Mzee wangu anapost sana memes mtandaoni!

Mzee wangu anapost sana memes mtandaoni!

Vinci Dayot Upamecano

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2020
Posts
524
Reaction score
1,288
Mimi sina noma na huyu mzee, lakini bwana father kazidisha kwakweli. Yeye hakuna meme au video ya kuchekesha inampita lazima ataiweka status tu, yaani hadi sometimes watu wangu wa karibu wenye namba yake wanakuwa wanascreen shot vitu vya ajabu alivyo'post mzee wangu na kunitumia huku wakiambatanisha na mshangao au kicheko!

Kwani huyu mzee ana shida gani lakini!? Mbona smart phone kanza kutumia kitambo sana tu. Yaani hapitwi na tukio lolote mzee wangu lazima ataliapload tu, na muda wote yeye status zake WhatsApp hazikauki hakuna tukio limetrend Bongo limempita father.

Nikijaribu kumwambia, "Sasa father kuna baadhi ya vitu saivi unatakiwa upunguze kupost mtandaoni", ataishia ku-reply kwa emoji za kucheka halafu cha kushangaza atanitumia na mimi vimeme viwili vitatu au stickers zile za kuchekesha basi.

Ni kweli kabisa kuna vingine vinachekesha sana lakini inabidi apunguze ukizingatia na umri wake umeshakwenda, naamini hata humu JF kuna baadhi ya wanajukwaa wana namba yake na watakuwa wanaenjoy sana memes zake lake jaribuni kumshauri na ninyi mzee wangu apunguze kidogo anajishusha ananishusha na mimi mwanaye.

Ramadan Mubarak.
 
Mkuu wewe jikite kutafuta hela. Wazazi huwa wanasikiliza watoto wenye wapo vizuri kifedha. Kama hauna hela hauwezi kumshauri anaona kama una msongo wa mawazo na unataka kumalizia stress zako kwake.
 
Ukifanya utafiti Wapost memes ktk mitandao hasa WhatsApp, Wengi wao wana stress za kimaisha... Hizo memes zina wafariji... Na ukiwauliza mbona unapost sana mitandaoni wanakuja na majibu ya kujitetea na kipuuzi tu... Mchunguze baba yako ana stress zipi ukiweza msaidie...
 
Nadhani umekariri kuwa ukifika umri fulani uishi kwa style fulani.

Hivi unajua wazee nao huwa wanaishi maisha kama ya wewe unayoishi na masela wako kwenye messages.

Cha kukushauri, mfundishe jinsi ya kuwa block wale anaohisi hawarakiwi kuona status zake za vichekesho ndivyo ambavyo Kuna mzee fulani ni rafiki angu nilipata fanya nae kazi mahala fulani, anaweka status zake.
 
Yaani vijana wanaona uzee kama ugonjwa au ulemavu....... unaweza kukuta mtu mwenyewe anayeitwa mzee hata miaka 70 hana.......

Vijana wajue kuwa uzee ni hali tu ya kuongeka na kuchoka mwili.....lakini nafsi haizeeki...... kutokana na umri Kuna mambo tu unajizuia kuyafanya kutokana na taswira yako kwenye jamii iliyokuzunguka......
 
Back
Top Bottom