Mzee Mwinyi: Baba yangu alinipeleka Zanzibar ili nikajifunze dini (Q'uran) ili niwe Sheikh maarufu, nilitokea Mkuranga

Mzee Mwinyi: Baba yangu alinipeleka Zanzibar ili nikajifunze dini (Q'uran) ili niwe Sheikh maarufu, nilitokea Mkuranga

Huyo Mzee Ruksa aliimega ardhi ya Wamaasai huko Loliondo akawapatia Waarabu ulitaka WaTanganyika tumchekee.

Kitabu chake tayari kina kasoro nyingi ikiwemo eti alifungua uchumi wakati si kweli hata kidogo.

Marehemu Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine alirejesha mahusiano yetu na Kenya bidhaa mbali mbali zikaanza kuingia katika soko la Tanganyika.Waziri Mkuu Salimu A Salimu ndiye aliyefungua mpaka biashara ya mutumba chini ya uongozi wa Mwl Nyerere.

Chini ya uongozi wa Mzee Ruksa siasa za udini ziliasisiwa na vikundi vya ugaidi vilishamiri.Bado tunakumbuka uchomaji wa shule ya Shauritanga na uchomaji wa makanisa.Vita ya KKKT Dayosisi ya Meru yote yalikuwa ni matunda ya uongozi wake dhaifu hadi ukazaliwa ule mtandao wa G55.
Ilitakiwa akili makosa yake kama mkapa alivyokiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIZO STORY ZINGETOKEA leo kulikuwa na shida gani yaani ujinga huo ukasabisha hatukuoan mechi jana kweli??
 
Pia amesema kwenye kitabu chake kuwa wengine walikuwa wanamtizama kwa jicho la udini,eti KWA kuwa yeye ni Muislam basi alikuwa anateua viongoz wake kwa upendeleo wa kidini, jambo hilo lilimkwaza Sana, Galatians hawajaanza leo chuki za udini,hata mama samia kaa nao KWA tahadhari,wameshaanza na kwako pia
Umeanza tena rasmi sasa
 
Huyo Mzee Ruksa aliimega ardhi ya Wamaasai huko Loliondo akawapatia Waarabu ulitaka WaTanganyika tumchekee.

Kitabu chake tayari kina kasoro nyingi ikiwemo eti alifungua uchumi wakati si kweli hata kidogo.

Marehemu Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine alirejesha mahusiano yetu na Kenya bidhaa mbali mbali zikaanza kuingia katika soko la Tanganyika.Waziri Mkuu Salimu A Salimu ndiye aliyefungua mpaka biashara ya mutumba chini ya uongozi wa Mwl Nyerere.

Chini ya uongozi wa Mzee Ruksa siasa za udini ziliasisiwa na vikundi vya ugaidi vilishamiri.Bado tunakumbuka uchomaji wa shule ya Shauritanga na uchomaji wa makanisa.Vita ya KKKT Dayosisi ya Meru yote yalikuwa ni matunda ya uongozi wake dhaifu hadi ukazaliwa ule mtandao wa G55.

Utakuwa ni mtu mjinga tuh kutaka kufananisha uchumi enzi za Urais wa Mwinyi na Nyerere,sababu ni jambo ambalo lipo wazi Sana,

Nchi hii Nyerere aliingiza kwenye umaskin baada ya kuifanya kuwa kitovu Cha vugu vugu la ukomboz wa bara la afrika,nchi nyingi ziliweka kambi hapa na kutumia rasilimali za nchi hii katika harakat zao za ukomboz,bila ya kusahau vita vyake vya kipuuz na Alhajj Idd amin dada wa Uganda,kushindwa kwake KWA sera zake za ujamaa na kujitegemea hadi kupelekea watu kuvaa kaniki na kupanga mistar mirefu kugombania unga wa sembe na sukari,mafuta ya taa n.k

Then uje ubeze juhud za Mzee rukhsa??we nenda zako ukaendelee kuimba kwaya juma pili hii
 
Mwinyi hakuwa dhaifu ila aliongoza kipindi kigumu.

Unadhani kwanini Nyerere aliukimbia urais?

