Kenya 2022 Mzee Odinga Kaamua: Kwa hizi Evidence Ruto Atapona kweli?

Kenya 2022 General Election
Kuna mambo kadhaa yanahitajika kueleweka hapa.

1. Kwa katiba ya Kenya ni haki kwa mgombea aliyeshindwa kwenda kuyapinga mahakamani matokeo. Hivyo katika hilo Raila yuko sahihi kwa 100%.

2. Sio kila dosari ya uchaguzi inatosha kuufuta uchaguzi. Ukubwa wa dosari ndio unaoweza kuamua kuufuta uchaguzi ikiwa athari zake zinatosha kuathiri matokeo ya jumla ya kumpata mshindi.

3. Mahakama ina option kadhaa katika kuamua kesi hii, kwa mfano:
-Kuamuru kura zipigwe upya
-Kuamuru kura zihesabiwe upya (ama kura zote au eneo fulani tu)
-Kutupilia mbali kesi hii.

4. Baadhi ya hoja za Raila alizoziweka wazi mpaka sasa hazina mashiko kabisa, ikiwemo;
-Madai ya kusema Ruto hakufikia 50%+1 ya kura zote halali. (Wakati kiuhalisia taasisi tofauti tofauti zilizojumlisha matokeo ya kura zilizopo mtandaoni zinaonyesha kufanana na matokeo ya IEBC yaliyompa ushindi wa 50%+1 Ruto)

-Madai ya Kaunti 27 hayakutangazwa matokeo ya Urais. (Ukweli ni kuwa hesabu ya jumla ya kumtangaza mshindi ilijumuisha kaunti zote ikiwemo hizo kaunti 27 zilizokuwa za mwisho kutakiwa kutolewa matokeo yake).

Binafsi naona kesi hii huenda Raila atashindwa na ikiwa mahakama itampa ushindi Raila basi ushindo huo utakuwa wa kwenda kuhesabu upya kura (hususani kwenye maeneo machache yenye utata) au kupitia upya majumuisho ya kura ili kupata mshindi halali (kitu ambacho nadhani kitaishia kumpa tena ushindi Ruto). Kuurudia upya uchaguzi wa Kenya ni jambo gumu, zito, gharama na tata sana, sio rahisi kihivyo kwa mahakama kulifikia.
 
Mkuu kumbuka hakutakiwi kufanyika estimate kutoka na na shariti LA 50%+1 Vote.
 
Huwa naona kama Afrika tulikurupuka au tulikuwa hatujawa tayari kuiga huu mfumo wa Kizungu wa kupiga kura ndio sababu machafuko ya uchaguzi hayaishi kila kona ya Afrka. Hai ingii akilini kwa Waafrika kuwa kiongozi mmoja kapata 50.2% na mwingine 49% halafu useme yule aliyepata 49% hana nafasi yoyote (amefeli kabisa). Naona kama mfumo wetu wa Machief wa kupendekeza bado ulikuwa unatufaa sisi waafrika
 
Swali hapa ni je hizo ambazo Team ya Raila inasema ni ndio Valid Votes je ndio valid votes?? Au zile za tume zilizompa ushindi Ruto ndio valid?
 
Naona wewe upo kihakimu hakumu zaidi kuliko waliopo field. - Sawa.
 
Nimeiona hiyo...

Wala hakuna error kubwa za kuweza kuinvalidate the whole election. Binafsi sioni Raila akishinda hii kesi kama jopo la majaji wakituliza akili.
Mkuu nimekupata barabara, ila mara nyingi tulio nje ya uwanja huwa tunaelewa zaidi kuliko walipo battle, au uongo ndg yangu!.
 
Mkuu nimekupata barabara, ila mara nyingi tulio nje ya uwanja huwa tunaelewa zaidi kuliko walipo battle, au uongo ndg yangu!.
Kutoa maoni inaruhusiwa.

Swala la usahihi au la hali husiani na kuwa kwenye battle au la.

Unaweza usiwe kwenye battle ukabakia kuwa sahihi kuliko aliyepo kwenye battle.

Maoni yangu nimeyatoa baada ya kuisoma petition ya Raila.
 
Tuwape muda wiki 2 sio nyingi
 
Naona team Ruto mmepanic
 
Vitu vingine kama hujui ni bora kuwa kimya, kwa hiyo kwa mawazo yako hata kama Raila ataifanya hiyo 49.997% ya Ruto kuwa 50% ingemfanya Ruto kutangazwa mshindi?wakati katiba ina taka mshindi lazima apate 50%+1?
La pili inshu sio hayo matokeo ya county 27 ynaweza kuathiri vipi matokeo ya jumla ya kura, au hayawezi, sheria inasemaje kuwa matokeo yote lazima yajumlishwe na ndipo mshindi atangazwe!!cha msingi ni kusubilia kuona kweli hayo wanayosema anaushahidi nayo ya kuweza kuithibitishia mahakama?!!
 
Huyu mzee uchaguzi kila sikua analalamika tu, akubali kuwa uraisi sio zali kwake
 
... ni ya kisiasa hakuna content ya maana.
☝🏾Bado nakuelewa sana, ila unaposema hakuna content ya maana bado huwezi kulingana na waliopo field mkuu .
Kutoa maoni inaruhusiwa.
Swala la usahihi au la hali husiani na kuwa kwenye battle au la.

Unaweza usiwe kwenye battle ukabakia kuwa sahihi kuliko aliyepo kwenye battle.

Maoni yangu nimeyatoa baada ya kuisoma petition ya Raila.
☝🏾Bado upo sahihi comrade, nami nasimamia pale pale huwezi kuona kwa ufanisi ukiwa nje ya nyumba but ukiingia unaweza kuongea kwa uzuri.
 
Mambo mengine hayahitaji nguvu sana kujua hatma yake.

Ukiwa na uzoefu kidogo tu unafahamu nini kinaweza jiri.

Sasa hii petition ya Raila to my opinion ni ya kisiasa tu.

Ushahidi mwingi umerembwa (coated).

Ukipata nafasi ya kuisoma petition kwa utulivu bila kuongozwa na hisia zozote utaona nachosema hapa.

Huyu mzee anakwenda kuangikia pua kama majaji watasimamia taaluma zao.
 
Kwa nini msiachie Mahakama waliobobea katika maswala haya ili wafanyie kazi kilichopelekwa mbele yao.Yani mmeshakuwa vichwani mwa panel itakayosikiliza hii petition na mmeshatoa na conclusion [emoji3]
 
Halafu wanao ongoza kumbully Mzee Odinga hapa ndiyo hao hao siku zote wanalalamikia swala la kukiukwa kwa haki za mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…