kufanana kidogo sana na hii yangu ambayo niliishugudia.
Hii imenikumbusha mwaka 2019 nilihudhuria msiba wa babu huko Musoma kijijini cha Nyabange Wilaya ya Butiama. Nzengo walikuja kama kawaida wakashughulika kila kitu wakaandaa, lilipofika suala la kula kile chakula wakaitana baadae nikaona kila mtu anaenda kwake, kila kitu walicho andaa walikiacha kama kilivyo tukabakia ndugu tu.
Wakasema, mjomba ambae ndio msiba ulikuwa umepangwa hakuwa anakula kwenye misiba na yeye alikuwa anachangia tu. Na mke wake alikuwa anakuja kupika na kuondoka kula hawali wala hawakai kwenye msiba wa nzengo. Waligoma kabisa, sasa chakula walichokuwa wameandaa nikama sisi ndugu tusingekimaliza hata kama tungekula siku 2 bado kingebaki kingi tu. Ikabidi ndugu waitane na wakaongee na wazee mjomba akapigwa faini ya mbuzi ndio wakaja kushiriki.
Toka hapo mjomba hajawahi kuacha kuhudhuria misiba anakwambia nilichokiona sikuile ni fedheha hata kama unauwezo ile ni mbaya sana.