Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Katika mada zako nyingi za historia ya taifa hili hua nikiangaliama Context naona mada zako zote zinalia kwa uchungu huku zikitoa ujumbe kua Waislamu tunaonewa, nikimaanisha kwamba mada zako karibu zote hua zina chembe chembe za Udini.
Nimesoma mara tatu huu uzi wako nikawa najishauri nikujibu au nisikujibu au nijibu kwa namna gani,lakini nafsi ikasita,nikajisemea nina kitu cha kusema hapa kisha nitatoa msimamo wangu mwishoni.

Kwamba je haya anayoyasema ni ya uongo au sababu yeye ameeleza yale ambayo hatukuyasikia au hatukupenda kuyasikia ? Nafsi ina maajabu yake sana.

Hivi mathalani mimi nikitetea haki yangu na kueleza sababu ya kukosa haki yangu ni dini yangu,nitakuwa mdini ?

Je haya anayoyasimulia mzee wetu ushawahi kujiuliza kwanini hayakusomeshwa vitabuni mwetu ? Je walifanya makusudi au kwa bahati mbaya ? Kama walifanya kwa bahati mbaya kwanini waliandika Historia bila kuchunga misingi ya kuandika Historia ?

Kila elimu ina takiwa ifate misingi 10,narudia tena kila elimu inatakiwa ifate misingi 10,ukiikosa misingi hiyo kaa ukijua hutaipata elimu hiyo. Misingi hiyo sitaitaja kwa sasa,kama ikibidi huko mbeleni nitaitaja. Maneno haya aliyasema mwanachuoni mkubwa Ali Swabaani.
Kila fani ya kielimu ina namna yake ya ukosoaji ila kwenye asili ndiko majambo hurudishwa.

Leo hii wewe ukitaka kuikosoa historia ambayo aliiandika mtu fulani basi na wewe rudi kule kule kwa wenye Historia yao kisha uikosoe ili ambayo iko dhidi.

Pia,kuna maneno ya uongo unayasema na haya bila shaka umeandika kwa chuki pia hali ya kuwa unataka kujaribu kuamisha ya kuwa huna chuki,ya kwamba muarabu ana dini,Muarabu hana dini,sababu kwa waarabu kuna wapagani,washirikina na wasio kuwa hao. Hili umelisema lakini ukiombwa ushahidi naamini hata ukipewa miaka mia hutaweza kuthibitisha ya kuwa Uislamu wa waarabu. Kwahiyo unatakiwa ukiandika uandike kwa haki.

Mathalani mnaposema Historia aliyoiandika mzee wetu ina Udini,basi mlitakiwa kuonyesha au kuandika Historia ya kweli ambayo inaonyesha haina Udini huku mkirejea kwa wenye Historia.
Hili na wewe linakuhusu bali hata mimi,na wale pia. Huu uzi wewe ndio umeziruhusu hisia zikuongoze ndio maana umeandika ya uongo mengi na moja wapo ni hilo la kusema Uislamu ni wa waarabu.

Hivi mfano wewe ukitaka ukiandika Ukweli labda kuhusu watu wako lakini katika ukweli huo kuna madhila na dhiki kubwa sana zilizo wakuta watu wako,ukweli huu ukitaka kuuwasilisha unauwasilishaje ? Je kwenye huzuni utaweka bashasha ?

Kwangu mimi mtu kama huyu hakupaswa kuruhusiwa kuandika makala kama zile au kwanza apewe masharti kabla ya kutuma makala zake wahakikishe ameweka na marejeo,kwani Elimu ni amana na amana huwa inarudishwa kwa watu wake,kama kweli watu wanapenda kusoma na kujifunza mambo. Tatizo kubwa la muandishi huyu ni kuwa maandiko yake hayarudishi kwenye asili yaani hana marejeo,pili mambo ya uhalisia anayasimulia kama kama habari za kubuni,mwisho wake anakuwa anapunguza au kuzidisha. Uzi huu naukumbuka na kuna nukta kadhaa nilimkosoa na kuna swali nilimuuliza lakini hakujibu,sijui kama labda huo ndio utaratibu wake au la ! Mimi namdhania kheri.

