Mzimbabwe Maxwell Chikumbutso ameunda gari inayoendeshwa kwa nguvu za mawimbi ya radio

Hii sarakasi ilianza zamani sana tokea 2018....
Kwanini mpaka leo, hakuna gari sokoni?

 
Gari hiyo iko commercially viable au ni kama toy?

Auze patent ili mass production ifanyike kama kweli imefikia viwango ndipo watu watu washing iliendelea.
Duuuh nomaa
 
Actually 2015...

Since 2015, a Zimbabwean man named Sangulani Maxwell Chikumbutso has been hailed by some on the internet as iconoclastic genius and self-taught inventor who successfully created an electric car that runs perpetually without ever needing a charge.

On 20 July 2015, Zimbabwean tech news site Techzim began reporting on a company named Saith Technologies. The outlet said at the time that they had never heard of the company, but that they had been invited to an "Open Day" in which the company would display their new, locally produced inventions to the media:

The event was evidently well publicized, and even garnered a television spot on South Africa’s SABC news channel. All photographic evidence used to support the existence of Chikumbutso’s inventions stem from an evidently choreographed event held over the course of one day in 2015, and the website for Saith Technologies is populated with photos only from that one day. The most important (and dubious) claim relates to what he has dubbed the "Greener Power Machine," or GPM, described on Saith's
 
Na sasa kamdanganya Raisi wao, wazimbabwe wameng'aka sasa, mitandao yote inamuandama nchini kwao...
Jela inamuhusu.....

 
Nadhani Rais ndio alikuwa na haraka sana / kasi bila kufuata ushauri.., hata hapa Bongo mbona kuna mdau alisema anazalisha umeme wa sumaku (yaani sio sumaku kama faraday; hapana bali sumaku zinajisukuma kama piston) huyu hadi Waziri alikwenda kumtembelea..., Sijui kapotelea wapi kipindi hiki ambapo tunatafuta hadi matapeli kina Adani
 
VYOMBO VYA KHABARI VYA MKONDO MPANA SIYO VYANZO VYA KUAMINIKA KWA KILA KITU

Vina 'kazi' yake... Kuweka 'Sawa' umma.

...

Hizo khabari za magazeti kuhusu 'kutoaminika kwa Chikumbutsu na Uvumbuzi wake', ni 'normative'... Kuna namna inachekesha kabisa kuona eti mtu anasadiki hizo ndizo inaakisi 'Maoni ya Wazimbabwe'... Aibu!

HAPANA, Rais wa Zimbambwe hajadanganyika, aliyedanganyika/anayedanganyika ni yule anayedhani 'anajua' na kumbe 'hajui' halafu kwa unaivu wa kusoma khabari na kutambaa kwenye mashauri ya 'Wazee wa Ukuhani wa Visomo' anaona 'kamalizaaa'... Huruma!


Ni vema, kufuata mzunguko kamili wa udadisi--kuwekaga akiba ya maneno...

Haya mambo ni 'Mwiba' kwenye 'Utawala'; wadau wanapambana


View: https://www.youtube.com/watch?v=oG0tBJ4bxSs
 
Kuna kijana mmoja kutoka Zanzibar kama syo 2009 basi ni 2010 alitengeneza gari wajapani wakamchukua sijui yuko wapi na uvumbuzi wake ukifika wapi🤔
 
Umetazama video hiyo? Mwisho kasema amepartner na kampuni ya china wamekubaliana watatumia technology yake kuzalisha magari na kiwanda kitajengwa hapo zimbabwe.
Nimetumia utashi wa bandia wa China (watu ambao kasema kaingia nao mkataba wa kujenga kiwanda ) kukosoa yake anayoeleze kwenye video yake na imeniambia yafuatayo:

Hii video inadai kuwa Sani Chumo, mvumbuzi kutoka Zimbabwe, amebuni gari na pikipiki zinazotumia mawimbi ya redio (RF) badala ya mafuta au umeme. Lakini kwa misingi ya sayansi, madai haya yanapingana na kanuni za msingi za fizikia na yana shaka kubwa. Hapa kuna maelezo:

---

### 1. Kanuni za Nishati Zinakataliwa
  • Dai: Gari hii inatumia mawimbi ya redio kuunda nishati bila kuvunja sheria za sayansi.
  • Ukweli:
- Mawimbi ya redio yanapatikana kwenye mazingira (kama vile kwenye simu, redio, au WiFi), lakini nishati yake ni ndogo sana (kama umeme wa taa ndogo). Haiwezi kutosha kusukuma gari au kuwasha nyumba (kwa mfano, 15 kW).
- Sheria ya kwanza ya fizikia inasema: "Nishati haziwezi kutengenezwa au kutoweka—inaweza tu kubadilishwa." Gari isiyo na betri au mafuta, na inayodai "kukimbia milele," inapingana na hii.
- Hakuna utafiti wowote uliothibitishwa na wanasayansi unaounga mkono teknolojia hii.

