Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Can be debated?Alipew mafao yake?
KichuguuRIP Mzee Sozigwa
Binafsi nitakukumbuka sana kwa utaalamu wako wa fasihi uliouonyesha katika vipindi vyako vya Mazungumzo Baada ya Habari. Yale mazungumzo yako ya Nokora Mpumbavu yaliishia kuwa dira yangu ya maisha kuwa popote nilipo huwa siwezi kusahau nilikotoka.
Sasa napata picha kwanini mafao yake yalileta mushkeli
First Zaramo to get a University degree- RIPnadhani mnakumbuka siku moja mzee lowasa alisimama kwenye mkutano mkuu wa ccm akasema, 'kama isingekuwa busara za mzee mkapa usingekuwa rais na mwenye kiti wa chama leo hii'. maneno haya alikuwa anamwambia kikwete. alimwambia maneno hayo kwa sababu ya report ya mzee Nsozigwa (R.I.P) kwenye report yake kwenye kikao cha maadili cha ccm, ambapo kikwete alionekana kutokuwa na sifa za kugombea kutokana na kugubikwa na rushwa katika mchakato wake wa kuusaka urais.
mzee mkapa alitumia busara za kuiweka kapuni report ile, ili kuruhusu mgombea anayependwa na wananch wengi apewe nafasi ya kupeperusha bendera ya ccm, ambapo wakati huo alikuwa ni kikwete.
baada ya kikwete kuupata uraisi maisha ya Nsozigwa ndo yalianza kwenda kombo. maana alifungashiwa virago, katolewa kwenye nyumba ya serikali, kanyimwa mafao. akaenda zake kuishi tabata magengeni pale. Nilimuona siku moja pale tabata magengeni amevaa malapa anasubiria daladala. alifuatilia mafao yake bila mafanikio, maana mzee jk (huyu huyu mnaemmisi leo) alimpiga pini asipate chochote, kama kulimpizia kisasi kwa harakati zake za kumkwamisha katika mbio zake za uraisi.
dhoruba hii pia ilimkuta mzee Mangula, alikuwa keshaenda kulima nyanya njombe.. sema baada ya mambo kwenda kombo chamani, kikwete ikamlazimu kuwarudisha wazee wakisaidie chama. ndo mzee mangula kupewa rungu tena.
Huyu Mzee alikuwa Mzaramo muadilifu sana na muumini mkubwa wa ujamaa inasemwa hata kuliko Mwalimu Nyerere. Kuna wakati gazeti la "Mfanyakazi" zama hizo lilitoa picha yake akiwa anatembea huku soli ya kiatu chake ikawa imechakaa ajabu!
Alikua na nyumba Chang'ombe niliona kwenye vyombo vya habari mkewe anataka kuiuza na watoto wanaweka pingamiz huyu Mzee alikua na tatizo la kupoteza memory ilifikia kipindi anapotea. Ripnadhani mnakumbuka siku moja mzee lowasa alisimama kwenye mkutano mkuu wa ccm akasema, 'kama isingekuwa busara za mzee mkapa usingekuwa rais na mwenye kiti wa chama leo hii'. maneno haya alikuwa anamwambia kikwete. alimwambia maneno hayo kwa sababu ya report ya mzee Nsozigwa (R.I.P) kwenye report yake kwenye kikao cha maadili cha ccm, ambapo kikwete alionekana kutokuwa na sifa za kugombea kutokana na kugubikwa na rushwa katika mchakato wake wa kuusaka urais.
mzee mkapa alitumia busara za kuiweka kapuni report ile, ili kuruhusu mgombea anayependwa na wananch wengi apewe nafasi ya kupeperusha bendera ya ccm, ambapo wakati huo alikuwa ni kikwete.
baada ya kikwete kuupata uraisi maisha ya Nsozigwa ndo yalianza kwenda kombo. maana alifungashiwa virago, katolewa kwenye nyumba ya serikali, kanyimwa mafao. akaenda zake kuishi tabata magengeni pale. Nilimuona siku moja pale tabata magengeni amevaa malapa anasubiria daladala. alifuatilia mafao yake bila mafanikio, maana mzee jk (huyu huyu mnaemmisi leo) alimpiga pini asipate chochote, kama kulimpizia kisasi kwa harakati zake za kumkwamisha katika mbio zake za uraisi.
dhoruba hii pia ilimkuta mzee Mangula, alikuwa keshaenda kulima nyanya njombe.. sema baada ya mambo kwenda kombo chamani, kikwete ikamlazimu kuwarudisha wazee wakisaidie chama. ndo mzee mangula kupewa rungu tena.
