Mzee Warioba na hoja fikirishi ya Mwalimu Nyerere kutohutubia Kanisani

Mzee Warioba na hoja fikirishi ya Mwalimu Nyerere kutohutubia Kanisani

Yah angekuwa padre angesaidia kuokoa nafsi nyingi ambazo zingekuwa zipotee kama zisingekutana nae.

Cheo cha rais inabidi ujishushe siku zote. Utambue ukubwa wa madaraka uliyonayo vinginevyo watu wataumia.

Kwa hiyo kujishusha ndio huko kukwepa kuongelea madhabahuni?! Na fikiri kila kiongozi kati ya hawa 5 ambao walikuwa Marais wa JMT wanayo mazuri na mapungufu yao.

Huyo Mh Makongoro mwenyewe ungekutana naye early 1980s asingeweza mzungumzia Baba yake kama anavyomzungumzia leo akiwa anatembelea nyota yake.
 
Nadhani huu uhuni wa kutumia mimbari za nyumba za Mungu kutoa matamko ya kisiasa tumeanza kuuona kwa JK,kwa Mwendazake ilizidi! Yaani akipewa Mic ilikuwa ni kufoka mpaka kukashifu Watumishi wa Mungu!
Mhe. Majaliwa naye mskitini alihutubia na kusema Rais Magufuli mzima wa afya anachapa kazi, kumbe....
 
Kwa hiyo kujishusha ndio huko kukwepa kuongelea madhabahuni?! Na fikiri kila kiongozi kati ya hawa 5 ambao walikuwa Marais wa JMT wanayo mazuri na mapungufu yao.

Huyo Mh Makongoro mwenyewe ungekutana naye early 1980s asingeweza mzungumzia Baba yake kama anavyomzungumzia leo akiwa anatembelea nyota yake.
Madhabahu ni mahali pa viongozi waliowekwa wakfu kufundishia waumini maisha ya kiroho. Wewe kusoma seminari haina maana kuwa tayari umeshakuwa mpakwa mafuta.

Haikuleta picha nzuri kiongozi wa kiserikali kuongea ndani ya kanisa tena wakati mwingine akiwakashifu hao hao viongozi waliomkaribisha!.
 
Naona wengi wenu bwana Phillipo Bukililo nmapitia The Epiphany Moment, na kuanza kujirudi kuwa binadamu waungwana. Mkubali au mkatae, mlikuwa mnaunga mkono udhalimu ambao ungeenda kuligawanya hili taifa letu. Nafurahi kuona busara za Mzee Warioba zimekufanya ujifikirie na kurudi kwenye mstari. Awamu ile usingekubaliana kabisa na hizi hoja za Mzee Warioba.......
 
Madhabahu ni mahali pa viongozi waliowekwa wakfu kufundishia waumini maisha ya kiroho. Wewe kusoma seminari haina maana kuwa tayari umeshakuwa mpakwa mafuta.

Haikuleta picha nzuri kiongozi wa kiserikali kuongea ndani ya kanisa tena wakati mwingine akiwakashifu hao hao viongozi waliomkaribisha!.

Kila aliye mpokea Bwana Yesu na kuokolewa au kupata Wakovu ni mpakwa mafuta pamoja na Bwana Yesu kupitia Roho Mtakatifu. 2 Wakorintho 1:21-22. Hivyo wanaruhusiwa kuwarudi watumishi wa madhabahuni baadhi yao walio kengeuka kwa dhahiri mbele ya macho ya jamii.

Huwezi kusikia mahubiri yenye ukweli wa aina hii mara kwa mara madhabahuni kwa vile yatawafumbua kondoo akili walizoshikiliwa kwa kutumia mafundisho ya Agano la Kale juu ya wapakwa mafuta wa Bwana. Kinacho sikika zaidi ni Viongozi wa madhabahuni kuwa omba waumini wa waombee kushinda majaribu. Unaombewa vipi na ambaye hajaokoka na kupakwa mafuta??
 
Kila aliye mpokea Bwana Yesu na kuokolewa au kupata Wakovu ni mpakwa mafuta pamoja na Bwana Yesu kupitia Roho Mtakatifu. 2 Wakorintho 1:21-22. Hivyo wanaruhusiwa kuwarudi watumishi wa madhabahuni baadhi yao walio kengeuka kwa dhahiri mbele ya macho ya jamii.

Huwezi kudikia mahubiri ya yenye ukweli wa aina hii maramara madhabahuni kwa vile yatawafumbua kondoo akili walizoshikiliwa kwa kutumia mafundisho ya Agano la Kale juu ya wapakwa mafuta wa Bwana. Kinacho sikika zaidi ni Viongozi wa madhabahuni kuwa omba waumini wa waombee kushinda majaribu. Unaombewa vipi na ambaye hajaokoka na kupakwa mafuta??
Ni ishara ya ukosefu wa unyenyekevu. Kwamba anaweza kuongea popote mahali popote na asifanywe kitu.

Ni kiburi cha mamlaka.
 