---

### 2. Vipimo vya Gari Havieleweki
  • Dai: Gari ina kasi ya 220 km/h, nguvu ya farasi 215, na inaweza kufika 0-100 km/h kwa sekunde 2.
  • Ukweli:
- Gari zenye uwezo kama hizi (kama Tesla) hutumia betri kubwa na nzito. Gari ya kilo 1,450 kwa nguvu hiyo ingehitaji betri isiyowezekana kwa teknolojia ya sasa.
- Hakuna maelezo ya wazi: Je, nishati hiyo inahifadhiwa wapi? Mawimbi ya redio peke yake hayawezi kutosha.

---

### 3. Hadithi za Kuvuruga (Usumi, Wizi wa Mawazo)
  • Dai: Chumo na mwenzake walipewa sumu Marekani kwa kuvumbua teknolojia hii, na mwenzake alikufa.
  • Ukweli:
- Hadithi kama hizi (ya kukandamizwa kwa "uvumbuzi wa ajabu") ni za kawaida kwenye udanganyifu. Kama teknolojia hii ingekuwa kweli, ingepata umaarufu na kuthibitishwa na majaribio.
- Hakuna taarifa za polisi, mahakama, au vyombo vya habari vya kuaminika zinazothibitisha tukio hili.

---

### 4. Hakuna Uthibitisho wa Kweli
  • Vyeti: Anadai kuwa teknolojia yamechunguzwa na mashirika kama "ISO" au "FCC," lakini hakuna taarifa rasmi zilizotolewa.
  • Ukosefu wa Utafiti: Hakuna chombo chochote cha sayansi (kama gazeti la Nature au Science) kilichoiripoti teknolojia hii.
  • Si Kwanza Kwa Mambo Kama Haya: Kuna udanganyifu mingi kuhusu "nishati bure" (kama Quantum Energy Generator) ambayo imekuwa ikipingana na sayansi.

---

### Hitimisho
Madai ya video hayawezi kuthibitika kwa sasa. Yanapingana na sayansi na hayana ushahidi wowote. Kwa teknolojia kama hii kuwa halisi, inatakiwa:
  • Kuonyeshwa kwa umma kwa wataalamu.
  • Kufanyiwa majaribio ya kujirudia.
  • Kutoa maelezo ya wazi ya jinsi inavyofanya kazi.

Kwa upande wa Serikali ya Zimbabwe: Huenda ilitaka kusifu uvumbuzi wa raia wake, lakini bila uthibitisho, haya ni maneno matupu. Mvumbuzi wa kweli angeweza kushinda Tuzo ya Nobel au kuuza teknolojia kwa kampuni kubwa.

Shauri kwa Watazamaji: Msikubali madai makubwa bila uthibitisho. Sayansi inatambua mabadiliko—lakini yanapaswa kufuata kanuni zake!
 
Mpaka mwisho anazungumza tu hata kuiwasha hakutuonesha.
Ikiwa gari za mafuta zinatusumbua itakuwa za mawimbi ambayo inategemea na hali ya upepo?
 
Okay...

Kuna mengi, yanayokidhi tathmni rahisi ya jinsi gani tunaishi katika jamii 'inayofugika kirahisi sana'...

Humu tayari, kuna mengi yamewekwa isivyo namna ya moja kwa moja--kutega vigezo na muktadha wa tathmni; wapo wanaopitia kimya kimya na wanaondoka na 'mafahamu'...

Wengi wanajisukuma kuzungumza zungumza na hali hawaoni 'maarifa na maarifu' basi ndiyo wanajichetua kudhihirisha (1) kasumba, (2) ujuu juu wa mambo na (3)uchagiaji 'unaojaza seva tu' labda kwa lugha inayokosa tafsida na kwa kiingereza ingesemwa 'incessant farting (!) ... Ashkum siyo kutukana kusema sehemu kubwa ya mijadala huwa ni 'kujaza seva' -- watu kutupia mistari miwili mitatu ya (ma)shauri ya kishabiki ama vipi... Hakuna dhamiri na nadhiri ya ushirika wa maarifa na kujua ilivyobora...