Yule Mzee Mkongwe na Gwiji la siasa l za Tanzania Mzee Sozigwa amefariki Dunia. Sozigwa alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Mtoto wa Mzee Sozigwa, Mchungaji Moses Sozigwa alisema tatizo la kwanza lililokuwa likimsumbua baba yao ni kupoteza kumbukumbu. Baadaye ilikuja kubainika ana tatizo la moyo, madaktari walisema moyo wake umekuwa mkubwa.
View attachment 508065
Paul Sozigwa ndiye Katibu wa kwanza wa Rais (IKULU-HABARI).
Mbali na kuwa katibu wa Ikulu, nyadhifa nyingine alizoshika ni Mkurugenzi wa kwanza wa Redio Tanzania(RTD), DO Wilaya ya Kisarawe katika serikali ya kikoloni na katibu Mkuu, Wizara ya Habari na Utangazaji.
Vilevile alishawahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya CCM zikiwemo za Mjumbe wa NEC, CC na M/kiti Tume ya Taifa ya Udhibiti na Nidhamu na M/kiti wa CCM mkoa wa Pwani.
View attachment 508066
Kutoka kushoto: Habib Halala, Paul Sozigwa, Mwalimu J.K. Nyerere, Brig. Hashim Mbita na Benjamin Mkapa mwaka 1985.
Rest in peace Mzee wetu
=======
Byendangwero Said
View attachment 508072
Kwa maoni yangu, sifa kuu inayompambanua mzee Sozigwa katika maisha yake yote ya siasa hapa alihubiri kile alichokiamini.
Katika miaka ya sabini, akiwa mkugenzi wa Redio Tanzania, alianzisha kipindi redioni kilichojulikana kwa jina la; "Mikingamo" katika mojawapo ya vipindi vyake, alisema kuwa ubepali ulikuwa unyama. Na kweli, mzee Sozigwa hata baada ya kusambaratika kwa siasa ya ujamaa aliendelea kuishi kama mjamaa.
Nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 1990, akiwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM alikuja Bukoba kwa shughuli za kikazi; mh. Kimiti wakati huo akiwa mkuu wa mkoa (k) alimtumia gari ya kwenda kumpokea melini; dereva alipomtafuta katika vyumba vyote vya daraja la kwanza hasimpate akarudi na kuripoti kwa bosi wake kuwa mzee hakuja; kumbe yeye alikuwa amekuja kwenye daraja ya tatu. Baadaye alimpigia mh. Kimiti kumjulisha kuwa alikuwa tayari amewasili na amefikia coffee Tree Inn.
Baadaye wakati tukinywa chai pamoja yule dereva alikuja kuomba msamaha huku akijitetea kuwa alikuwa amepita kwenye vyumba vyote vya daraja la kwanza lakini hakumuona.
Kitu alichomjibu mzee yule ni;"wewe nani alikwambia kuwa chama kina fedha za kupoteza kwa kusafirisha watu daraja la kwanza." Na aliyasema hayo miaka mingi baada ya azimio la Zanzibar kuiweka CCM katika njia ya ubepari.
View attachment 508073
Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia CCM wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005, sekretariati ya CCM chini ya Philip Mangula iliazimia kuondoa mgombea yeyote atakakayebainika kutoa rushwa kwenye kinyanganyiro.
Mzee Sozingwa akiwa anasimamia idara ya nidhamu katika sekretariati hiyo akalivalia njuga azimio hilo, Nakumbuka wakati Kikwete alipokuja Bukoba kusaka wadhamini, mzee Sozigwa alikuwepo akifuatilia nyendo zote zilizoashiria kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
Inasemekana wakati wa kujadili wagombea urais katika kamati kuu taarifa aliyokuwa ameiandaa ilitupwa kapuni, na hatimaye sekretarati yote ilifungiwa virago baada ya JK kuukwea wenyekiti wa CCM.
Huyu Mzee alikuwa Mzaramo muadilifu sana na muumini mkubwa wa ujamaa inasemwa hata kuliko Mwalimu Nyerere. Kuna wakati gazeti la "Mfanyakazi" zama hizo lilitoa picha yake akiwa anatembea huku soli ya kiatu chake ikawa imechakaa ajabu!
Huyu Mzee alikuwa Mzaramo muadilifu sana na muumini mkubwa wa ujamaa inasemwa hata kuliko Mwalimu Nyerere. Kuna wakati gazeti la "Mfanyakazi" zama hizo lilitoa picha yake akiwa anatembea huku soli ya kiatu chake ikawa imechakaa ajabu!
Isije ikawa ndo kisa cha mvua hizi. Tooba. Mkwere hukumtendea haki baba wa watu.Kama mpaka anakufa alikuwa hajalipwa mafao yake basi tutegemee laana kwa hii nchi yetu.
Mzee amepumzika kwa Amani.