PostGE2025 Mzee wa Upako: Wanaosema Rais Samia anakosolewa sababu Muislamu, wamefilisika kimawazo. Wajibu hoja, wasiingize mambo mengine

PostGE2025 Mzee wa Upako: Wanaosema Rais Samia anakosolewa sababu Muislamu, wamefilisika kimawazo. Wajibu hoja, wasiingize mambo mengine

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Utashangaa Sasa watakao mjibu Mzee Wa upako wataanza kuiponda kofia yake na maisha yake hawata jibu hoja yake hata moja
 
Kufupisha habari, Mzee kasema yule mkubwa amefilisika kimawazo.
 
Amekosea kimoja kudai alipata asilimia 98 wakati tunajua matokeo ni feki
 
Wale wazee wananikera sana wanapoleta mambo yao ya udini yasiyokuwepo..
 
Kut 3:7-9
BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
MENE MENE TEKELI NA PERESI

Maandishi yenyewe ni: ‘MENE, MENE, TEKELI, PARSINI.’ Na hii ndiyo maana yake: MENE maana yake, Mungu amehesabu siku za ufalme wako na kuukomesha. TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. PERESI maana yake, ufalme wako umegawanywa kati ya Wamedi na Wapersi
 
Back
Top Bottom