Ni ishara ya ukosefu wa unyenyekevu. Kwamba anaweza kuongea popote mahali popote na asifanywe kitu.

Ni kiburi cha mamlaka.

Sio kweli Pazia la Patakatifu pa Patakatifu lilisha chanika/pasuka Bwana Yesu alipoangikwa pale Msalabani hivyo yeyote aliye mpokea Bwana Yesu kuwa Mwokozi wake ana accsses ya Patakatifu pa Patakatifu. Labda useme JPM alikuwa haongelei mambo ya maadili ya Mungu hapo madhabahuni.
 
Alikua mungu mtu yaaani one man show. Anajua kila kitu uganga uchawi kanisani udaktari ufundi aisee 🙌🏻🙌🏻🙌🏻 kwa ufupi alikua raisi wa hooovyoooooo kuwahi kutokea na mshamba mni
Tatizo la magufuli ilikuwa anajiona anafahamu kila kitu. Alivuka mipaka sana kwenye hili jambo. Mbaya zaidi alikuwa anawapa maagizo watumishi wa Mungu akiwa madhabahuni. Wote tumeuona mwisho wake.
 
Sio kweli Pazia la Patakatifu pa Patakatifu lilisha chanika/pasuka Bwana Yesu alipoangikwa pale Msalabani hivyo yeyote aliye mpokea Bwana Yesu kuwa Mwokozi wake ana accsses ya Patakatifu pa Patakatifu. Labda useme JPM alikuwa haongelei mambo ya maadili ya Mungu hapo madhabahuni.
Pamba uwezavyo kwa kila kifungu unachokifahamu cha Biblia, lakini JPM alikosea kuongea madhabahuni. Kuishia seminari sio kigezo cha kuitumia mimbari kuonyesha muelekeo wa serikali yake.
 
Pamba uwezavyo kwa kila kifungu unachokifahamu cha Biblia, lakini JPM alikosea kuongea madhabahuni. Kuishia seminari sio kigezo cha kuitumia mimbari kuonyesha muelekeo wa serikali yake.

Atleast mbele za Mungu JPM hatajibu kwa Mungu wake kwa nini watu aliowaongoza waliacha kumtegemea Mungu wakategemea barakoa. Hilo swali halitamuhusu. Alisitiza wazi kumtegemea Mungu wa Mbinguni kwa kila jambo na kumuweka wa Kwanza kwa kila kitu.
 
Nyerere alikuwa msomi wa falsafa, kamsoma John Stuart Mill Edinburgh Scotland na kumuandikia papers, anajua separation of church and state ni nini.

Ndiyo maana hakuhubiri kanisani.

Kuhusu humility, kuna siku Mama yangu alivyokuwa anafanya kazi Ikulu, alikuwa anakata kona kwenye corridor moja ya Ikulu. Ikawa bado kidogo agongane na Nyerere uso kwa uso, kwa sababu hakumuona kwenye kona.

Basi Mama akawa ameogopa sana akaona atakaripiwa na Nyerere. Akaja kumkuta Nyerere mwenyewe ndiyo yuko so concerned kuhusu hali ya Mama, alimuona Mama kama kapanic hivi, Nyerere akawa anamtuliza anamuuliza kama yuko poa.

Nikasema, mtu mwenye cheo kikubwa anavyo ji conduct akiwa peke yake na staff wake inaonesha mambo mengi sana kuhusu integrity yake.

In this capacity, Nyerere was the consummate gentleman.
Mkapa aliifuata hiyo tabia, mnapishana tu mle ndani kawaida tu.
 
No offence hii stori hujamaliziwa mkuu,nyerere mtu mbad
 
Mkapa aliifuata hiyo tabia, mnapishana tu mle ndani kawaida tu.

Mnapishana kichwa kimejaa Yohana Mtembezi lazima uonepoa tu unasogelea Madhabahu katika hali hiyo na unaona ndio ustaarabu na kustarabika kwenyewe huko.
 
Mnapishana kichwa kimejaa Yohana Mtembezi lazima uonepoa tu unasogelea Madhabahu katika hali hiyo na unaona ndio ustaarabu na kustarabika kwenyewe huko.
Ballantine ndugu, sijawai kumuona na john mtembezi labda JD.
Na sijawai kuona kalewa.
Tuwe na heshima hapo.
 
Ballantine ndugu, sijawai kumuona na john mtembezi labda JD.
Na sijawai kuona kalewa.
Tuwe na heshima hapo.

Waulize wakongwe wa JF watakuibulia nyuzi inayo zungumzia kutembelewa kwa na Mwl usiku hapo mahakama ya samaki.
 
Nilimsikiliza vyema Waziri Mkuu mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba pale alipopewa nafasi ya kuhutubia nyumbani kwa Mwalimu Nyerere pale Msasani kama sehemu ya sherehe ya kufikisha miaka 100 ya hayati Mwalimu.