Kwanza alichokosea yeye ni jambo la kidini kulizungumza kihuni kwa kutaka kutenganisha dini na jambo lile,inaonekana huko anakochukua ambako huwa hatuonyeshi ni kuwa wtu hao hawaijui dini.

Nakumbuka nilimkosoa katika kichwa habari,katika Kiswahili hakuna sentensi "....mbele ya kadamnasi..." kuandika hivi ni kufanya makosa. Tamko "kadamnasi" limejitosheleza kwa lenyewe kwani ni muunganiko wa atamshi mawili nayo ni "kadamu" kwa maana ya mbele ya kitangulia na tamko la pili ni "nasi" kwa maana ya watu,makosa hayo ni sawa na kuandika "......mbele mbele ya watu ....." hakuna Kiswahili cha namna hii.

Angalizo anatakiwa akiwa anazungumzia mambo ya dini basi ahakikishe ana ujuzi na maarifa mapana juu mambo hayo.
Kuna mambo mengine kutokana na umaarufu wake hata kama una hila ya kwapa,huwezi kuuficha ukweli zaidi ya kujibaraguza kwenda na hatua na mirindimo husika. Hapa kuna tegemeana.

Hilo jambo mpaka umelijua wewe ujue watu wengi wamelijua,lakini kuhusu Historia hiyo ya uhuru wengi hawakuwa wakiujia Ukweli,sasa hapa ndipo utakapo jiuliza kama nilivyo gusia huko,je walifanya makusudi kuificha au walikuwa naaarifa machache juu ya uandish wa Historia na kama walikuwa na maarifa machache juu ya kuandika Historia kwanini waliiandika na kuitawanya ?
NB: Yote hayo najaaribu kukuonyesha ni jinsi gani kuna udini kwenye mada zako, lakini lengo langu sijaandika uzi huu ili tujadili udini wala dini yako ila lengo langu hasa kuandika huu uzi ni

Hu ni mtazamo wangu tu,kwangu mimi sijaona udini katika maandiko yangu,na mwisho nitatoa msimamo wangu juu ya maandiko ya mzee wetu.

Mimi nilicho kiona ni kuwa mzee wetu ametuoyesha ya kuwa kumbe kuna watu wengine hawatajwi japokuwa walicheza nafasi kubwa sana katika jambo hilo la uhuru.

Hivi kwani wewe hapo kabla hao wazee alio wazungumzia mzee wetu ulikuwa unawajua ? Kama ulikuwa huwajui kwanini ulikuwa huwajui ? Je tatizo ni lako au tatizo ni la wale walio andika Historia ?

Au jalia tukwamba hao wazee hawakutoa mchango mkubwa kihivyo je ni kwa lipi hawakutajwa ?

Je hawakustahili kutajwa na kwanini ?
Mkuu ni kweli wamechangia kiasi kikubwa kupatika uhuru hapa lakini, ukweliutabaki pale palekua ni J.K.Nyerere the Almighty ndio kaleta uhuru Tanganyika na sio hao wengine bila kuzingatia kigezo cha udini. kwanini nasema hivi?

Kawaida katika wengi lazima wawepo wawakilishi kwanini umtaje yeye Nyerere pekee kwani kule alipewa uhuru baada ya kupigana au aliupora au alipewa tu baada ya muda kufika ? Hii hata lugha inakataa kukata na kumuweka yeye pekee.
Kila mtu akizaliwa hapa duniani huja na kusudi (Purpose) aliloletwa kulitimiza, kwa mantiki hiyo Mwalimu aliletwa kwa kusudi la kuikomboa Tanganyika kutoka kwenye mikono ya
Hili sio lengo bali ni matokeo,kwani lengo la sisi kuumbwa ni kumuabudu Mola pekee,haya mengine yanayotokea ni sehemu ya maisha wala hutokuja kuulizwa kwanini hukupigania uhuru wala kwanini wewe ulipigania uhuru.

