Tetesi: Mzize asusa kusaini Yanga, Kutimkia Simba!

Tetesi: Mzize asusa kusaini Yanga, Kutimkia Simba!

Acheni kejeli sasa kama kumlipa hamuwezi...

Lini mmeanza kufanya evaluation ya thamani za wachezaji?

Sio nyinyi mlikuwa mnamlipa Makambo 7mls na hachangii chochote uwanjani?

Wakati huohuo mnamlipa Fei 4mls na alikua anafunga karibu kila mechi!

Najua kuna wachezaji wanalipwa vizuri kisa wametoka nje ila wanazidiwa ubora na Mzize kwa mbali sana...

Hii ligi haipaswi kuwafaidisha wageni tu, tuamke.
EValuation inafanyika siku zote na ndio tunayoweka kwenye mikataba.
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu.
Akae kwa kutulia.
Fei tulimlipa 4m kwa mkataba aliosaini na wanasheria wake.
Makambo naye 7m kwa mkataba, kama hutaki unasaini ili nini?

Yanga hatujawahi kulazimisha mtu kusaini.
 
Ipo hivi kaka, Mzize anajilinganisha na hawa pro kutoka Congo na Burkinabe, anajihisi anastahili kama wao.
Hajui mshahara wa Aziz Ki unakatwa kodi kubwa, anakatwa hela ya Visa na working permit wakate yeye hayo yote hana.
Ana demand Appatrment Masaki ambapo kodi ni milioni 5 kwa mwezi badala achukue chumba maeneo ya Temeke kwa laki 5 ni full house.
Tusubirie tuone movie itaishaje
 

Clement Mzize ambaye anadai kuzaliwa 2004 , yani sasa ana miaka 20 ambaye kwa sasa mkataaba wake na Yanga umeisha amegoma kusaini mkataba mpya.

Mzize amegoma mkataba mpya na anataka kupandishiwa dau.
Ikumbukwe Mzize alikuwa "afisa usafirishaji " -bodaboda Pale Igumbilo Iringa akivaa yebo yebo za Njano huku akiwa anaishi na mama yake mzazi maeneo ya Zizi la Ngombe.
Mzize akaonekana na ghafla akatua Yanga, baadae sasa inaonekana mabega yameanza kuzidi kichwa.

Yanga wanataka kumpa Mzize yafuatayo:
1. Mzize analipwa milioni 7 kwa mwezi.
2. Nyumba ushuani.
3. Gari na mafuta.
4. Milioni 200 ya usajili
NB : Hayo yote ameyagomea.

Matakwa ya Mzize:
1. Milioni 10 kwa mwezi.
2. Nyumba Masaki .
3. Iphone 15 Pro Max
4. Milioni 300 za usajili .

Simba ambayo imeamua kusajili makinda na Yanga imeamua kusajili "wastaafu" wameanza harakati za kumsajili Mzize kwa mshara wa milioni 11 na ada ya usajili ya milioni 300 na iphone 15 pro max elite .

Ubaya Ubwela.
Yan iPhone?😂
 
Jana Mzize katandika ball sio kitoto..akirekebisha mapungufu yake atafika mbali. Ni top striker kwa bongo
 
Kwani hana kipaji? Mkuu naona hapa tungejikita kujadili kipaji chake sio kazi yake ya zamani, hamna mtu anae okotwa "jalalani" timu yangu ya yanga sio charity organisation kwamba anasaidia watu bure, hapana eliona kwamba anamanufa kwake ndo maana elimleta na kumlipia hicho kias regardless his past history ya bodo bado.
Wote waliopo Jangwani wana vipaji, ,kama vipi aende tu.
 
Mzize apunguze wenge, halafu amrudie Kristo mambo yake yatanyooka.
 

Attachments

  • Clement Mzize.jpg
    Clement Mzize.jpg
    166.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom