Iko hivi, Afrika hatuna utamaduni wa kutambua mchango wa viongozi waliotangulia, always tunawaweka kama watu walioharibu nchi, hii hali ndio inapelekea nchi zetu kuzidi kuwa masikini kwa maana hatuna muendelezo.
Dos Santos kapambana kuibadilisha Angola iliyokuwa na umasikini pamoja na Vita ya wenyewe kwa wenyewe. Nusu ya utawala wa Dos Santos ulikuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Mara ya kwanza nafika Angola, Luanda 1996 hapakuwa vizuri sana na hii ilichangiwa na ukosefu wa amani ambapo SAVIMBI na kundi lake walikuwa wanahatarisha sana usalama.
Miaka ya 2000s ndio Angola ikachipukia na sasa ni moja ya nchi zenye chumi imara.
Rejea BOTSWANA, Rais mstaafu Bw. IAN KHAMA ambaye aliibadilisha Botswana kuwa nchi nzuri leo anaandamwa kwamba hafai, hakuwa Raia halisi, fisadi nk.
Afrika tuna ujinga mwingi sana vichwani, na hii huambukiza watu wengine kama wewe.
Leo hii ukipata URAIS utataka umshtaki Rais Samia, Kikwete nk bila kukaa nao na kuangalia namna bora ya kuendeleza nchi yenu.
AFRICA WILL ALWAYS BE POOR.