Huu ni uongo,mkubwa sana,je kusudi huwa unalijua kabla au baada ?
Hii sio hoja bali ni malalamiko,huu ni uwakilishi ambao ulikuwa na sababu.

Hapa uko sahihi kabisa lakini wale wote walio kuwa bega kwa bega na mitume tunawajua na michango yao inajulikana tangu mwanzo mpaka kiyama kinasimama na tunawaombea dua kila kukicha,je hao waliomsaidia Nyerere mbona hawatajwi,mpaka mzee wetu alipokuja kuelezea upande wa pili au wewe uliwasoma hao hapo kabla ?

Kutetea hila na uongi wa watu wa ovu kuna ujasiri na kujitoa akili.

Sasa haya ndio mahaba niue na aya yako ya mwisho imesisitiza hilo.

Sisi huwa tunasema hivi "Kitengeneze kiti chako kwanza kabla ya kukitia nakshi"
Niombe radhi kwa yoyote ambae andiko langu limemuudhi kwa namna moja au nyingine.

Ciao
- Da'Vinci

Mimi binafsi nimekupa udhuru sababu umetumia hisia sana kuliko ukweli na maarifa. Hisia zako nimekuachia mwenyewe.

MSIMAMO WANGU.

Waislamu tukiona tunakuwa wadhaifu sana na kuhisi tunaonewa basi tukae tukijua kwamba sisi ndio sababu basi lazima turudi nyuma na kujitathmini upya.

Kama kuna lolote ambalo nimekosea basi ni kwa udhaifu wangu.
 
Zurri,
Ahsante sana.

Nimesoma ndugu yangu anasema kuwa Julius Nyerere alihudhuria mkutano wa Manchester 1945 akiwa na umri wa miaka 23.

Hapana hakuhudhuria.

Kuna kitabu cha Thomas Morlon, "Nyerere The Early Years," asome kitamsaidia.

Mimi nikiandika Abdul Sykes alifanya mkutano na Jomo Kenyatta Nairobi 1950 akiwa na umri wa miaka 26 na nawawekea ushahidi wa confidential report za Special Branch kutoka Rhodes House Oxford wananitukana.
 
Waislamu wanaonewa wapi..? Mbona mwapenda kunungunika
 
Kaka chukulia jambo moja,je kama kweli waislamu wanaonewa yeye hatakiwi kusema ? Kwa maana ukweli uafiche ?

Je kama yeye ameamua kuuwasemea Waislamu kuna ubaya ?

Hasa mimi sijakuelewa hapo.
Wapi mwaonewa? Na nani? Kwanini muonewe ninyi tu?
 
Mkuu. Waweza niambia ni mambo gani mnaona ninyi mnakandamizwa..na sababu unaweza ziorodhesha?
Swali kama hili ukimuuliza mtu kama mzee Mohamed Said ni kutomtendea haki. Unaonaje kwanza ukaenda kusoma vile vitabu kikiwemo cha profess Hamza Njonzi ambacho kipo kwa kiswahili halafu ndio utakuwa na maswali haswa ya kumuuliza mzee wetu
 
Swali kama hili ukimuuliza mtu kama mzee Mohamed Said ni kutomtendea haki. Unaonaje kwanza ukaenda kusoma vile vitabu kikiwemo cha profess Hamza Njonzi ambacho kipo kwa kiswahili halafu ndio utakuwa na maswali haswa ya kumuuliza mzee wetu
Relief...
Wanaotuhumiwa wamekuwa kimya baada ya kuomba ushahidi ambao uliwekwa wazi ndani ya kitabu cha Prof. Njozi.

Akisoma kitabu hicho atajifunza mengi.

Na yeye kama ni mtu makini angejiuliza kwa nini serikali imezuia wananchi wake wasijue kilichoandikwa mle nini hofu yao?

Serikali inajua kuwa tunachosema Waislam ni kweli lakini haijapata ujasiri wa kukubali ukweli kwa kuhofia matokeo ya kukubali kuwa kumekuwa na njama ya kubagua jamii moja katika misingi ya dini.
 
na hiyo ni illa katika ilmu.

ni khiyaana katika elimu.

leo historia ya uislamu inatuambia kwaba kulitokea fitna kubwa baina ya waislmu wakauwana wenyeqe kwa wenyewe.

lakini licha ya tukio hilo baya uislamu haukuona busara kuificha historia hiyo kwa sabbu kupindisha historia ni katika mambo yanayovunja uaminifu
 
Mohamed Said,

Umeandika vizuri kabisa na nimekuelewa. Hongera sana Mohamed Said kwa kuthubutu kufanya kile unachoamini na kukisimamia. watu wa aina hiyo ni adimu sana hapa Tanzania. wengi tunapenda kuimba nyimbo za Chama na Serikali bila hata kuelewa maana yake.
 
Umeandika vizuri kabisa na nimekuelewa. Hongera sana Mohamed Said kwa kuthubutu kufanya kile unachoamini na kukisimamia. watu wa aina hiyo ni adimu sana hapa Tanzania. wengi tunapenda kuimba nyimbo za Chama na Serikali bila hata kuelewa maana yake.
Mindi,
Tunawajibu sisi kama raia kuileza serikali yetu na viongozi wake kuwa ndani ya serikali kumejengeka mfumo ambao unabagua wananchi katika misingi ya dini zao ili ifahamu na kuchukua hatua kurekebisha.
 
Shukrani Mzee Mohammed Said.
 
Mzee wangu,

Nimesoma maelezo yaliyomo kwenye link uliyonipatia lakini bado yameniacha na shauku kubwa! Vitabu ulivyoviambatisha kwenye simulizi iliyopo kwenye Blog yako nitavipatia wapi?

Ukinelekeza itatosha, nitafika Mungu akipenda.
 
Mzee wangu, Vitabu vyako Mkuki na Nyota vinapatikana?
 
Mzee wangu,

Nimesoma maelezo yaliyomo kwenye link uliyonipatia lakini bado yameniacha na shauku kubwa! Vitabu ulivyoviambatisha kwenye simulizi iliyopo kwenye Blog yako nitavipatia wapi?

Ukinelekeza itatosha, nitafika Mungu akipenda.
Hammaz,
Kitabu kipo Msikiti wa Manyema na Mtoro Ibn Hazm Bookshop bei shs: 10,000.00.
 
Safuher,
Mimi nimejiuliza sana kwa nini zilifanyika juhudi za kufuta historia ya kweli na kuweka historia ambayo haikuwa sawasawa.

Mtu wa kwanza kukutana na hali hii ya kutaka kubadili historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ilimkuta Abdul Sykes mwenyewe miaka ya mwanzo ya uhuru pale TANU yenyewe ilipotaka kuandika historia yake na Abdul na Dr. Wilbard Kleruu wakakabidhiwa kazi hii.

Yale aliyokutananayo Abdul aliamua kujitoa lakini Dr. Klerruu alikamilisha kazi ingawa kazi hiyo haikuchapwa kitabu ikabaki mswada katika maktaba ya TANU Mtaa wa Lumumba hadi ilipochukuliwa na kuchapishwa kitabu na Abubakr Olotu baada ya mswada kufanyiwa mabadiliko ya hapa na pale.

Kitabu hiki kinaitwa. ''Historia ya TANU,'' (1971) na hakina tofauti na kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni, ''Historia ya YANU 1954 -1977.(1981).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…