TANZIA Mzee Paul Sozigwa, aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Mwalimu Julius Nyerere afariki Dunia

Duh wanamtandao walihakikisha Mzee wetu anataabika hapa duniani.RIP Mzee Sozigwa.
 
Kichuguu
Nashukuru umenikumbusha mbali sana.
Mheshimiwa sana Baba yangu alikuwa akinisomea vitabu hivi, kimojawapo hiki che hadithi ya NOKORA MPUMBAVU, na Vitabu vya Pamela Ogoth Yule Author M-kenya,(sina hakika kama nimepatia)..Looong time. Sad😳😳😳😳
Old is GOLD!
R.I.E.P!
 
nadhani mnakumbuka siku moja mzee lowasa alisimama kwenye mkutano mkuu wa ccm akasema, 'kama isingekuwa busara za mzee mkapa usingekuwa rais na mwenye kiti wa chama leo hii'. maneno haya alikuwa anamwambia kikwete. alimwambia maneno hayo kwa sababu ya report ya mzee Nsozigwa (R.I.P) kwenye report yake kwenye kikao cha maadili cha ccm, ambapo kikwete alionekana kutokuwa na sifa za kugombea kutokana na kugubikwa na rushwa katika mchakato wake wa kuusaka urais.

mzee mkapa alitumia busara za kuiweka kapuni report ile, ili kuruhusu mgombea anayependwa na wananch wengi apewe nafasi ya kupeperusha bendera ya ccm, ambapo wakati huo alikuwa ni kikwete.

baada ya kikwete kuupata uraisi maisha ya Nsozigwa ndo yalianza kwenda kombo. maana alifungashiwa virago, katolewa kwenye nyumba ya serikali, kanyimwa mafao. akaenda zake kuishi tabata magengeni pale. Nilimuona siku moja pale tabata magengeni amevaa malapa anasubiria daladala. alifuatilia mafao yake bila mafanikio, maana mzee jk (huyu huyu mnaemmisi leo) alimpiga pini asipate chochote, kama kulimpizia kisasi kwa harakati zake za kumkwamisha katika mbio zake za uraisi.

dhoruba hii pia ilimkuta mzee Mangula, alikuwa keshaenda kulima nyanya njombe.. sema baada ya mambo kwenda kombo chamani, kikwete ikamlazimu kuwarudisha wazee wakisaidie chama. ndo mzee mangula kupewa rungu tena.
 
Sasa napata picha kwanini mafao yake yalileta mushkeli

Tukisema Chama Cha Mauaji wanakasirika,watuambie sababu z kumnyima stahiki zake huyu Mzee mpaka anakufa wakati enzi hizo ilikuwa Chama na Serikali ni kitu kimoja.
 
First Zaramo to get a University degree- RIP
 
Huyu Mzee alikuwa Mzaramo muadilifu sana na muumini mkubwa wa ujamaa inasemwa hata kuliko Mwalimu Nyerere. Kuna wakati gazeti la "Mfanyakazi" zama hizo lilitoa picha yake akiwa anatembea huku soli ya kiatu chake ikawa imechakaa ajabu!

Sasa hiyo ni sifa nzuri?

Hapo cha kujifunza kuhusu uadilifu wa ujamaani ni kwamba utaishia kutembea na viatu vinachomoka soli kama Mzee Sozigwa.

Kambona alipinga hizi itikadi akakimbizwa na Nyerere.
 
Alikua na nyumba Chang'ombe niliona kwenye vyombo vya habari mkewe anataka kuiuza na watoto wanaweka pingamiz huyu Mzee alikua na tatizo la kupoteza memory ilifikia kipindi anapotea. Rip
 
Huyu Mzee alikuwa Mzaramo muadilifu sana na muumini mkubwa wa ujamaa inasemwa hata kuliko Mwalimu Nyerere. Kuna wakati gazeti la "Mfanyakazi" zama hizo lilitoa picha yake akiwa anatembea huku soli ya kiatu chake ikawa imechakaa ajabu!

Sasa hiyo ni sifa nzuri kutembea na soli imelala upande?

Cha kujifunza kuhusu uadilifu wa ujamaani ni kwamba utaishia kutembea na viatu vinachomoka soli kama Mzee Sozigwa.

Kambona alipinga hizi itikadi akakimbizwa na Nyerere.
 
Huyu Mzee alikuwa Mzaramo muadilifu sana na muumini mkubwa wa ujamaa inasemwa hata kuliko Mwalimu Nyerere. Kuna wakati gazeti la "Mfanyakazi" zama hizo lilitoa picha yake akiwa anatembea huku soli ya kiatu chake ikawa imechakaa ajabu!

Sasa hiyo ni sifa nzuri kutembea na soli imelala upande?

Cha kujifunza kuhusu uadilifu wa ujamaa ni kwamba utaishia kutembea na viatu vinachomoka soli kama Mzee Sozigwa.

Kambona alizipinga vikali hizi itikadi extremist za Nyerere toka mwanzo, akakimbizwa nchini.
 
Kama mpaka anakufa alikuwa hajalipwa mafao yake basi tutegemee laana kwa hii nchi yetu.

Mzee amepumzika kwa Amani.
Isije ikawa ndo kisa cha mvua hizi. Tooba. Mkwere hukumtendea haki baba wa watu.
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na ustahamilivu wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…