Mzee Warioba ateuliwe tena kukamilisha kazi aliyotumwa na Watanzania

Mzee Warioba ateuliwe tena kukamilisha kazi aliyotumwa na Watanzania

Lisu.
Kabudi.
Warioba.
Kinana.
Mnyika.
Zito.
Watuandalie katiba
Bila kumsahau Dr Wilbroad SLaa.

Anyway,

RASIMU ya judge WARIOBA IPO, irudishe mezani, yafanyike maboresho kidogo tuchague wajumbe wa Bunge maalum la Katiba.
 
Ikipatikana KATIBA mpya Bora, muda kama huu Ripoti ya cag imetoka tu, tayari WEZI wa pesa zetu wangeshakamatwa bila hata ya Rais Kutoa maelekezo.
 
😅😅😅Mama anakwepa kwepa sana Katiba Mpya nishaona.
Ni Kweli wanajaribu kukwepa lakini imeshindikana sababu Muda wa KATIBA mpya Tanzania umefika.

Mzee PINDA na Mzee Wassira walitangulizwa Ili kutufanya tumsahau Mzee Warioba lakini wameishia kutafutiwa KAZI nyingine.
 
Kweli aisee laana za watz

Tuliona KAZI iliyotukuka iliyofanywa na Tume ya kukusanya maoni juu ya Katiba mpya mwenyekiti wa Tume hiyo akiwa Mzee Warioba.

Walikuwepo wazee kama Mzee Sitta walioshiriki katika mchakato huo katika ngazi mbalimbali, pamoja na kuwa na AFYA njema enzi hizo, Leo hatunao tena Duniani lakini Mzee Warioba yupo.

Mzee Warioba ni Mzee aliyelitumikia Taifa letu Kwa uadilifu mkubwa na ameshiriki kikamilifu kulisaidia Taifa kufika hapa tulipo Kwa uzoefu na BUSARA zake.

Mzee Warioba ni Mzee amekula chumvi nyingi na kushiba siku nyingi za kheri katika Nchi yetu nzuri TANZANIA. Hadi hivi Leo Watanzania tunatambua mchango wake katika mambo mengi ,lakini jambo kuu lililotugusa Watanzania ni Utumishi wake uliotukuka katika mchakato wa KATIBA mpya.

Alizunguka Nchi nzima akiwa na Tume yake na Watanzania tulishiriki Kutoa maoni tukimuamini Nia yake njema juu ya Taifa letu. Pamoja na mchakato huo kukwama mwaka 2014, bado wananchi tunayo Imani juu yake kuwa ana uwezo kusaidia Nchi kupata KATIBA mpya nzuri ya kulivusha Taifa letu Kwa sasa.

Mnyukano unaoendelea wa wasaka urais usipotanguliwa na kupatikana Kwa Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi, HAKIKA "Watatoana macho" .

Watanzania tunaendelea kumuombea Kwa Mwenyezi Mungu amjalie maisha marefu Ili ashuhudie Kwa macho yake MAONO yake ya nchi yetu ikipata KATIBA mpya itakayozaa vyama imara, Uchumi imara, viongozi mahiri na Usimamizi Bora wa Raslimali zetu Kwa SHERIA zinazotekelezeka.

USHAURI: Mzee Warioba Bado ana nguvu, BUSARA, Nia na utayari wa kumalizia KAZI aliyoianza.

Arudishwe kwenye Tume ya KATIBA mpya, mchakato uhuishwe UPYA, tuondoe uchafuzi Ule unaoitwa " KATIBA Pendekezwa".

Tuanze na RASIMU ya KATIBA mpya kabla ya kuingia Bunge la Katiba, mchakato uanzie hapo, tujadiliane Kwa kina mfumo mzuri wa kuwapata wabunge wa Bunge maalum la Katiba wasio mapandikizi ya chama Dola, na hatimaye tupate KATIBA mpya.

Mungu mbariki Mzee Warioba,

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen.
Naunga mkono hoja.
 
Ni muda mwafaka Kwa Taifa letu:

1. Kupata Mawaziri wasiotokana na wabunge.

2. Wakuu wa wilaya na mikoa waondolewe, tupate viongozi wa kisiasa waliopigiwa kura kuanzia mbunge, diwani, mkuu wa Jimbo nk.

3. Viongozi watangaze Mali zao wanapoingia katika uongozi na wanapotoka.

4. Wazee wote walipwe pension bila ubaguzi unaowaacha waliofanya KAZI sekta binafsi, Nchi itabarikiwa.

5. Sauti ya wananchi iheshimiwe. TABIA hii ya kutowajibika Kwa viongozi wanaotuhumiwa Kwa RUSHWA ikome. Katiba mpya tuhakikishe inatatua shida hii.

6. Wezi wote walioliibia Taifa ktk miradi mbalimbali warudishe pesa zetu.

Tusipoteze Kodi za wananchi kuzungukwa Bure, Rasimu alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani tufanye marekebisho.

Mzee Warioba ateuliwe kumalizia KAZI njema aliyoianza.
 
Ni muda mwafaka Kwa Taifa letu:

1. Kupata Mawaziri wasiotokana na wabunge.

2. Wakuu wa wilaya na mikoa waondolewe, tupate viongozi wa kisiasa waliopigiwa kura kuanzia mbunge, diwani, mkuu wa Jimbo nk.

