Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Mtu mzima kwenda misibani mpaka upigwe faini, kweli umri ni namba tu
 
Sasa mkuu mandala hapo huwa nawazaga sana Mie siend kwenye misiba, siend sherehe yoyote kwenye imani yangu sehemu ya ibada daftari la mahudhurio sipo, sitembeleagi ndugu wala kuwasiliana naoπŸ€”

S ndo kwangu watahudhuria mtu NNEπŸ˜…
Huoni kwamba utakua umepunguza gharama kubwa, viti, chakula vinywaji , usafiri, Kisha ukabaki na madeni, ukawa una misiba miwili?
 
KWANI WASIPOENDA MSIBANI KUNA SHIDA?
UMASKINI KITU MBAYA SANA.
 
Siyo kila watu ni wa kuingiliana nao. Wengine ni nuksi. Ndiyo maana Wengine wanasema wema hawana maisha, pengine ni ile hali ya kuishi bila limit. Kila mtu anajichanganya naye. Kumbe anajimaliza
sahihi mkuu.
 
Ila jamani waswahili sie tuna nongwa, tusilipe ubaya kwa ubaya, labda kama mna ugomvi personal bila bora tuu kwenda ukajumuike na wafiwa.
 
Tatizo liko wapi?
 
Mtu ajitwishe jeneza wakazike hata wakija maelf harudi tena.
 
Kwa waislam kama ulikuwa mzinzi,mlevi,muasherati,huhudhurii misiba siku ukifa utazikwa tu mambo mengine it is up to you kujibu kwa mola wako huko juu.
 
Misiba kama hiyo naipenda sana.

Ni kama misiba ya wazungu majuu.

Familia mnaumaliza msiba fasta bila usumbufu na gharama za kulisha watu
Yani watu huja kula na kuangalia nani kaja nani hajaja....pumbavu sana.
 
Kashakufa ata msipo enda hadhuriki kwa chochote
Kwanza nyie ni mapimbi mnamsimanga marehemu yan mnaleta ugomvi na mfu

Kashakufa mkienda msipoenda haisaidii wala hapati aibu tyr ni marehemu

Watu weng kuja msiban ni sifa kwa ndg na jamaa walioko hai ila kwa mfu haina maana yyte
 
Hii tabia siipendi jamani yaan wanajamii huwa wapo macho sana kuangalia nani anakosea ili wamkomoe siku moja siwapendi kabisa ,watu kujaa na kusubiri kula ,sisi kwetu huwakomesha nzengo wanakuja tunawapa kazi ya kukatakata vitu kupika tunaweka mtu anapika na kusimamia kila kitu sasa wanachukia kwa sababu hawawezi kuiba wale wanawake ni wezi mno wa nyama sijui wapoje,msiba wa babu yangu watu wanakuja muda wa kula mpaka tukawatangazia jamani msiba umeisha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ watu wanapenda vyakula vya msiban hasa penye vinono
 
Waje wabadili msiba uwe kwa ndugu na jamaa wa karibu
 
Ningewapa kongole kama wangesusa hadi kupika. Walijua tu kuna kitu kitafanyika wakale minyama. mshua mmoja aliishi sana Ulaya, akarudi Dar akafiwa na mzazi. Hakuzoea misongamano. Waswazi wakapika tena menu yenye kuku pia, wakasepa, wanasubiri kuombwa radhi ili warudi kula. Shubuuutuuu. Mfiwa Alikodi gari likafuata masela manzese wakala ubwabwa fresh, wacha wapishi wa uswazi walalamike.
 
Wanawatahadharisha kabisa watoto wao wasicheze mbali maana kwao hakupikwi siku hiyo. Ushamba huu sijui utaisha lini. kijana mmoja alibeba na ndizi mbivu kabisa, anasema eti akila pilau kavu choo kinakuwa kigumu. Oh Lord.
 
Wanawatahadharisha kabisa watoto wao wasicheze mbali maana kwao hakupikwi siku hiyo. Ushamba huu sijui utaisha lini. kijana mmoja alibeba na ndizi mbivu kabisa, anasema eti akila pilau kavu choo kinakuwa kigumu. Oh Lord.
Familia nyingi njaa kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…