Mzee mmoja alikuwa haudhurii misiba leo kafariki, kinachoendelea hapa naona ni msiba wa familia tu

Kama waliopo wanatosha kumzika hakuna tatizo hapo.
 
Me mwenyew nikifa staki shobo.Umasikini wa kiafrika mnahisi mkirundukina au msiba ukiwa na watu wengi basi kuna maana au ni ufahari.

Kampuni kibao zinashughulikia mazishi sasa nyie walalahoi msio na hela ndio mpambanie watu wa kuwazika.

📌Na mkiona tabu pelekeni maiti msikitini itazikwa huko hawana ubaguzi wa kijinga.

📌Mtu akishakufa biashara imeishia hapo haijalishi atazikwa na mtu mmoja au maelfu ya watu.🤝
 
Ila ni sawa tu maana wasioenda wamewapunguzia gharama wafiwa. Kama familia inajiweza kiasi hapo ni kununua tu jeneza, wakodi watu wachache wa kusaidia kuzika makaburini, siku imeisha.
Huwa tunacomplicate sana misiba
Yes kabisa, sikuhizi kuna funeral services, watatafuta na watu wa kuwalipa hata wasiopungua 10, wanamaliza bila stress ya masufuria ya ubwabwa jikoni
 
Mnajazana msibani kufanya nini?
 
Msiba mzuri kabisa huo. Sio kwenda kuweka kiwingu misiba ya watu. By the way siku hizi kuna huduma za kukodi mazishini. Kwa hiyo nyie vinyangarika piteni mbali. Msisogee hata kula wali kwenye bufee kumbaf
 
Hana maumivu yoyote hapo alipo; wala hisia; wala haoni; wala hasikii! "Kumkomoa" hakuna maana yoyote unless kama watoto au ndugu zake nao walikuwa na tabia kama yake wanafundishwa namna ya kuishi na watu kupitia kifo cha mzee wao. Ila kama kwa ajili ya marehemu hao wanaofanya hivyo ni wajinga.
 
Kutumia fedha nyingi kwenye msiba na watu wengi ni kuendeleza umasikini. Baada ya msiba familia inakosa mahitaji muhimu kama ya afya na elimu. Wanaanza kulaumu Trump na wengine wanaoelekeza kubana matumizi.
 
Mwisho wa siku atazikwa tu.
Ila ni vizuri kujihusisha na mambo ya kijamii mara moja moja. Tupunguze nyodo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…