Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kuna mambo kadhaa yanahitajika kueleweka hapa.
1. Kwa katiba ya Kenya ni haki kwa mgombea aliyeshindwa kwenda kuyapinga mahakamani matokeo. Hivyo katika hilo Raila yuko sahihi kwa 100%.
2. Sio kila dosari ya uchaguzi inatosha kuufuta uchaguzi. Ukubwa wa dosari ndio unaoweza kuamua kuufuta uchaguzi ikiwa athari zake zinatosha kuathiri matokeo ya jumla ya kumpata mshindi.
3. Mahakama ina option kadhaa katika kuamua kesi hii, kwa mfano:
-Kuamuru kura zipigwe upya
-Kuamuru kura zihesabiwe upya (ama kura zote au eneo fulani tu)
-Kutupilia mbali kesi hii.
4. Baadhi ya hoja za Raila alizoziweka wazi mpaka sasa hazina mashiko kabisa, ikiwemo;
-Madai ya kusema Ruto hakufikia 50%+1 ya kura zote halali. (Wakati kiuhalisia taasisi tofauti tofauti zilizojumlisha matokeo ya kura zilizopo mtandaoni zinaonyesha kufanana na matokeo ya IEBC yaliyompa ushindi wa 50%+1 Ruto)
-Madai ya Kaunti 27 hayakutangazwa matokeo ya Urais. (Ukweli ni kuwa hesabu ya jumla ya kumtangaza mshindi ilijumuisha kaunti zote ikiwemo hizo kaunti 27 zilizokuwa za mwisho kutakiwa kutolewa matokeo yake).
Binafsi naona kesi hii huenda Raila atashindwa na ikiwa mahakama itampa ushindi Raila basi ushindo huo utakuwa wa kwenda kuhesabu upya kura (hususani kwenye maeneo machache yenye utata) au kupitia upya majumuisho ya kura ili kupata mshindi halali (kitu ambacho nadhani kitaishia kumpa tena ushindi Ruto). Kuurudia upya uchaguzi wa Kenya ni jambo gumu, zito, gharama na tata sana, sio rahisi kihivyo kwa mahakama kulifikia.