3. Viongozi watangaze Mali zao wanapoingia katika uongozi na wanapotoka.

4. Wazee wote walipwe pension bila ubaguzi unaowaacha waliofanya KAZI sekta binafsi, Nchi itavarikiwa.

5. Sauti ya wananchi iheshimiwe. TABIA hii ya kutowajibika Kwa viongozi wanaotuhumiwa Kwa RUSHWA ikome. Katiba mpya tuhakikishe inatatua shida hii.

6. Wezi wote walioliibia Taifa ktk miradi mbalimbali warudishe pesa zetu.

Tusipoteze Kodi za wananchi kuzungukwa Bure, Rasimu alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani tufanye marekebisho.

Mzee Warioba teuliwe kumalizia KAZI njema aliyoianza.
Ameen emeen
 
Ukome kubeza Watanzania huku Ukijidai kuwatetea wadai Katiba Mpya wakati mna ajenda ya siri mnayotaka iwanufaishe nyie maharamia kwa kujificha kwwnye chaka la kudai ati 'Warioba' Wacheni kuwatukana na kuwabeza Watanzania.

Kweli aisee laana za watz
Una matatizo na Waafrika.
 
Ukome kubeza Watanzania huku Ukijidai kuwatetea wadai Katiba Mpya wakati mna ajenda ya siri mnayotaka iwanufaishe nyie maharamia kwa kujificha kwwnye chaka la kudai ati 'Warioba' Wacheni kuwatukana na kuwabeza Watanzania.

Una matatizo na Waafrika.
Kudai KATIBA mpya na agenda ya Siri wapi na wapi ndugu SYLLOGIST?
 
Kudai KATIBA mpya na agenda ya Siri wapi na wapi ndugu SYLLOGIST?
Mkuu Rabbon wala usifadhaike...bandiko langu limekuwa limeelekezwa kwa Baadhi ya wachangiaji, na hususani hapo juu ilikuwa kwa Bush Dakta.

Hakika lengo langu halikuwa Direct kwa mada yako. Mimi binafsi ni mmoja wa wale wanaotaka Tuendelee pale alipoacha Mzee Warioba. Samahani kwa kukukwaza. Tuendelee kuipigania nchi yetu sote.
 
Ukome kubeza Watanzania huku Ukijidai kuwatetea wadai Katiba Mpya wakati mna ajenda ya siri mnayotaka iwanufaishe nyie maharamia kwa kujificha kwwnye chaka la kudai ati 'Warioba' Wacheni kuwatukana na kuwabeza Watanzania.

Una matatizo na Waafrika.
Hasira za nini au nyie ndio wanufaika na hii iliyopo
 
Hasira za nini au nyie ndio wanufaika na hii iliyopo
Mimi sina hasira ndugu Wewe ndio unakasirika, nasema, Acha kuwatukana Watanzania... Kudai kuwa watanzania wamelaaniwa ni kuwatukana. Na huwezi kuwa raia mwema au mzalendo kwa mtazamo wangu, kwa kuwatia doa wananchi wenzako na, au wenzakokuwa wamelaaniwa huku wakati huo huo ukidai uko nao kudai katiba mpya.... Hiyo haiwezekani nakusihi uache kufanya hivyo, Ukome, kwani sioni sababu ya kuwa na lugha ya chuki kwenye bandiko lako....No one has provoked you and thus far ulitaka kutukana tu.. hiyo ni nini? Wewe umelaaniwa?
 
CCM tujisahihishe.

KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi iliyo dhahiri bila Hila ndani yake, ndiyo njia nzuri yenye Nuru njema Kwa Taifa.

Tukubali kupatikana Kwa Katiba mpya hata kama chama Chetu kitapoteza umiliki wa Dola.

Nchi Bado itakuwa salama hata kama CCM itakufa.

Mzee Warioba arudishwe kukamilisha KAZI njema iliyotukuka.
 
Ndani ya Rasimu alosimamia Mzee Warioba, wananchi tulipendekeza Serikali ya majimbo.

Muundo huu wa Serikali utasaidia kuondoa Hila Kwa viongozi wenye uchu wa madaraka ambao hugawanya majimbo ya Uchaguzi Ili kupata uwakilishi bungeni au kupunguza nguvu ya upinzani.

Mfano mzuri ni Wazi lililotolewa Leo kuomba Bunge kuligawa Jimbo la Mbeya mjini.
 
Lissu: Serikali haijajibu mapendekezo yoyote Hadi sasa Kwa mwaka nzima kuhusiana na namna Bora za kupata KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

Nashauri CDM ijiondoe katika maridhiano Ili tuungane mtaani kuidai Katiba ya Kweli.

Bring back our WARIOBA!!!!
 
Dr SLAA amekiri kuwa Tundu Lisu ni kiongozi MKWELI asiyeficha UKWELI, hivyo kukiri kwake juu ya Serikali kupuuza mapendekezo ya CDM juu ya Katiba mpya ni Ishara kuwa hawana Nia ya kuingia katika uchaguzi 2024 Kwa Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

CDM ijitoe katika maridhiano.

Tuungane kuidai mtaani Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

Bring back our WARIOBA 💪💪💪
 
Bring back our WARIOBA 💪 💪 💪💪

Pesa za Watanzania ziheshimiwe.

Rasimu ya Warioba irudi mezani.
 
Back
Top Bottom