Mzee Warioba na hoja fikirishi ya Mwalimu Nyerere kutohutubia Kanisani

Mzee Warioba na hoja fikirishi ya Mwalimu Nyerere kutohutubia Kanisani

Magufuli alipoanza kuhutubia vijimambo kila alipoenda kusali, nilimtonya rafiki yangu mmoja nikamwambia , huyu jamaa hajui anafanya nini.
Na nilijisemea tu kuwa madhabahu itamwadhibu, pale si mahali pa mizaha.

Mtu asiye na roho wa Mungu huwa haelewi kuwa madhabahu zinawekwa wakfu na ni mahali pa waliowekwa wakfu vile vile.
Tatizo la magufuli ilikuwa anajiona anafahamu kila kitu. Alivuka mipaka sana kwenye hili jambo. Mbaya zaidi alikuwa anawapa maagizo watumishi wa Mungu akiwa madhabahuni. Wote tumeuona mwisho wake.
 
Tatizo la magufuli ilikuwa anajiona anafahamu kila kitu. Alivuka mipaka sana kwenye hili jambo. Mbaya zaidi alikuwa anawapa maagizo watumishi wa Mungu akiwa madhabahuni. Wote tumeuona mwisho wake.
Kiburi ikifikia kiwango cha kuongea mizaha madhahabuni, mwisho wa mtu huyo ni karibu lakini huwa hajijui.
 
Nilimsikiliza vyema Waziri Mkuu mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba pale alipopewa nafasi ya kuhutubia nyumbani kwa Mwalimu Nyerere pale Msasani kama sehemu ya sherehe ya kufikisha miaka 100 ya hayati Mwalimu.

Aliongea kwa lugha nzuri kama mwanasheria na mtu muungwana. Akamuelezea Mwalimu Nyerere jinsi alivyokuwa akimfahamu tangu alipokuwa kijana kabisa. Tukumbuke kuwa mwaka 1961 Mzee Warioba alikuwa ni mmoja wa vijana waliokuwepo pale uwanja wa Uhuru siku ya tarehe 9 mwezi Desemba. Hivyo anamfahamu vyema hayati Mwalimu.

Akiwa anaendelea kujenga hoja ya unyenyekevu(humility) wa hayati Baba wa Taifa akaongelea suala moja lililoniacha nikiwa nimezama katika fikra nyingi aple aliposema kuwa Mwalimu Nyerere hakuwahi hata mara moja kuhutubia kanisani.

Nikaona kamera ikizungushwa na akaonyeshwa Amani Karume mdogo wake na rais wa zamani wa Zanzibar, macho yake yakawa yanatazama juu hewani kama alikuwa na mawazo fulani yaliyomjia kichwani muda huo.

Kwamba Mwalimu Nyerere alipenda mno kujishusha na hakulewa na madaraka.Siku zote alikuwa tayari kujiweka katika nafasi ya mtu wa kawaida pasipo uwepo wa dalili wala viashiria vya makuu, ni kama Mzee Warioba aliamua kusisitiza kwa viongozi wa sasa waendelee kujishusha wawe ni watu wa kawaida wasiwe ni Miungu watu.

Nikakumbuka miaka ile ya 1980 pale kanisani Saint Joseph Hayati Baba wa Taifa alikuwa siku moja moja akipenda kusali. Kilichokuwa kikituonyesha kwamba yeye ni rais ni kwamba kile kiti chake kirefu kilikuwa kikikaliwa na watu watatu tu. Yeye mwenyewe katikati kushoto mlinzi mmoja na kulia mlinzi mwingine. Hakuwa na mbwembwe za kutaka kupewa kipaza sauti wakati misa ikiwa inaendelea ili eti aanze kutoa maagizo mle mle kanisani.

Hoja kama hii ya Warioba ni nzito na pengine katika utu uzima wake alionao kwa sasa ni wakati muafaka kufikisha ujumbe kama ule ule aliousema Askofu Niwemugizi kwa Samia kule Kagera. Kwamba cheo chako kipo leo na kesho kinakwenda kwa mtu mwingine, hivyo tumia busara siku zote katika maamuzi yako.

Nakumbuka JK katika kumuongelea akasema kitu alichojifunza kwake ni kauli yake kwamba hoja hujibiwa kwa hoja na siku zote haipigwi bunduki. Kutoipiga bunduki hoja ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujifanya wewe ni wa kawaida tu hata kama yanayosemwa dhidi yako yanaiumiza nafsi yako.

Pia ni kama ile picha maarufu ya Bilionea Bill Gates aliyoipiga akiwa kapanga foleni huko USA kavaa jeans yake kama vile ni mtu wa kawaida tu.

Anajishusha na kutojikweza siku zote, jaribu kumuweka Gates na pesa zake na ushawishi wake katika nafasi ya hawa matajiri wanaomiliki mabasi ya mikoani na vituo kadhaa vya kuuza petroli, namna wanavyotaka wanyenyekewe kama vile wao ndio wanaowapa binadamu wengine uhai na kuuondoa!.

Tutamkumbuka sana Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu wa kawaida mwenye ucheshi mwingi na busara nyingi. Lakini ndani kabisa ya nafsi yake akiwa mtu wa kawaida kabisa.

