Tuliona kazi iliyotukuka iliyofanywa na Tume ya kukusanya maoni juu ya Katiba mpya mwenyekiti wa Tume hiyo akiwa Mzee Warioba.
Walikuwepo wazee kama Mzee Sitta walioshiriki katika mchakato huo katika ngazi mbalimbali, pamoja na kuwa na afya njema enzi hizo, Leo hatunao tena Duniani lakini Mzee Warioba yupo.
Mzee Warioba ni Mzee aliyelitumikia Taifa letu Kwa uadilifu mkubwa na ameshiriki kikamilifu kulisaidia Taifa kufika hapa tulipo kwa uzoefu na busara zake.
Mzee Warioba ni Mzee amekula chumvi nyingi na kushiba siku nyingi za kheri katika Nchi yetu nzuri Tanzania. Hadi hivi leo Watanzania tunatambua mchango wake katika mambo mengi, lakini jambo kuu lililotugusa Watanzania ni Utumishi wake uliotukuka katika mchakato wa Katiba mpya.
Alizunguka Nchi nzima akiwa na Tume yake na Watanzania tulishiriki Kutoa maoni tukimuamini Nia yake njema juu ya Taifa letu. Pamoja na mchakato huo kukwama mwaka 2014, bado wananchi tunayo Imani juu yake kuwa ana uwezo kusaidia Nchi kupata KATIBA mpya nzuri ya kulivusha Taifa letu Kwa sasa.
Mnyukano unaoendelea wa wasaka urais usipotanguliwa na kupatikana Kwa Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi, hakika "Watatoana macho"
Watanzania tunaendelea kumuombea Kwa Mwenyezi Mungu amjalie maisha marefu Ili ashuhudie Kwa macho yake maono yake ya nchi yetu ikipata katiba mpya itakayozaa vyama imara, Uchumi imara, viongozi mahiri na Usimamizi bora wa Raslimali zetu Kwa Sheria zinazotekelezeka.
USHAURI: Mzee Warioba Bado ana nguvu, busara, nia na utayari wa kumalizia kazi aliyoianza.
Arudishwe kwenye Tume ya Katiba mpya, mchakato uhuishwe UPYA, tuondoe uchafuzi Ule unaoitwa "Katiba Pendekezwa".
Tuanze na Rasimu ya Katiba mpya kabla ya kuingia Bunge la Katiba, mchakato uanzie hapo, tujadiliane Kwa kina mfumo mzuri wa kuwapata wabunge wa Bunge maalum la Katiba wasio mapandikizi ya chama Dola, na hatimaye tupate KATIBA mpya.
Mungu mbariki Mzee Warioba.
Mungu ibariki TANZANIA.
Amen.