IDFakenyingine
Senior Member
- Sep 28, 2022
- 176
- 441
Inkuntum tuhibbuna-Llaaha Fattabi'uuni...Mimi ni muislam lakini katika suala la kuwahisha mazishi niko kinyume na wengi.
Kuzika haraka mtu anapofariki sio muongozo wa quran bali ni maelekezo ya mtume wetu kutokana na wakati wao hakukuwa na teknolojia ya kuhifadhi maiti ili ikae muda mrefu.
Pia kutokana na joto la huko jangwani ikawa ni rahisi maiti kuharibika upesi, lakini pia kutokana na kukosa mawasiliano ya simu wakati huo ikawa sio rahisi kuwapelekea taarifa watu waliopo mbali ili wawahi mazishi, kwa hiyo mtume kwa hekima akasema kati ya mambo yanayotakiwa kufanywa haraka basi mazishi ni mojawapo.
Sasa kwa kuwa nyakati zimebadilika, teknolojia imekua kwa maana maiti inaweza kuhifadhiwa muda mrefu na pia wafiwa pengine wapo mbali na taarifa wamepata kupitia simu au whatsapp, je kuna ubaya gani kuchelewesha mazishi kwa sababu mazishi pia ni ibada mtu akihudhuria anapata thawabu.
Haya ni maoni yangu binafsi kwa sababu kuna Uislam na Uarabu, kun mambo inabidi kuyafuata kama Uislam unavyosema lakini pia kuna masuala ya utamaduni wa kiarabu ambao huku kwetu hauko applicable sio mbaya kama tutaacha huo utamaduni bila kuathiri dhima ya Uislam.
Wewe sii muislam.
Km ni muislam, hujielewi!