Ukikutana nae pale ikulu katika zile koridoo karibu na yule Simba aliyekaushwa miaka ile anakuwekea mkono kichwani na kukuuliza hujambo mwanangu!?. Ni kama jana tu lakini inakaribia miaka 40 sasa.
Kwanza tufute lile jina Mhe kwa viongozi wote ibaki ndugu
 
You should have seen the pain portrayed by Magufuli's assistants the day he was pronounced dead; you then would have realized how much they revered him! Hakuna Rais anayechukiwa na watu wanaofanya kazi IKULU!
Ulikuwa ni usanii tupu, hata mimi ningeonyesha huzuni sababu kifo hata akifa kichaa lazima utapata huzuni lakini kimoyo moyo watu walifurahi sn
 
Kutaka kumgonga Rais kwenye ciridor ni uzembe mkubwa sana.

Kule China mngefunga turubai siku hiyo hiyo!
Hata kwa huyu
1650794378372.png
 
Tatizo la magufuli ilikuwa anajiona anafahamu kila kitu. Alivuka mipaka sana kwenye hili jambo. Mbaya zaidi alikuwa anawapa maagizo watumishi wa Mungu akiwa madhabahuni. Wote tumeuona mwisho wake.
Kiburi kibaya sana na ukianza kuwakwaza mapadre na maaskofu ndani ya eneo lao la uongozi wa kijamii tena mahali pale pale wanapohubiri, you are in for a blind and a destructive fate.
 
Kiukweli siipendi CCM, ila Mwalimu Nyerere namkubali sana kama Kiongozi mahiri, na Baba wa Taifa la Tanzania.
CHADEMA hawampendi na Wala siyo wafuasi wa Mwalimu Nyerere lakini wanaishi kinafiki tu kwasababu wanahisi watapoteza kukubalika kama wataonesha wazi suala Hilo.
 
Mimi nafikiri washauriwe wajikite kwenye huu mchakato wa kumfanya Mwl kuwa Mtakatifu wa Kanisa Katoliki la Mitume haya mengine waachane nayo.

Mwl Nyerere akiongea na wazee wa Daisalamu wakati flani alisimulia mambo aliyo ya fanya hadi alivyozikwa kaburini akiwa mzima huko Bagamoyo. Labda dhamira yake haikumtuma kusimama madhabahuni na kuongelea hapo. Pengine kwa kufanya hivyo angeharibu masharti na kuwudhi wale waliomzika mzima mzima. JPM alitaka kuwa Padri unaona tofauti hapo.
 
Nyerere alikuwa msomi wa falsafa, kamsoma John Stuart Mill Edinburgh Scotland na kumuandikia papers, anajua separation of church and state ni nini.

Ndiyo maana hakuhubiri kanisani.

Kuhusu humility, kuna siku Mama yangu alivyokuwa anafanya kazi Ikulu, alikuwa anakata kona kwenye corridor moja ya Ikulu. Ikawa bado kidogo agongane na Nyerere uso kwa uso, kwa sababu hakumuona kwenye kona.

Basi Mama akawa ameogopa sana akaona atakaripiwa na Nyerere. Akaja kumkuta Nyerere mwenyewe ndiyo yuko so concerned kuhusu hali ya Mama, alimuona Mama kama kapanic hivi, Nyerere akawa anamtuliza anamuuliza kama yuko poa.

Nikasema, mtu mwenye cheo kikubwa anavyo ji conduct akiwa peke yake na staff wake inaonesha mambo mengi sana kuhusu integrity yake.

In this capacity, Nyerere was the consummate gentleman.
Mama Ana Mwansansu Aliyeongea juzi nyumbani kwa Mwalimu Nyerere unamkumbuka vizuri?. Alikuwa anaishi nyuma ya eneo walilokuwa wanaishi wale tausi, nyumba yake ikitazamana na bahari na kulia kwake ndio soko la feri.
 
Hawa kinamama wengine vigumu kuwakumbuka, tulikuwa wadogo sana.
 
Naomba kusahihisha yafuatavyo kwani wabongo nyie ni wazuri sana katika kupotosha vitu ;
Amani Karume si mdogo wa Rais wa zamani wa Zanzibar bali ni Mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume.
Msemo wa JK ni kuwa " Hoja haipigwi rungu" na siyo " Hoja haipigwi bunduki"!
Tuepuke distortion kwenye mambo ya msingi ili kuonyesha umakini wetu.
 
Asante sana Fumadilu ni Ali Karume balozi wa zamani wa Tanzania nchini Ujerumani ni makosa ya uandishi.

Na huo msemo wa JK pia asante kwa kurekebisha, ni makosa yale yale ya uandishi ingawa walio wengi hayo hawajayatazama sana, wameangalia mantiki ya kilichoandikwa.
 
Mimi nafikiri washauriwe wajikite kwenye huu mchakato wa kumfanya Mwl kuwa Mtakatifu wa Kanisa Katoliki la Mitume haya mengine waachane nayo.

Mwl Nyerere akiongea na wazee wa Daisalamu wakati flani alisimulia mambo aliyo ya fanya hadi alivyozikwa kaburini akiwa mzima huko Bagamoyo. Labda dhamira yake haikumtuma kusimama madhabahuni na kuongelea hapo. Pengine kwa kufanya hivyo angeharibu masharti na kuwudhi wale waliomzika mzima mzima. JPM alitaka kuwa Padri unaona tofauti hapo.
Yah angekuwa padre angesaidia kuokoa nafsi nyingi ambazo zingekuwa zipotee kama zisingekutana nae.

Cheo cha rais inabidi ujishushe siku zote. Utambue ukubwa wa madaraka uliyonayo vinginevyo watu wataumia.
 
Back
Top Bottom