JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mzee Said Mohamed ambaye ni Baba Mzazi wa Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) amefariki dunia alfajiri ya leo Machi 1 2022 na anatarajiwa kuzikwa leo saa kumi jioni kwenye makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

Marehemu Mzee Said ni Mfanyabiashara wa muda mrefu Tanzania ambapo alianzisha biashara ya kwanza mwaka 1955 kwa kuuza bidhaa ndogondogo Tanga lakini baadaye alihamia kuuza nguo na kuhama kutoka Tanga hadi Songea ambako alijitanua katika kilimo cha korosho ambacho Familia yake imekiendeleza hadi leo.

Marehemu Mzee Said alistaafu mwaka 1996 na kuruhusu kizazi kilichofuatia kuchukua usukani wa kila siku wa biashara na kuamua kuhamia Dar es Salaam na kuwa wasambazaji wakubwa wa mazulia ya PVC ndani ya Tanzania na nchi jirani.

Ghalib Said Mohamed (GSM) ni mdhamini wa Klabu ya Yanga ambapo amekuwa na msaada mkubwa miaka ya hivi karibuni tangu alipoanza uwekezaji klabuni hapo.

 
Mzee Said Mohamed ambaye ni Baba Mzazi wa Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) amefariki dunia alfajiri ya leo March 1 2022 na atazikwa leo saa kumi jioni kwenye makaburi ya Kisutu Dar es salaam.

Marehemu Mzee Said ni Mfanyabiashara wa muda mrefu Tanzania ambapo alianzisha biashara ya kwanza mwaka 1955 kwa kuuza bidhaa ndogondogo Tanga lakini baadae alihamia kuuza nguo na kuhama kutoka Tanga hadi Songea ambako alijitanua katika kilimo cha korosho ambacho Familia yake imekiendeleza hadi leo.

Marehemu Mzee Said alistaafu mwaka 1996 na kuruhusu kizazi kilichofuatia kuchukua usukani wa kila siku wa biashara na kuamua kuhamia Dar es Salaam na kuwa Wasambazaji wakubwa wa mazulia ya PVC ndani ya Tanzania na nchi jirani.


Pichani ni mzee Said Mohammed(Katikati) akiwa na wanae wawili
 
Poleni sana GSM company, innalilayhi wa inayilaihy rajiuun
 
Ni Saad mohamed na sio said mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…