Mgalatia mwenzako ameegemea kwenye hasadi za udini tuh,hana lolote,

Anachekesha eti anapinga kuwa uchumi ulikuwa dhooful hal enz ya Nyerere hadi akaamua kukimbia na kusalim amri,

Sasa kama jambo ambalo liko wazi kama hilo anapinga,atakubali jambo gan
 
Yeye si Rais wa kwanza kushutumiwa juu ya kuteua viongizi wa upande wake. Aache kulialia na wewe kumsaidia kwa kughalagala chini!

Nyerere alishutumiwa vivyo hivyo kwamba anawapendela Wakatoliki katika uteuzi wake, wakati hata yeye alipokuwa anawateua hakujua dini za wateuliwa wake.

Amekiri hili mara nyingi na katika moja ya hotuba zake ameliongelea!

Hivyo si sawa kuonekana kwamba yeye tu ndio alishutumiwa.

Mzee mwinyi hajalia,kaandika wasifu wake,ww ndie unaona kama Analia Lia,

nyerere mchonga meno,siyo tuh alikuwa anahujumiwa,ni kweli alikuwa anafanya na had mwenyewe alikuja kukiri na kuomba radhi kuwa yeye alikuwa hajui,eti alikuwa hajui kuwa huyu Muislam au huyu mkristo na alikua haangalii dini, pathetic,,utetez huo angewambia wajinga tuh kwani hakuna vetting,na yeye hakuwa anajua kuwa nchi hii ni multi cultural society?atakuja na hoja kwamba waislam hawakuwa na shule,okay sasa iweje aanze kumtuhum mwinyi kwenye utawala wake alipoanza kuwapa nafas hao waislam wakionekana japo kwa uchache wenye shule kuweza kuhudumu katika uongoz??
 
Waislamu hatuna utaratibu wa kujiandikia kitabu cha maisha yako eti unaeleza kila kitu humo ndani, haya mambo yameanzishwa kutoka huko upande mwengine hayana umuhimu wowote wala maana yeyote.

Kitabu cha kila mtu kinajulikana kwenye maisha yako automatically wala hakuna haja kuandika, wewe ukifa watu wako wataelezea kila kitu chako ulivyokuwa na kama ulikuwa mtu maarufu ndio kabisa dunia inakutambua kwa kila kitu chako.

Mfano halisi ni Ivi ni mtanzania gani saivi hana kitabu ha mwendazake? au asiyemjua mwendazake, kila mtu ukimuuliza atajaza kurasa tele, ndio mana hakuna haja kuandika haya mambo ambayo wakati mwengine ukweli hutausema lakini watu wanaokujua watasema tu.
Naona Unabishana na Mwamadi maana na Yeye ana vitabu vingi vinavyoelezea ushujaa wake vitani na pia udhaifu wake kufia mikononi kwa mwanamke Yahud.
 
Kwa hiyo Mzee kiasili siyo Mzenji au baba yake alikuwa Mzenji aliyehamia bara?
Hakuna Mzenji yoyote mwenye jina la Mwinyi, hata ukimuona mtu ana jina hilo asili yake ni pwani ya bara. Huyu wazenji walibambikiziwa tu , kama vile marehemu mzee Jumbe ( inavosemekana hata hao wazee wa Jumbe huko Tanganyika sio kwao , wametokea Sudan ya kusini.
 
Waislamu hatuna utaratibu wa kujiandikia kitabu cha maisha yako eti unaeleza kila kitu humo ndani, haya mambo yameanzishwa kutoka huko upande mwengine hayana umuhimu wowote wala maana yeyote.

Kitabu cha kila mtu kinajulikana kwenye maisha yako automatically wala hakuna haja kuandika, wewe ukifa watu wako wataelezea kila kitu chako ulivyokuwa na kama ulikuwa mtu maarufu ndio kabisa dunia inakutambua kwa kila kitu chako.

Mfano halisi ni Ivi ni mtanzania gani saivi hana kitabu ha mwendazake? au asiyemjua mwendazake, kila mtu ukimuuliza atajaza kurasa tele, ndio mana hakuna haja kuandika haya mambo ambayo wakati mwengine ukweli hutausema lakini watu wanaokujua watasema tu.
Shaaban Robert:
Maisha yangu na Maisha yangu baada ya miaka Hamsini.
 
Back
Top Bottom