Mzee Warioba akieleza jinsi Zanzibar walivyopora mamlaka ya raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kujitoa kwenye muungano kinyemela!

Basi mwakani ni lazima tumwambie Samia kama bado anautaka Urais, akagombee Zanzibar, na siyo Tanganyika, maana anayetajwa kuwa Rais wa Tanzania, kiuhalisia ni Rais wa Tanganyika.


Hii ni fedheha kubwa!! Yaani Tanganyika inatawaliwa na mtu ambaye siye raia wa Tanganyika!!

Samia awaondoe haraka sana mamia ya wazanzibari aliowatrua na kuwapachika kwenye nafasi mbalimbali za kiutawala Tanganyika. Kama anawataka, awapeleke Zanzibar maana kule wanan nchi yao.
TAnganyika is dead, labda useme "bara"
Tanganyika haijafa na haitakuja kufa. Inaweza kubadilisha majina mara kadhaa lakini haiwezi kufa. Ni sawa na wewe, ukitaka unaweza kwenda kuapa kwa wakili na kulibadilisha jina lako lakini hiyo haimaanishi umekuwa mtu mwingine.
 
Has
Na hasa masikini wa akili.
 
Ingekua ipo hai, mzenji mnaemlalamikia anaongoza asingeweza kua madarakani anaongoza hiyo tanganyika
 
Kipindi kile walipoioitisha tu Katiba yao, sikuwahi kufikiri kwamba Muumgano huu ungeishi zaidi ya miaaka 6 iliyofuatia. Kupitia ile Katiba tayari Muungano ulikuwa umeshakufa.

Hata sasa nadhani kinachopelekea Zanzibar ku delay kuna vitu wanamakizia kuvichuma, na mkiona siku linatengenezwa tukio kubwa litakalopelekea vifaa vingi vya kisasa vya kijeshi vinapelekwa zanzibar kutumika kwenye zoezi, hilo, ndege za ATC, Dreamliner na Airbus, na ile ya mizigo nazo zikaenda Zanzibar kwa wakati mmoja. Meli nazo zikatakiwa kwenda huko.

Siku hiyo mkiona hayo yanayokea, nasi mjue siku hiyo ndiyo Zanzibar watatangaza kuvunja Muungano ambapo kilichopo kule kitabaki kule na kilichopo Tanganyika kitabaki Tanganyika.
Zanzibar kupitia Katiba yao wameshajitoa, kilichobaki ni Tangazo rasmi tu
 
Samia hadi 2030 halafu ndo atuachie wagalatia,,,kwa sasa akija msikiti mwengine asije akataka kukaa mpaka 2035
 
Muungano haupo ni vile Zanzibar bado wanachuma mali za wajinga bara pamoja na ajira, sahivi Zanzibar haidaiwi deni lolote nje bara tunalipa kila kitu nadhani ndiyo taifa pekee hana deni duniani.
 
Ingekua ipo hai, mzenji mnaemlalamikia anaongoza asingeweza kua madarakani anaongoza hiyo tanganyika
DRC kuna wakati iliitwa Congo Kinshasa, Baadaye ikaitwa Zaire, leo inatwa DRC. Nchi ni ile ile, majina tu ndiyo yanabadilika.

Na tunavyoenda, naamini lazima hii iliyoitwa Tanganyika, kisha Tanzania bara, ama italirudia jina lake la awali au itaitwa jina jingine, lakini nchi itabakia ni ile ile.

Mzanzibari kuongoza Tanganyika, ni makosa tu ya kiutawala, na makosa, mara nyingi husahihishwa pale wahusika wanapokubali kuwa kuna makosa.

Tume ya Warioba na Watanzania waliotoa maoni waliliona hilo, ndiyo maana walisema kuwa Muungano kuwe na Serikali 3: ya Zanzibar itakayoongozwa na Rais wao (itaongozwa na mzanzibari kama ilivyo sasa), ya Tanganyika (itakayoongozwa na mtanganyika, tofauti na ilivyo sasa), na ya Tanzania (ambayo inaweza kuongozwa kwa kupokezana).
 
