Ni muda mwafaka Kwa Taifa letu:
1. Kupata Mawaziri wasiotokana na wabunge.
2. Wakuu wa wilaya na mikoa waondolewe, tupate viongozi wa kisiasa waliopigiwa kura kuanzia mbunge, diwani, mkuu wa Jimbo nk.
3. Viongozi watangaze Mali zao wanapoingia katika uongozi na wanapotoka.
4. Wazee wote walipwe pension bila ubaguzi unaowaacha waliofanya KAZI sekta binafsi, Nchi itabarikiwa.
5. Sauti ya wananchi iheshimiwe. TABIA hii ya kutowajibika Kwa viongozi wanaotuhumiwa Kwa RUSHWA ikome. Katiba mpya tuhakikishe inatatua shida hii.
6. Wezi wote walioliibia Taifa ktk miradi mbalimbali warudishe pesa zetu.
Tusipoteze Kodi za wananchi kuzungukwa Bure, Rasimu alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani tufanye marekebisho.
Mzee Warioba ateuliwe kumalizia KAZI njema aliyoianza.