Hakuniuma, nilimpenda na ndio maana hata Avatar yangu miaka nenda rudi unamkuta Magufuli, nachukia ile approach ya kuona waliokutangulia hawajafanya kitu. Na hiyo ndio sumu inayotumaliza Afrika.
Lazima tujifunze kwenda mbele, tuache visasi, Dos Santos ametoka kwa amani tu, ameenda kujipumzikia, kulikuwa na haja gani kusakama watoto wake?
Angetumia njia sahihi katika kurejebisha pale ambapo Dos Santos alifanya vibaya. Yes na nimekumbuka Msumbiji wako Njema sana katika kujenga nchi yao, hawatengani wanajadiliana kama marais kwa manufaa ya nchi.
Ukija kuelewa ninachokisema hapa utaona ni kwa jinsi gani imeathiri sana maendeleo ya nchi zetu.
Cardless, mimi nimekuelewa, ila sijui na mimi kama wewe umenielewa, Na chukia mno looting inayofanywa na viongozi wa Kiafrika, tuna miaka zaidi ya Sabini toka tujipatie uhuru kwa Wakoloni, lakini nchi nyingi ni kama tunazunguka mduara tu! Vicious circle of poverty! Na ukiondoa sababu za nje ambazo hatuna control nazo, sababu za ndani ni viongozi kama Dos Santos. Kafanya yale yale waliofanya kina Mobutu, Bokassa na kina Sani Abacha.
Napenda kukutarifu nimetembea Cardless, ufahamu wangu wa Nchi za Kiafrica si haba, na kwa taarifa yako hata sasa tunapowasiliana siko Tanzania. Naujua umaskini wa Waafrika ambao huwezi kabisa kuwalaumu wazungu! Kwa mtazamo wako unataka viongozi waliondoka Madarakani hata kama wamefanya mabaya wawe treated with kid gloves, with respect! Hapo naomba tutofautiane! Ni respect gani unaweza kuwapa watu kama kina Mobutu na kundi kama hilo, au akina Jacob Zuma! Ni kweli wametutoa mbali, lakini tena wakatupeleka kungine kabisa...tumeruka mkojo.....Unaiona Zaire, Chad, Equorial Guinea nk.
Huewezi kwenda mbele kwenye lolote lile kama kiongozi bila kuaangalia kwanza umefikaje hapo, kuna mambo utabadilisha kabisa, kuna mambo utayaendeleza, na kuna mambo utaondoa kabisa, na mengine utaanza upya. Naona wewe unataka tuendelee mbele bila kuangalia wapi tulipojikwaa. Mimi na msimamo wa kuangalia wapi nilipojikwaa kama nimeshindwa kufika nilipofika! Nadhani na Rais Joao Laourence amengalia wapi Angola ilipojikwaa, Kwa nini Angola imefika hapo! Wewe unaona wamefika mbali, lakini kwa utajiri walionao wangefika mbali zaidi!
Kuna watu wengi wameandika kuhusu umaskini wa nchi za kiafrika na jinsi ya kuondoka nao, ni wanazuoni toka nchi mbali mbali na hata Waafrika wenyewe, mojawapo ya sababu ni viongozi wa nchi za Kiafrika kuwa ni wafujaji wakubwa. Soma
The State of Africa: A History of Fifty Years of Independence- Meredeth, ni muda umepita sasa toka kitabu hicho kitoke, mwandishi kajaribu kupitia kila nchi, unachoona tatizo la viongozi ni kubwa sana! Tafuta vitabu hata ambavyo ni current, na assessment zinazofanywa kuhusu bara letu, kwa kifupi Africa tuna matatizo, ni kila mwenye mapenzi mema na bara letu lazima aumize ubongo kipi kifanyike, na kujaribu kutoa mchango wake kadri ya nafasi yake inamvyomuwezesha.
Shukrani!