Muungano haupo ni vile Zanzibar bado wanachuma mali za wajinga bara pamoja na ajira, sahivi Zanzibar haidaiwi deni lolote nje bara tunalipa kila kitu nadhani ndiyo taifa pekee hana deni duniani.

Mtu na nduguye, wakishirikiana na vibaraka wa Tanganyika akina Mwegulu, Majiliwa et al, wameamua kuitumia Tanganyika, kuijenga Zanzibar.

Fikiria watu 0.5% ya population ya Tanzania wanagawiwa 19% ya mikopo na misaada yote, lakini wa kulipa madeni ni Tanganyika! Wazanzibari walikuwa wanapata 4% ambayo bado ilikuwa ni kubwa mno kwa kuzingatia idadi ya watu na ukubwa wa Zanzibar. Cha ajabu, wanayemwita mama, kaongeza mpaka 19%!!, na matanganyika vibaraka na machawa, yanashangilia.
 
Muungano ni falsafa iliokufa na kubaki vichwani mwa wanasiasa wa ccm, kimsingi muungano ulikufa muda mrefu , ukweli uwepo wa ccm Zanzibar na Tanganyika ndio uzi ulioshika hicho kinachoitwa muungano ambacho pia haipo,
 
Zanzibar ina mamlaka yake kamili lakini Tanganyika imejificha kwenye koti la muungano , ambao kimantiki haupo
 
Na Jeshi JWTZ walipeleke Zanzibar kisha watangaze muungano umevunjika😀

Ni hivi kamanda, Zanzibar hawawezi kutangaza rasmi bila makubaliano na bara kwamba muungano umevunjika, ndio maana wanauvunja kinyemela na kimyakimya. Wakitangaza rasmi itakuwa uhaini, na itabidi JWTZ waende Zanzibar kuvunja uasi.

Ila sasa, JWTZ hawawezi kuwa deployed kuingia Zanzibar bila amri ya raisi wa Tanzania. Hivyo kama Zanzibar wanataka kutangaza kujitenga ni sasa wakati Tanzania ina raisi wa Zanzibar. Hata hivyo, sidhani kama raisi Samia atazuia jeshi kuingilia kati, kwa sababu Zanzibar wakitangaza kujitenga na yeye akakaa kimya basi itabidi na yeye aondolewe. Kumbuka Samia ni raisi kwa sababu JWTZ walikubali awe raisi. Sehemu moja ambayo raisi Samia anajua hataweza kuiweka kabisa kwapani ni JWTZ. Hili litabaki predominantly la Watanzania bara, hata akiwaambia vijana wote wa Zanzibar wajiunge na JWTZ. Taasisi moja iliyomweka sawa Mwinyi wakati ule ilikuwa JWTZ, wakati wa Generali Mwita Kiaro, na Samia anajua hilo. Kwanza wanajeshi wa Zanzibar maserule sana.
 
Shida ni ccm ya Tanganyika..ifike mahali isiende kama gurudumu lililochomoka kwenye gari
Tatizo ni kwamba kuna watu ndani ya CCM wanafaidika sana na hali iliyopo, na wanajua mabadiliko ni jambo la hatari sana kwao. Na ndio maana nahisi hawa ndio wanatumia hata taasisi za serikali za ulinzi na usalama kuondoa watu wanaopinga ujinga na kukosoa serikali, ndio maana kuna confusion watu wakidhani hzi operation za kuteka na kuua zinafanywa chini ya maelekezo ya serikali. Uwezekano mkubwa ni kwamba zinafanywa na vyombo vya serikali kwa watu kufani kuvitumia vyombo vya dola kwa manufaa binafsi
 
Ililetwa hoja ya selikali 3 ikabezwa vikali kisa ililetwa wakati ambao upande Fulani wanautawala upande Fulani,Leo mungu kaingilia kati mambo yamebadilika munaleta malalamiko, sometimes adui wa hii nchi ni unafki, tuachane na unafki aisee tutafka mbali nawaambia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…