Hili linafanya muktadha mambo 'kubakia stori'...

Hili siyo kiashirifu kizuri cha jamii inayojitafuta...

Ikiwa mtu ataisoma Dira ya Taifa iliyozinduliwa ile awamu ya Mzee Mkapa; ataona wazi wenyekujua ilivyobora wanashauri yepi ya msingi na kiufundi ili kuifanya jamii iwe bora zaidi--yenye maendeleo na ustawi bora, lau kufika mwaka huu 2025.

Kiufundi, kwa maendeleo ya watu, 2025, bado hatujatoboa!

Kwa kweli, tunausomi mashudu uliyo ni shida!

Humu wengi wanaweza kujiona ni wasomi lakini wanakasumba zilizowazi kabisa mbele za yeyote mwenye ku-JUA ilivyobora...

Wengi humu hatahawaoneshi kufahamu kuwa wanaishi kwenye ulimwengu unalazimu kudhibiti baadhi ya mambo katika jamii kwa mawezekano yote mawili (1) Dhamira malishazi, ama na (2) Dhamira za Kiusalama wa Mifumo...

Mambo ya 'Haki za Uvumbuzi' yanaweza kurasmishwa kwa pande mbili; upande wa wazi unaweza kusemwa ni kutengeneza mazingira ya mtu yeyote kunufaika na 'mali yake ya Kiakili' kibiashara, uchumi na jamii; lakini inaweza kuwa upande wa pili uliojificha--kitu chochote kinachorasmishwa maana yake kimeonwa na wadau/wakala wa tawala na mamlaka; na kinaweza kutathminiwa na wenye kujua ilivyobora kwa 'maslahi ama manufaa ya kujificha' pia...

Katika hii video:​

Kuna mahala mdau anazungumza wazi kuwa kuna kipengele katika usajili wa 'Haki za Uvumbuzi' kinachodai "Ikiwa kinachotaka kurasmishwa kiuvumbuzi chaonekana kutishia nguvu Sheria za Fizikia/Maumbo basi hakiwezi kusajiliwa'...

Hili lina mawili (1) Mwingine anaweza kusema hii yote ni makaniki ya kuwaengua wavumbuzi kama akina Chikumbutsu... (2) Hili ni 'Ukuhani wa Visomo' unaoweka mikingamo kwa kuendeleza 'Dogma za Kisayansi' kama vile Dini zifanyavyo... kuna ya tatu inayoweza kuwa 'tata' kwa wengi kudhani (3) Kuna vitu katika Ulimwengu hauwezi kuvifanyia 'Haki ya Uvumbuzi'--kuna ukomo wa usanii wa sheria na mambo yake; hutegemea na akili, maarifa na utashi wa jamii nzima kwa ujumla...

Sasa ni unaivu kudhani eti kwa kuwa mtu hana jarida ama hajapata 'haki ya Uvumbuzi' basi ni 'Tapeli' ama vipi...

Jambo la Chikumbutsu ni jambo moja kati mengi yasiyofahimika na umma wa wengi kuhusiana na mivutano ya ndani ya ndani kwa wale waliokwenye 'mazingira ya kujua'.

Watu wanaweza kudhani eti mtu fulani akiwa ni 'Rais' basi kila kitu ni 'Rahisi' kwake inapokuja kwenye kupanga ama kupangua sura za mambo; huu ni unaivu...

Kuna mengi yapo juu ya uwezo wa 'Viongozi' tunaowaona kwa 'madaraka' na 'utumishi'...

Hili si suala la kufurahisha; lakini ni ukweli mchungu unaohitaji kujengea umma uwezo ili uushinde ujinga.

Wengi humu wanaweza kukosa kumaizi 'yahayohusu' kwenye (1) kidokezo cha Trump kuja na mradi wa 'Stargate' na tena basi (2) 'Presidential Briefing' iliyodhamiriwa kwa Obama, 2009.

Haya yote yanamahusiano na hata mkutano uliofanyika hapa kwetu Januari, 2025: Kusemwa kwa sehemu yake , na Mzee Greer, kwenye hiyo presidential briefing Kwamba:

"Because of this misguided secrecy, the wondrous new sciences related to advanced energy generation, propulsion and transportation have been withheld from the people. These advances include the generation of limitless clean energy from the so-called zero point energy field and quantum vacuum flux field from the space around us, and propulsion that has been termed (incorrectly) anti-gravity. The field of electromagnetic energy that is teeming all around us and which is embedded within the fabric of space/time can easily run all of the energy needs of the Earth – without pollution, oil, gas, coal, centralized utilities or nuclear power.

