Vinci Dayot Upamecano
JF-Expert Member
- Nov 11, 2020
- 524
- 1,288
Mimi sina noma na huyu mzee, lakini bwana father kazidisha kwakweli. Yeye hakuna meme au video ya kuchekesha inampita lazima ataiweka status tu, yaani hadi sometimes watu wangu wa karibu wenye namba yake wanakuwa wanascreen shot vitu vya ajabu alivyo'post mzee wangu na kunitumia huku wakiambatanisha na mshangao au kicheko!
Kwani huyu mzee ana shida gani lakini!? Mbona smart phone kanza kutumia kitambo sana tu. Yaani hapitwi na tukio lolote mzee wangu lazima ataliapload tu, na muda wote yeye status zake WhatsApp hazikauki hakuna tukio limetrend Bongo limempita father.
Nikijaribu kumwambia, "Sasa father kuna baadhi ya vitu saivi unatakiwa upunguze kupost mtandaoni", ataishia ku-reply kwa emoji za kucheka halafu cha kushangaza atanitumia na mimi vimeme viwili vitatu au stickers zile za kuchekesha basi.
Ni kweli kabisa kuna vingine vinachekesha sana lakini inabidi apunguze ukizingatia na umri wake umeshakwenda, naamini hata humu JF kuna baadhi ya wanajukwaa wana namba yake na watakuwa wanaenjoy sana memes zake lake jaribuni kumshauri na ninyi mzee wangu apunguze kidogo anajishusha ananishusha na mimi mwanaye.
Ramadan Mubarak.