Mzee Warioba: Siyo lazima Mbunge aitwe Mheshimiwa

Hata huyu enzi zake aliitwa mheshimiwa. Asiwe na wivu kwa waheshimiwa wa sasa
 
Huyu babu bado yupo vizuri sn kichwani na bado ana kumbukumbu nyingi sema CCM wanaweza kumtafuna any time
 
Du hongera mkuu
 
Wapuuzi kama wewe bado mpo wengi sn Tz
 
Waheshimiwa walikuwa zamani sio hawa wa siku hizi kwani 'wengi wao' hata matendo yao ndani na nje ya mjengo hayana maadili.
Angalia hata miswada waliyotunga hasa kipindi cha 'huyu mtu' ni hovyo na isiyo na tija kwa wananchi zaidi ya ukandamizaji.
Wamebaki kutetea matumbo yao na sio ya jamii iliyowapeleka huko!
Nashauri waitwe NDUGU kama zamani kama hawataki waache huo ubunge waje mtaani tupambane na hali zetu,
 
Nyerere hakuwahi kuitwa 'mtukufu rais', hiyo ya kuitana 'mtukufu' ilianzishwa wakati wa awamu ya pili.
Okay, ila ikaishia hapo hapo. Wakati huo Mzee Waryoba alikuwa akihudumu; kwanza kama PM na baadaye Waziri wa TAMISEMI. Kwa hiyo kwenye utawala huo walianzisha kuitana Mtukufu, mbona anapiga kelele kuhusu Mheshimiwa?
 
Naunga hoja yako mkono kwa 100%
 
Hapa umeongea ki emotional zaidi.
Mbunge Hana thamani mbele ya mjeda labda hao Askari wanaowabambikizia kesi.
M jwtz ni mtu mkubwa Sana.
Mbunge hawezi pigiwa salute na mjeda hujui unachokiongea Ila DC rc anasalimiwa
Hivi una akili kweli mpaka leo hujui kwamba hata jwtz ni askari pia !!!?
Mwanajeshi ni neno linatokana na maneno mawili yaani Mwana+Jeshi=Mwanajeshi
Majeshi ni kama Jwtz,Polisi,Magereza nk
Hivyo tuna tuna wanajeshi wa jeshi la wananchi(jwtz) Wanajeshi wa jeshi la polisi(Polisi) Wanajeshi wa Jeshi la Magereza (Magereza) nk
Wote hao wanaitwa askari hivyo hakuna utambulisho unaitwa sijui mwanajeshi bali wanatambulika kwa kuitwa Maafisa/Askari.
Nikimaanisha Afisa ni askari mwenye cheo kuanzia single star begani na askari ni rank and file yani kuanzia Private/constable/Wdr mpaka Rsm kama sijakosea
Nimekupa elimu uelewe uelimishe na wengine Soma katiba ibara 147 na ibara zake ndogo zote
 
Okay, ila ikaishia hapo hapo. Wakati huo Mzee Waryoba alikuwa akihudumu; kwanza kama PM na baadaye Waziri wa TAMISEMI. Kwa hiyo kwenye utawala huo walianzisha kuitana Mtukufu, mbona anapiga kelele kuhusu Mheshimiwa?
Better late than never, sioni ubaya wowote hapo kwani alichosema ni jambo la maana.
 
Si kweli kuwa hapa Tanzania Rais alikuwa akiitwa Mtukufu! Ni Kenya Rais Mzee Kenyatta alikuwa akiitwa Mtukufu lakini hapa Tanzania tulimwita Ndugu Rais Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…