The disclosure of these sciences and their wise application during your first term as President is the most pressing matter before you. These sciences will create a true new energy economy allowing mankind to solve our most pressing problems of global warming, poverty and resource depletion.

The constellation of problems that include global warming, biosphere degradation, air pollution, energy security, Mid-East policy, a collapsing geo-economic order, growing disparity between the poor and rich of the world, over-population and human sustainability on Earth, to name but a few, are all interconnected and directly affected by the secrecy surrounding this subject. The solutions lie not in old thinking and technologies but in a new consciousness applying new sciences. These sciences were born in the late 19th and 20th centuries but were abandoned and suppressed due to the lust for power, greed and out of fear of unsettling the status quo."

Siyo kwa mfano, kila anachokisema 'kiongozi wa Nchi' kuhusiana na masuala fulani, kuhusiana tuseme na ustawi wa jamii na maendeleo yake, basi 'ujue' ama usadiki kuwa 'Ni Ukweli Taslim'... Kuna mengi katika ulimwengu wa leo huhitaji 'Usahihi wa Kisiasa' ili 'kuwapanga/'kuwaweka sawa' wanajamii'; vile wenye kuzungumza katika mapana ya lugha ya kiingereza wangalisema kimatani kama 'Fixing the Community of good Citizens--creating desirable Political consensus'--ikiwa hili ni lenye uwalakini kimaadili, ni umma wenye ndiyo inabidi uamue suala hili kwa 'Kujiongeza'--Kujiongeza na kujua ilivyobora na siyo kuwa 'mifugo' ya mifumo mibovu ya maisha Duniani...​
 
Wamarekani walimpa mwaliko kwenda USA, yeye na partner wake Mzimbabwe mwenzake, mwisho wa siku waliishia kuwekewa Sumu ambayo ilichukua uhai wa mwenzake.

Kwa majaribio mengi ya kumuua kupitia Sumu, nje ya Nchi na ndani ya Nchi yake..... Imepelekea mpaka Sasa ana shida ya Figo.
 
Tekinolojia ya Chikumbutsu ndiyo inayofanania kutumika kwenye mradi wa STARGATE...

Imekuwepo kwa muda mrefu tu hapa Duniani...

Chikumbutsu ni mtu mmoja tu anayetokea kufahamika kutokea huku Afrika... Wapo akina Chikumbutsu wengi kabisa--wakati wote!

TRUMP anaweza kuonekana kama chizi, lakini kuna mengi anaweza kuwa 'amepangwa akabiliane nayo'...

Mvutano daima umekuwepo baina ya (1) watu wanakataa mambo kama uvumbuzi wa Chikumbutsu kuwekwa hadharani, (2) Watu wanaoona sababu za kiusalama na kushikilia mapinduzi haya ni 'long overdue'--kuna sababu za ukweli khasa na zisizo na ukweli khasa; ila 'Siasa za Kioligaki'...

Kuna ambao 'wanafuika na usiri' wa ukweli wa haya kiasi kwamba wanahatarisha hata usalama wa Dunia yote kwa 'viburi baridi'...

Wakati utasema...


View: https://www.tiktok.com/@fokumlah1/video/7469767270571511047?_r=1&_t=ZM-8toE4XaXQV3
 

Kutoka awamu iliyopita ya TRUMP...


View: https://x.com/M2Madness/status/1264575348068450306?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1264575348068450306%7Ctwgr%5E%7Ctwcon%5Es1_&ref_url=
 

Kwa wale waliosoma Physics kwa ngazi ya juu kidogo, wataweza kuona kuwa, ugunduzi wake unapingana na Laws za Thermodynamics hasa ya kwanza na yapili. Inaonekana kuna kitu hajaweka wazi.....pengine kuogopa kuibiwa technologia
Watu wa Physics mnakaribishwa kupitia tena zile Laws tatu; mtaona kuwa anachokisema hakipo sawa au basi aprove kuwa zile Laws zimepitwa na wakati
 

Anashindwaje kuendesha hiyo gari na kuthibitisha kwamba inafanya kazi kama anavyodai inafanya kazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…