Hekima ni Uhuru, hii inakuja kutuletea muktadha wa ELIMU 2.0 ambavyo 'ukasuku' wa visomo unaumbuliwa na uono fasaha wa mifumo, sura za mambo, mielekeo na vina vya tafsiri... Sasa unadhani utajuaje misingi ya uvumbuzi wa Maxwell Chikumbutsu kwa ELIMU 1.0 ya uhandisi wa Umeme, kwa mfano? Yeye ni mvumbuzi asiye 'msomi' katika jamii ya wasomi 'kasuku'--na hili ni majanga! Hakuna hata 'msomi' kasuku aliyejitokeza kuunga mkono jitihada zake-- walau hata kubayanisha ni namna gani uvumbuzi wake unaweza kujumuishwa katika maendeleo ya jamii yake... Ni >
wadau wachache kutoka nchi jirani na Zimbabwe<, na tena >
wengine kutoka Amerika< 'wamemshika mkono' kwa kuchangia mazingira ya urutubishaji wa tekinojia zake za 'nishati-huria' na utunzaji wa 'siri za uvumbuzi' kwa tekinolojia habari za 'blokucheni'... Nje ya haya, mdau wetu huyu katika maendeleo ya kitekinolojia kakwama...
Tunahitaji ELIMU 2.0 ili watu kama Maxwell Chikumbutsu, vumbuzi zao ziote mizizi na kustawi. Uhuni wa makuwadi wa ubeberu unatawala kwa kuwa sisi watu hatujui ilivyobora--tunahadaika kwa kudhani fedha ndiyo msingi wa maendeleo; badala ya kuthamini ufundi, mbinu za kazi na ubunifu. Wakati mmoja huwa tunasema 'pesa ni matokeo' lakini kiukweli >
kuna mahala 'tumevurugwa' na 'wahuni' na tena wataalam wetu 'waliokwama'<... Maxwell Chikumbutsu, yuko Zimbambwe, lakini tuna akina 'Chikumbutsu' hata hapa Tanzania hivi sasa... Ni vema akina 'Chikumbutsu' hawa waelewe: hawana msaada kupitia 'mtu' wala 'taasisi' katika ulimwengu ambao bado unasukumwa kwa ELIMU 1.0...
Ni bora wafanye bidii katika ELIMU 2.0 iliwasiingie kwenye mitego ya hadaa za jitihada kwa kupata 'haki za uvumbuzi' ama 'ndoto' za 'utajiri/umaarufu' katika uwekezaji na mitaji utokanao na bidhaa za uvumbuzi husika. Walau Rais wa Zimbabwe anaweza kudhani kamsaidia Chikumbutsu kwa >
kuutandaza mtandao wa ngamuzi kwa ajili ya vitovu vya blokucheni< -- ili hata ikiwa atadhurika, habari za uvumbuzi wake haziwezi kupotea, lakini hili kiufundi si ujanja sana. Huko duniani 'wahuni' tayari wanakila aina ya >
'suluhu' na tekinolojia< na basi shida yao wala si 'Uvumbuzi wa Chikumbutsu'; shida yao ni kuthibiti 'mapinduzi' kabla ya wao 'kuruhusu'... >
'Wahuni' wanao uwezo wa kubangua mtandao wa blokucheni yoyote<, ila wanajikausha... Sana sana wanatega 'mtama kwa watoto', kujidai kuachia tekinolojia za 'sarafu-kripto' na blokucheni na kumbe hilo ni 'farasi la Trojani'...