Aliongea kwa lugha nzuri kama mwanasheria na mtu muungwana. Akamuelezea Mwalimu Nyerere jinsi alivyokuwa akimfahamu tangu alipokuwa kijana kabisa. Tukumbuke kuwa mwaka 1961 Mzee Warioba alikuwa ni mmoja wa vijana waliokuwepo pale uwanja wa Uhuru siku ya tarehe 9 mwezi Desemba. Hivyo anamfahamu vyema hayati Mwalimu.

Akiwa anaendelea kujenga hoja ya unyenyekevu(humility) wa hayati Baba wa Taifa akaongelea suala moja lililoniacha nikiwa nimezama katika fikra nyingi aple aliposema kuwa Mwalimu Nyerere hakuwahi hata mara moja kuhutubia kanisani.

Nikaona kamera ikizungushwa na akaonyeshwa Amani Karume mdogo wake na rais wa zamani wa Zanzibar, macho yake yakawa yanatazama juu hewani kama alikuwa na mawazo fulani yaliyomjia kichwani muda huo.

Kwamba Mwalimu Nyerere alipenda mno kujishusha na hakulewa na madaraka.Siku zote alikuwa tayari kujiweka katika nafasi ya mtu wa kawaida pasipo uwepo wa dalili wala viashiria vya makuu, ni kama Mzee Warioba aliamua kusisitiza kwa viongozi wa sasa waendelee kujishusha wawe ni watu wa kawaida wasiwe ni Miungu watu.

Nikakumbuka miaka ile ya 1980 pale kanisani Saint Joseph Hayati Baba wa Taifa alikuwa siku moja moja akipenda kusali. Kilichokuwa kikituonyesha kwamba yeye ni rais ni kwamba kile kiti chake kirefu kilikuwa kikikaliwa na watu watatu tu. Yeye mwenyewe katikati kushoto mlinzi mmoja na kulia mlinzi mwingine. Hakuwa na mbwembwe za kutaka kupewa kipaza sauti wakati misa ikiwa inaendelea ili eti aanze kutoa maagizo mle mle kanisani.

Hoja kama hii ya Warioba ni nzito na pengine katika utu uzima wake alionao kwa sasa ni wakati muafaka kufikisha ujumbe kama ule ule aliousema Askofu Niwemugizi kwa Samia kule Kagera. Kwamba cheo chako kipo leo na kesho kinakwenda kwa mtu mwingine, hivyo tumia busara siku zote katika maamuzi yako.

Nakumbuka JK katika kumuongelea akasema kitu alichojifunza kwake ni kauli yake kwamba hoja hujibiwa kwa hoja na siku zote haipigwi bunduki. Kutoipiga bunduki hoja ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujifanya wewe ni wa kawaida tu hata kama yanayosemwa dhidi yako yanaiumiza nafsi yako.

Pia ni kama ile picha maarufu ya Bilionea Bill Gates aliyoipiga akiwa kapanga foleni huko USA kavaa jeans yake kama vile ni mtu wa kawaida tu.

Anajishusha na kutojikweza siku zote, jaribu kumuweka Gates na pesa zake na ushawishi wake katika nafasi ya hawa matajiri wanaomiliki mabasi ya mikoani na vituo kadhaa vya kuuza petroli, namna wanavyotaka wanyenyekewe kama vile wao ndio wanaowapa binadamu wengine uhai na kuuondoa!.

Tutamkumbuka sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu wa kawaida mwenye ucheshi mwingi na busara nyingi. Lakini ndani kabisa ya nafsi yake akiwa mtu wa kawaida kabisa.

Ukikutana nae pale ikulu katika zile koridoo karibu na yule Simba aliyekaushwa miaka ile anakuwekea mkono kichwani na kukuuliza hujambo mwanangu!?. Ni kama jana tu lakini inakaribia miaka 40 sasa.
Magufuli aliidhihaki sana madhabahu... hata ingekua madhabahu ya nini ile kitu huwa haidhihakiwi... unaiba chaguzi... unaua watu na kushiriki uchawi bado unasimama madhabahuni kudhihaki? Yule jamaa alijiandalia kifo chake.
 
Kifupi warioba kakulia kwenye eneo la usabato

Mkewe Evelyn Ojjiki ni msabato hasa

Wasabato na siasa kanisani mbali kabisa nje fanya sio kanisani .Mkewe ndie kam shape kwenye hilo

Apigiwe mkewe makofi ya hongera kwa kumshikisha adabu kuwa siasa fanya nje ya kanisa sio ndani ya kanisa

Hongera mama Evelyn Ojjiki kwa kazi umefanya credit zije kwako sio kwa warioba wala Nyerere
Yule mchawi wenu JIWE aliikanyaga sana madhabahu
 
Mama Ana Mwansansu Aliyeongea juzi nyumbani kwa Mwalimu Nyerere unamkumbuka vizuri?. Alikuwa anaishi nyuma ya eneo walilokuwa wanaishi wale tausi, nyumba yake ikitazamana na bahari na kulia kwake ndio soko la feri.
We unamjua?
 
Back
Top Bottom