Phewww
Hili linaweza kuwa swali la kipuuzi...
Je, hata kama Chikumbutsu angeonekana anaendesha gari, kana ni gari ya kutumia umeme, na kumbe ni gari inayotumia utundu mwingine wakinishati na uwezo--utajua tu kwa kutazama kwenye 'Youtube'?
HAPANA, tabia ya kuwa mpondeajipondeaji inaweza kuwa nasibu ya yote mawili, (1) kutengeneza mazingira ya Udadisi ili kuchimbua ukweli wa jambo, ama (2) Kutokubaliana na shauri la mwingine linaloweza kuwa 'limekuzidi kimo' na halafu hauna nidhamu kibinafsi iliyobora ili ku-JUA ilivyobora...
Daima ni vema kuwa na 'kiasi', hata katika 'upinzani'; kwa kuwa 'Dunia ina Mengi'... Kuna mengi kwenye 'Sayansi' huenda hayako kama unavyofundishwa khasa 'Darasani'--iwe ulichofundishwa kuanzia shule ya msingi hata chuo kikuu, Je, utajua?
Haya hufahamika kwenye 'Ugani tu'... Daima ni 'Siri za Kambi'... Tekinolojia ina mengi ya namna hii... Ikwa unaamini sana mambo ya 'Sheria ya Ujihifadhi wa Nguvu za Kinishati'--Jiulize 'Nishati' ni kitu gani khasa?
Mambo ya 'Nishati' ni kabila moja na 'Shauri la Mungu'...
Kama vile kwenye Mashauri ya Dini kuna shauri la 'NENO', kwenye sayansi kunaibuka nadharia ya khabari--'
Information Theory', Je, kuna uhusiano gani wa 'khabari' na 'nishati' kwa mfano?
Noumenoni ya M(i)uundo, simetria na umodelishi ni jambo linaloweza kupitiliza nadharia za 'nishati' na 'Sura' za mambo--kutoka ukawaida kuelekea usikawaida...
Kama huu unaivu wa kupondeapondea, ungebaki kwenye akiba ya maneno, basi kuna mashauri yangeweza kufikiwa ilivyobora... Kwa mfano, kwa nini uvumbuzi wa Chikumbutsu 'uuzie nyago' kuhusiana na magari tu?
Kiukweli khasa wa mambo, tekinolojia ya Chikumbutsu inaweza kutumika hata kwenye vyombo vidogo vya uchukuzi kama baiskeli, pikipiki, guta na hata mikokoteni...
Siku za mbele, ndani ya miaka 15 kuanzia hii 2025, hii tekinolojia ya ZPE (Tekinolojia ya Chikumbutsu) inakwenda hata kutumika kutengeneza vyombo vinavyoelea hewani--hata mikanda tu ambayo mtu anaweza kuvaa na akawa na uwezo wa kuelea--hata viatu vya uwezo huu. Hill hutalisikia kwa sasa, lakini ni bora ufahamu kujua haya yote ni mawezekano na labda kuna wengine hapa hapa Duniani tayari hivi ni vitu wanaishi navyo kila siku...
Sasa, Mambo ya 'Utomaso' yana faida na Khasara yake; kuna namna siyo ujanja kivile...